Kamati za bunge zifutwe!

Hizi kamati za bunge ni deal. Mwenye dau kubwa anatetewa asiye na dau anateketezwa! Kamati zinaanza kupteza uhalali kwa kujiingiza katika utendaji wa serikali ndio maana hata maoni yao hayazingatiwi. Wanajulikana wanafanya nini hao.

Wakuu unaweza kushangaa watu wanakuwa victimized na wenye makosa wanaachiwa simply because wana dau kubwa.

Hapo kwenye nyekundu mkuu tupe mfano ili tukulewe vizuri.
 
Hizi kamati za bunge ni deal. Mwenye dau kubwa anatetewa asiye na dau anateketezwa! Kamati zinaanza kupteza uhalali kwa kujiingiza katika utendaji wa serikali ndio maana hata maoni yao hayazingatiwi. Wanajulikana wanafanya nini hao.

Wakuu unaweza kushangaa watu wanakuwa victimized na wenye makosa wanaachiwa simply because wana dau kubwa.
Hii hoja inahitaji ushahidi stahili. Maana hizo kamati za bunge zinapotoa hoja pale huwa zinaleta na evidence. si uliona kwa mfano Nundu, alikataa weee, baadaye akakubali kwamba mwenye makosa ni naibu wake. Sasa alichokuwa anakataa ni nini? Yaani ukiangalia kila anayening'inizwa utakuta kuna evidence. Sasa kwa mfano report ya CAG utasema imemuonea nani na imembeba nani ilihali data zipo clear?
 
Bunge kama kawaida yake limeendelea na usanii na kipindi kihi tumeona jinsi urais unavyowafanya wabunge wachachawe na kupigana vikumbo na mawziri wasiowapenda wanaodhani wana nuru ya kugombea urais au wapambe wao.Mbaya zaidi na Mkuu wa nchi naye anachekelea katika hili ili akijitahidi kuwaacha mawaziri waendelee kuumbuka akijifanya anawapigania kwa vile kati ya wote wanaotakiwa kujiuzulu hayuko ambaye yupo katika kambi yake au chaguo lake. Kwake Rais waziri akijiuzulu mapema kabla ya uchaguzi ni hatari kwani anaweza kuiadhiri serikali yake, anawaacha wajikanyage huku umaarufu wao ukiporomoka wakati yeye mwenyewe anayajua madudu yote aliyowaagiza kufanya ndio maana nasema hakuna waziri mwenye kosa la kujiuzulu endapo rais ataendelea kuwa madarakani
 
Sio siri inauma yaani inauma sana. Hata bunge lifutwe tu waendelee kula kodi zetu wapendavyo maana hakuna impact ya bunge watu wanasimamia hoja za msingi hawasikilizwi nchi ipo mikononi mwa watu wachache
I concur you mkuu. Bunge liwe ni kwaajili ya kupitisha sheria na bajeti tuu. Maana haya mengine wanajadili hayana kazi. Wamapigia kelele suala la Jairo wee, likaishia tu somewhere. Bunge likachonga wee kuhusu HOsea, Mwanyika na yule katibu wa nishati na madini wa wakati ule, serikali ikakaa kimya hadi akina Mwanyika na mwenzake wakastaafu na kula mafao yao yote, na zaidi sana Hosea hadi leo bado yupo. JIkumbushe tena ya juzijuzi hii kuhusu Luhanjo, aaah, yaani kikwete ni kama ameweka pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao. Inaudhi, siyo siri. Hapa akijitokeza mtu anambie niandamane usiku kucha sitasita kufanya hivyo.
 
Hakika hii serikali ni ya kuzimu kabisa kwani inafanya dhambi mbaya sana na lichama lake, kila siku inawafunga wezi wa kuku tena kwa shuruti nzito lakini wenyewe wameiba matririoni ndo kwanza wanazidi kujenga majumba na kununua magari yenye viyoyozi na wakati huo huo vijana wenzangu wanofeli 404 kila mwaka wanatapatapa tu mitaani bila ya mwelekeo, jamani watanzania wenzangu ifike muda sasa tuseme imetosha kwani mpaka lini tutaendelea kunyanya swa na hawa majambazi wa kijani?

Vipi kuhusu hatima yetu kwa sisi ambao bado angali damu changa na tupo shuleni? Hizo fedha za kamati wameshindiwa nini kujenga hata visma nyumbani tabora watu watumie maji safi?

SIO SIRI KAKA NA DADA ZANGU WANA JF MIMI INANIUMA SANA NA NAAMINI MUNGU YULE WA ISRAEL NA MUNGU WA LEMA HATAWAACHA HAWA MAGAMBA SALAMA HADI 2015, AMEN.
Mkuu, tufanyeje sasa.

Umeandika kwa uchungu mkubwa sana. Mtu akisoma tu mistari yako anaweza kufeel namna gani ulikuwa wakati unaandika. Lakini sasa tufanye nini kujikomboa na hali hii? Tumshawishi Mbowe na Slaa waandae maandamano ya nchi nzima, au tujikusanye tuingie mstuni?
 
Ni kweli kabisa, tatizo ni IKULU na Wabunge wa CCM.

Ikulu haiwachukulii/wajibishi mawaziri wanaofanya ufisadi. Matokeo yake tunajenga culture ya mawaziri na watendaji wakuu kufanya ufisadi.

Wabunge wa CCM hawataki kupitisha sheria kali ambazo zitawafanya hao mawaziri na watendaji wengine serikalini waweze kuwajibika. Sheria zikipelekwa wanazipitisha kama zilivyo pamoja na kwamba zina matobo kibao.

Dawa ni kupunguza idadi yao, ili wasiwe wanalitumia vibaya Bunge kwa manufaa ya Chama chao na kulinda watendaji wabovu wa serikali yao.
wazo zuri, lakini tunawapunguzeje hawa wabunge wa CCM? Just recall chaguzi mbalimbali tulizofanya. Humu JF tunaongea sana, tunatamani mabadiliko lakini wapiga kura hawafanyi hivyo, je unalichukuliaje hilo? Tuanzie wapi?
 
Mimi ninafikiri kwamba hakuna haja ya kuwa na Bunge.

Nipeni japo mfano mmoja tu wa maazimio ya Bunge ambayo yalishawahi kutekelezwa na serikali.

Bunge tulilonalo sasa hivi, ni baya sana kuliko hata Bunge la Mfumo wa Chama Kimoja. Hatuwezi kutoka kwenye hili tope mpaka dominance ya chama kimoja itakapokuja kuisha.

Let us pray that hii 75% ya CCM ipungue hapo 2015.
siyo waondoke kabisa madarakani?
 
mkuu kwa mtazamo wa nje utasema ya kishikaji ila kiukweli hii ndio shida ya kuongozwa na wafuasi wa freemason, walala makaburini na wapiga ramli....wao mateso ya wananchi ndio mtaji kwao...Mungu wa Mbinguni aliyezifanya Mbingu na Dunia na awe upande wa nchi na taifa la Tanzania ili wenye haki wake wasionewe na hawa wachawi.
Mkuu tupe evidence au japo mfano wa member wa freemanson katika serikali ya Kikwete.
 
Bunge kama kawaida yake limeendelea na usanii na kipindi kihi tumeona jinsi urais unavyowafanya wabunge wachachawe na kupigana vikumbo na mawziri wasiowapenda wanaodhani wana nuru ya kugombea urais au wapambe wao.Mbaya zaidi na Mkuu wa nchi naye anachekelea katika hili ili akijitahidi kuwaacha mawaziri waendelee kuumbuka akijifanya anawapigania kwa vile kati ya wote wanaotakiwa kujiuzulu hayuko ambaye yupo katika kambi yake au chaguo lake. Kwake Rais waziri akijiuzulu mapema kabla ya uchaguzi ni hatari kwani anaweza kuiadhiri serikali yake, anawaacha wajikanyage huku umaarufu wao ukiporomoka wakati yeye mwenyewe anayajua madudu yote aliyowaagiza kufanya ndio maana nasema hakuna waziri mwenye kosa la kujiuzulu endapo rais ataendelea kuwa madarakani

now we are reading on the same page
 
jamaa kamwambia watanzania kuwasahaulisha ongea vitu wanavyopenda ndo kaamua kusema simba kupotosha ukweli
Hii sikuinyaka, nani aliyeongelea habari za simba? Pinda ndiyo alisema habari za simba bungeni?
 
Hana tuu uwezo wa utawala pia ni mwizi mawaziri wengi,wakuu wa mikoa na wilaya wengi wanalinda utajiri wake atamtoa nani wakati anakula nao sahani moja angoje kimbunga chake kinakuja hasira ya wananchi ni zaidi ya anavyofikiri kuwa ni upepo eti yatapita
 
Naonga mkono hoja...kamati za nini kama hakuna mapendekezo hayana maana? Ya nin kuchezea hela zetu wakati hata wanayoyasema yanakuwa kama tafti hewa za vyuo vyetu vikuu? YA NINI SASAAAA??????
 
Waziri mkuu amehitimisha hoja ya serikali kutekeleza mapendekezo ya bunge kama kamati zilivyo shauri,wabunge wa chama tawala wamenyamaza hakuna mwenye hoja zaidi ya kutazamana.Utamaduni wa kulindana unazidi kushika kasi huku haijulikani nani atayemfunga paka kengele.Bunge kimya,spika naye kama kawaida yake ana chakachua sauti za wabunge za kuahirisha bunge huku Watanzania wakishikwa na simanzi kutokana na hali iliyo likumba taifa letu.Maneno yaliyosemwa kwenye baadhi ya nyuzi humo JF kuwa kutojiuzuru kwqa mawaziri kuna baraka za baba mwanaasha sasa zimejidhihirisha wazi. Tanzania kwanza itikadi za vyama vyetu baadae,huu ni wakati wa wabunge kuthibitisha kauli zao kwa vitendo bila kujali wanatoka mchama kipi.Kama kweli wanaongozwa na dhamira ya kushughulikia matatizo ya wananchi ni wakati wao wafanye maamuzi magumu ya kujivua ubunge kwa sauti moja ili kuivunja serikali dhalimu ambayo imewageuka na kusababisha matabaka ya wenye nacho na wasi nacho.Usanii unaofanya na kila waziri katika serikali hii inadhihirsha hakuna msafi katika seriakali hii,na ile dhana ya chukua chako mapema (CCM) imechukua mkondo wake. Huu si wakati wakulaumiana bali kuchukua maamuzi magumu,ili kuiondoa ile dhana ya bunge letu kugeuzwa kijiwe cha kahawa kwa bunge kushindwa kuiwajibisha serikali kwa mara nyingine.Uko wapi umahiri wa wanaojiita viranja wa kupinga ufisadi.Hali hii inajipambanua kuwa hakuna aliye msafi na hakuna naye weza kumfunga paka kengele ndani ya CCM.Mashtaka yanayo subiri hukumu ya serikali yapo mikononi mwa wananchi.Katu hatuwezi kuendelea kuongoza na chama legelege kinachoshindwa kuisimamia serikali kwa kuogopa maslahi binafsi yasiyona tija kwa watanzania.Ni wakati sasa wa nguvu ya umma kuchukua hatua dhidi ya udhalimu unaotishia mustakabali wa amani ya nchi yetu.Tumechoka kuwa mbuzi wa kafara na kutazama rasilimali zetu zinanufaisha wachache na kuwakumbatia wageni. Kitendo kilchoonyeshwa leo na mwekezaji huko wilayani Monduli kwa kuuwawa kwa mifugo isiyo na hatia kwa mwekezaji kunyunyiza sumu bila kutoa tahadhari katika kijiji husika ni ukiukwaji mkubwa kwa haki za wanyama,serikali ipo,viongozi wapo ila tu kwa ile dhana ya kitu kidogo taifa limepoteza sifa yake ya kuwa kisiwa cha amani.Inasikitisha kuona hatuna utawala bora ila ni mabingwa wa kujinadi kwenye mikutano ya wazungu kuwa bunge letu linaongozwa kwa uwazi ili hali serikali ikikaidi kutekeleza mapendekezo halali ya bunge.Wapi tunakwenda ikiwa serikaliimekosa dira na mwelekeo!?
 
Wadau, kutokana na sarakasi zilizochezwa leo bungeni, nina wazo kwamba hatuna haja ya kuendelea kupoteza hela kwa kulipa kamati za bunge, kwa kuwa hazina impact yoyote kwa nchi.

Kama kamati za bunge zitakuwa zinazunguka kwenye migodi, maliasili, sijui huko bandarini, mashambani na kwingineko kote kutafuta ukweli wa mambo halafu ukiletwa serikalini hakuna kinachofanyika, ni za kazi gani sasa?

Na je next time kuna mtu atapoteza muda wake kukusanya data za uhakika ilihali anajua hazina kazi?

Mkuu siku zote jaribu kuepuka fikra nyepesi katika michakato migumu! ipo wazi kamati zetu zinakumbana na vikwazo vigumu na vingi, chamsingi ni kuchukulia hili swala kama changa moto, apo kwa 100% halijafanikiwa naimani litatoa fundisho na angalizo kwa mbeleni. kamati zetu za bunge zinafanya vyema!
 
Mkuu siku zote jaribu kuepuka fikra nyepesi katika michakato migumu! ipo wazi kamati zetu zinakumbana na vikwazo vigumu na vingi, chamsingi ni kuchukulia hili swala kama changa moto, apo kwa 100% halijafanikiwa naimani litatoa fundisho na angalizo kwa mbeleni. kamati zetu za bunge zinafanya vyema!
Hakuna popote nilipoonyesha udhaifu wa kamati za bunge. Wasiwasi wangu ni haya matumizi makubwa ya pesa kwa ajili ya hizi kamati halafu matokeo ya kazi zao hayaonekani. Inafaa nini kuendelea kukusanya maoni katika mazingira magumu hivyo kiasi cha kutishiwa maisha halafu yale mnayoyafanya hayaleti tija?
 
Ndugu zangu wana JF Hata mimi binafs nimepatwa na msongo wa mawazo kipindi fulan kabla bunge halija hairishwa, lkn nikakumbuka yale maono yangu, zile damu zilizo mwagwa na huyu PM Zikimlilia nae Benjamini W.M Nae analiliwa tena sana, hili ni taifa teule la Mungu msiofu yeye yupo nasi. Mtaona mengi wala msikome kumwomba Mungu Muumbaji wa vyote.
 
Na we uwe sehemu ya mabadiliko sio tu unataka changes na hata kura hujawai kupiga
 
acha kuongea pumba kijana watu wana uchungu na nchi yao

Ukitafakari utaona ukweli wa hiyo statement ya huyo bwana.Tatizo sio mawaziri wala serikali,tatizo ni wananchi wanaokubali maazimio na hatua zinazochukuliwa na viongozi wetu.Pamoja na PM kuacha kuwajibisha mawaziri,wewe na mimi tunaendelea na maisha yetu ya kawaida na nina hakika baada ya wiki mbili tutasahau hili na kudandia lingine tofauti.Poleni watanzania.
 
Back
Top Bottom