Spika wa Bunge, Dkt. Tulia aunda Kamati kufuatilia kama kuna uvunjifu wa Haki za Binadamu katika mgogoro wa ardhi unaohusisha Kanisa la EFATHA

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,512
6,014
Snapinsta.app_446660058_4588952277995715_6457819694320408747_n_1080.jpg

Snapinsta.app_446314119_443473288636318_7689251848114144303_n_1080.jpg


1.0 Waheshimiwa Wabunge, tarehe 14 Februari, 2024 nilipokea barua kutoka Kanisa la EFATHA, ikiwasilisha utetezi wake kuhusu mchango alioutoa Mhe. Deus Clement Sangu, (Mb) dhidi ya EFATHA, Mchango huo ulihusu mgogoro wa Ardhi kati ya Wawekezaji kwenye Shamba la Malonje na Vijiji vinavyolizunguka shamba hilo kikiwemo Kijiji cha Sikaunga katika Jimbo la Kwela. Kwa kuzingatia maombi ya Kanisa la EFATHA kukutana na Kamati ya Bunge inayohusika, nililipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ili lifanyiwe kazi.

2.0 Waheshimiwa Wabunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilikutana na Viongozi wa Kanisa la EFATHA, Mbunge na wawakilishi wa Kijiji cha Sikaunga. Tarehe 9 Mei, 2024, Kamati hiyo iliwasilisha kwangu taarifa kuhusu matokeo ya Kikao hicho. Katika Taarifa hiyo Kamati ilibainisha yafuatayo:-

(a) Mgogoro wa Shamba la Malonje ni wa muda mrefu, na kwamba umekuwa ukizungumzwa Bungeni na Wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti kabla Mhe. Deus Clement Sangu (Mb) hajaingia humu ndani;

b) Licha ya kuwepo kwa kumbukumbu za mawasiliano kati ya Waziri wa Ardhi na Wawekezaji wa Shamba hilo zinazoonesha mgogoro umekwisha, kiuhalisia mgogoro huo bado upo na umedumu kwa miaka 13 ukiwa na madhara makubwa kwa pande zinazohusika;

(c) Hatua zilizochukuliwa na Mhe. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kutatua mgogoro huo tarehe 17 na 23 Novemba, 2023 haziendani na kumbukumbu zilizopo Bungeni kuanzia Mwaka 2014 hadi 2015 zilizohusu Majibu ya Serikali kwa Maswali ya Wabunge wakiwemo Mhe. Ignas Aloyce Malocha na Mhe. Khalfan Hilary Aeshi; na

(d) Wananchi wa Vijiji vinavyozunguka Shamba la Malonje hawaridhiki na namna Wizara inavyoshughulikia mgogoro huo.

3.0 Waheshimiwa Wabunge, baada ya kupitia barua ya Kanisa la EFATHA, Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard) nimeamua kuunda Kamati Maalumu chini ya Kanuni ya 144 ya Kanuni za Kudumu za

Bunge, Toleo la Februari, 2023. Kamati hiyo itaongozwa na Hadidu za Rejea zifuatazo:-

(a) Kubaini eneo la Shamba la Malonje lilipoanzia;
(b) Kubaini mipaka halisi ya Shamba la Malonje na Vijiji vinavyolizunguka;
(c) Kubaini iwapo taratibu za uongezaji wa eneo zilifuatwa katika ongezeko la ukubwa wa Shamba la Malonje;
(d) Kubaini iwapo kuna dalili za vitendo vya uvunjifu wa Haki za Binadamu vinavyodaiwa kufanywa na walinzi wa Shamba la Malonje, na iwapo vitendo hivyo vinatokana na miongozo ya Wamiliki wa Shamba; na
(e) Kubaini jambo lingine lolote linalohusiana na mgogoro huo.

4.0 Waheshimiwa Wabunge, kwa kuzingatia Hadidu hizo za rejea hapo juu, nawateua Wabunge wafuatao kuunda Kamati hiyo. Wajumbe hao ni:-

(i) Mhe. Dkt. Hamisi Andrea Kigwangala (Mb)
(ii) Mhe. Lucy Thomas Mayenga (Mb)
(iii) Mhe. Mhandisi Stela Martin Manyanya (Mb)
(iv) Mhe. Innocent Sebba Bilakwate (Mb)
(v) Mhe. Festo Richard Sanga (Mb)
(vi) Mhe. Asia Abdukarimu Halamga (Mb) (vii) Mhe. Erick James Shigongo (Mb)
(viii) Mhe. Ester Amos Bulaya (Mb)
(ix) Mhe Joseph Anania Thadayo (Mb) (x) Mhe. Tauhida Gallos Cassian (Mb) na
(xi) Mhe. Prof. Shukran Elisha Manya (Mb)

5.0 Waheshimiwa Wabunge, Kamati hii itaongozwa na Mhe. Prof. Shukran Elisha Manya (Mb) na itafanya kazi kuanzia tarehe 1528 Julai, 2024. Aidha, Kamati Maalum itapaswa kukabidhi Taarifa kwangu kabla ya tarehe 2 Agosti, 2024 kufuatana na masharti ya Kanuni 144 (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Dkt. Tulia Ackson (Mb) SPIKA 27 Mei, 2024

Pia soma
 
Kuna jambo la kuangalia kwa makini naana uwekezaji kwenye asa vijijini asa zamani uligubikwa na mambo mengi zaidi rushwa
 
Back
Top Bottom