Kamati za bunge zifutwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za bunge zifutwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Apr 23, 2012.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wadau, kutokana na sarakasi zilizochezwa leo bungeni, nina wazo kwamba hatuna haja ya kuendelea kupoteza hela kwa kulipa kamati za bunge, kwa kuwa hazina impact yoyote kwa nchi.

  Kama kamati za bunge zitakuwa zinazunguka kwenye migodi, maliasili, sijui huko bandarini, mashambani na kwingineko kote kutafuta ukweli wa mambo halafu ukiletwa serikalini hakuna kinachofanyika, ni za kazi gani sasa?

  Na je next time kuna mtu atapoteza muda wake kukusanya data za uhakika ilihali anajua hazina kazi?
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade hata nyani kule msituni katika hali yao hawawezi kufanya ujinga kama huu wa serikali leo ukiongozwa na bwnPinda yaani Twiga,Tembo Viboko wanibwa Waziri mkuu anakaa kimya anatueleza habari ya Sensa na kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne? jamani nyani na utawala wao wanaweza fanya nujinga huu
   
 3. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kila jambo na wakati wake, tujipange tatizo cyo mawaziri
   
 4. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Exactly uko sawasawa mkuuu! hapa kinachofanyika ni kupromote bifu na na kuchezea hela za walipa kodi tu.
   
 5. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hebu tueleze tatizo liko wapi?
   
 6. mayuni

  mayuni JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 406
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  bora kusiwe na hvyo vikalimat km sio kamat
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Hizi kamati za bunge ni deal. Mwenye dau kubwa anatetewa asiye na dau anateketezwa! Kamati zinaanza kupteza uhalali kwa kujiingiza katika utendaji wa serikali ndio maana hata maoni yao hayazingatiwi. Wanajulikana wanafanya nini hao.

  Wakuu unaweza kushangaa watu wanakuwa victimized na wenye makosa wanaachiwa simply because wana dau kubwa.
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Serikali ya kishkaji ya kikwete.mwizi ana haki,mwema/ MKOSOAJI anafuatiliwa na TISS,ila 2na hasira na nampongeza Jk kusaidia kuizika ccm.
   
 9. Mauntana

  Mauntana Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sio siri inauma yaani inauma sana. Hata bunge lifutwe tu waendelee kula kodi zetu wapendavyo maana hakuna impact ya bunge watu wanasimamia hoja za msingi hawasikilizwi nchi ipo mikononi mwa watu wachache
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hakika hii serikali ni ya kuzimu kabisa kwani inafanya dhambi mbaya sana na lichama lake, kila siku inawafunga wezi wa kuku tena kwa shuruti nzito lakini wenyewe wameiba matririoni ndo kwanza wanazidi kujenga majumba na kununua magari yenye viyoyozi na wakati huo huo vijana wenzangu wanofeli 404 kila mwaka wanatapatapa tu mitaani bila ya mwelekeo, jamani watanzania wenzangu ifike muda sasa tuseme imetosha kwani mpaka lini tutaendelea kunyanya swa na hawa majambazi wa kijani?

  Vipi kuhusu hatima yetu kwa sisi ambao bado angali damu changa na tupo shuleni? Hizo fedha za kamati wameshindiwa nini kujenga hata visma nyumbani tabora watu watumie maji safi?

  SIO SIRI KAKA NA DADA ZANGU WANA JF MIMI INANIUMA SANA NA NAAMINI MUNGU YULE WA ISRAEL NA MUNGU WA LEMA HATAWAACHA HAWA MAGAMBA SALAMA HADI 2015, AMEN.
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Siyo kamati tu hata bunge la jamhuri ya Muungano halina tena maana yoyote kwetu. Kama wameshindwa kutumia mamlaka na kanuni za kuwawajibisha watesi wetu serikali ya Jk, kuna haja gani ya wao kuendelea kuzifaidi kodi zetu?

  Kuanzia leo nakilaani kiti anachokikalia spika wa bunge na kila mwana mama atakaetaka kukikalia alaaniwe.

  Laana ya Yezebeli wetu kwa taifa hili imethihirika wazi leo hii, pale aliposhiriki hila ya kunyanganya haki ya wanyonge wanaoteseka kwa thuluma ya mawaziri. Sina imani nae, sina imani na mwanaume anaeburuzwa na jike sina imani ni ngonjera za wale wanaojiita wasimamia katiba ya nchi, maana wameuridhia uovu wa mwanamke mwovu wa taifa.
   
 12. M

  Mchomamoto Senior Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkubwa nakuunga mkono yaani zaidi ya 100% maana huu ni ushe*** sioni maana ya kuwa na kamati mm NASHAURI SASA KILA MTU AFANYE LOLOTE ANALOLIJUA POTELEA MBALI ACHA WANYAMA NA MADINI YAISHE TUU KILA MTU ATAJIJUA!!aaaah tumechoka bwana!!
   
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  umesahau na kuisifia Simba SC tena kwa kurudia rudia kuonesha ameguswa....nchii hii inaongozwa na wapuuzi.
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa, tatizo ni IKULU na Wabunge wa CCM.

  Ikulu haiwachukulii/wajibishi mawaziri wanaofanya ufisadi. Matokeo yake tunajenga culture ya mawaziri na watendaji wakuu kufanya ufisadi.

  Wabunge wa CCM hawataki kupitisha sheria kali ambazo zitawafanya hao mawaziri na watendaji wengine serikalini waweze kuwajibika. Sheria zikipelekwa wanazipitisha kama zilivyo pamoja na kwamba zina matobo kibao.

  Dawa ni kupunguza idadi yao, ili wasiwe wanalitumia vibaya Bunge kwa manufaa ya Chama chao na kulinda watendaji wabovu wa serikali yao.
   
 15. S

  Sam Upendo Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ule usemi kwamba kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji umetimia leo hii bungeni. Pamoja na hoja kali za wabunge na watanzania wote kwa ujumla kuhusu ubadhirifu wa mawaziri, leo hii wakati wa kuahirisha bunge Pinda hakueleza lolote kuhusu msimamo wa serikali kuhusu hoja hizo.

  Kwa maana nyingine Serikali imezipuuza "kelele" za wabunge kwamba ni upepo wa kupita. Eti wabunge wanapiga kelelle kusudi wasikike majimboni kwao! Kweli hii ni dharau kubwa sana kwa watanzania. Kumbe mawaziri hawawajibiki kwa Bunge!!!

  Ndiyo maana hata JK akajiondokea kwenda Malawi bila wasiwasi wowote na bila hata kushauriana na Pinda kuhusu hali ilivyo bungeni kwa sababu alijua tu kwamba hayo ni "Majungu" tu ya wabunge yasiyo na maana!

  Kumbe hata Kamati za Bunge zinapoteza muda wake pamoja na fedha za watanzania tu, hivyo ni heri zivunjwe. Si mlisikia jinsi waziri wa uchukuzi alivyowaeleza waandishi wa habari kwamba alipuuza maagizo ya kamati kuhusu mambo fulani ya bandari? Je, Jairo na yule mzito wa TBS si wanaendelea kutanua tu pamoja na kelele zote za wabunge?

  Tena basi, si ajabu hata kesho au kesho kutwa tukasikia kwamba Jairo sasa ameteuliwa kuwa Balozi wetu nchi za nje. Ama kweli wanyonge tulie tu! Kweli?
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi ninafikiri kwamba hakuna haja ya kuwa na Bunge.

  Nipeni japo mfano mmoja tu wa maazimio ya Bunge ambayo yalishawahi kutekelezwa na serikali.

  Bunge tulilonalo sasa hivi, ni baya sana kuliko hata Bunge la Mfumo wa Chama Kimoja. Hatuwezi kutoka kwenye hili tope mpaka dominance ya chama kimoja itakapokuja kuisha.

  Let us pray that hii 75% ya CCM ipungue hapo 2015.
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa mtazamo wa nje utasema ya kishikaji ila kiukweli hii ndio shida ya kuongozwa na wafuasi wa freemason, walala makaburini na wapiga ramli....wao mateso ya wananchi ndio mtaji kwao...Mungu wa Mbinguni aliyezifanya Mbingu na Dunia na awe upande wa nchi na taifa la Tanzania ili wenye haki wake wasionewe na hawa wachawi.
   
 18. M

  Mchomamoto Senior Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe MNAMBOWA!!nina wasiwasi na uraia wako haki ya nani ww sio raia wa Tanzania ninauhakika!!
   
 19. K

  King kingo JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kiongozi hapo kwenye red ndio haswa tunachotakiwa kufanya na sio kuiachia Chadema kazi hiyo, sisi kama watanzania ndio tunatakiwa kupambana kuhakikisha wabunge wanaopiga makofi tu (CCM) wanapungua kama kweli tunataka kuwa na Bunge lenye nguvu kwa maendeleo ya Tanzania vinginevyo hizi sarakasi na sanaa kama za bunge hili hazitaisha na tutazidi kulalamika tu.
   
 20. E

  ELIESKIA Senior Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamaa kamwambia watanzania kuwasahaulisha ongea vitu wanavyopenda ndo kaamua kusema simba kupotosha ukweli
   
Loading...