Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,548
- Thread starter
- #41
Madela wa Madilu, KUB ni Kambi rasmi ya Upinzani ambayo yote imehodhiwa na Chadema. Kambi rasmi ya upinzani ndio itaunda baraza kivuli la mawaziri.hebu nipige shule ya uhakika kuhusu KUB,sielewi KUB ni nini na inahusianaje na hizo kamati nyingine.
Endapo nimeelewa vizuri ina maana Mpini bado wanao CDM, kazi itakuwa ni moja kutimua wenyeviti wa kamati ili uchaguzi ufanyike tena na tena hadi ifike 2015. Hata ikibidi kuwatimua kwa sababu zozote hata mara 1000.
Hizi kamati tatu zinaitwa Oversee Committe (PAC, LAC na POC) zilitakiwa kuongozwa na wabunge wa kambi rasmi ya upinzani hivyo zingeongozwa na wabunge toka Chadema.
Baada ya jana kupindisha kanuni, sasa wabunge wengine wowote wa upinzani wanaweza kuziongoza kamati hizo za oversee.
Kamati hizi haziwajibiki kwa kiongozi wa upinzani bungeni bali zinawajibikq kwa spika.