Kamati za Bunge: PAC-Cheyo, LAC-Mrema & POC-CUF! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za Bunge: PAC-Cheyo, LAC-Mrema & POC-CUF!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 8, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Kesho ndio siku ya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge baada ya leo kutangazwa majina ya wajumbe wa kamati hizo.

  Chama kilichoshika mpini Bingeni ndio determinant za nani waongoze kamati zipi. Hivyo CCM wameamua kuionyesha Chadema kuwa si lolote si chochote kwa kuhakikisha hawachaguliwi kuongoza kamati yoyote!.

  Hivyo wameamua uenyekiti wa PAC kumpigia kura John Memosa Cheyo wa UDP, LAC watampigia Agostino Lyatonga Mrema wa TLP na POC itakwenda kwa mwanamama wa CUF.

  Kama ni kweli hivyo ndivyo itakavyokuwa kesho, then Chadema wataongoza serikali kivuli kipofu maana haitakuwa na macho ya kuangalia ndani ya serikali baada ya kupoteza hizi over sight committies.

  Habari hizi ni kwa mujibu wa corridors za Bungeni Dodoma.
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivyo ndio Rostam alivyoiweka selikali mfukon!Mungu pekee atakaye isambalatisha ccm kwa kutumia mitume wake chadema.FREEDOM IS COMING TOMOROW!
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa CHADEMA wana maana gani kuendesha kambi ya upinzani kipofu.....better waachie wanaotaka rasmi waiendeshe wao maana kwa hali ilivyo ni vigumu kuniambia kutakuwa na ushirikiano kati ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na viongozi wa kamati hizi ambao watakuwa wamejaa jeuri kwa kuteuliwa kwako kutokea kwenye mgongo wa wabunge wengi wa CCM

  Better achiwe Hamad na Kafulila waongoze kambi ya upinzani maana huu ni upuuzi kuwa kiongozi wa upinzani huku kamati muhimu za kuisimamia serikali zikiwa virtually chini ya CCM. Utaisimamiaje serikali ambayo huoni inafanya nini kwa kunyang'anywa macho?
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Mbowe bado atabaki ndiye waziri mkuu kivuli na atateua baraza la mawaziri vivuli.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chadema waachane na hicho kinachoitwa kambi ya rasmi ya upinzani.badala yake wapange hoja nzito kwa maslahi ya wananchi waliowachagua.
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni fedha na marupurupu ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ni vigumu sana kwa Mbowe kuviachia!!
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Kwa ajuaye, hivi hizo kamati tatu ndio zinazoainisha upinzani bungeni au ni maeneo ya ulaji tu?
   
 8. w

  warea JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtindo huu haina haja hata ya kufanya siasa.
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Inaonekana humu ndani wamejaa wataalumu wanaomfahamu mbowe vizuri sana.

  ...Inaburudisha!
   
 10. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi sikubaliani na ushauri wa chadema kuachia kambi rasmi ya upinzani kwani hiyo pesa itawasaidia kujiimarisha kwa ajili ya 2015. Wakiachia ina maana ziende tena Pemba (CUF), haiwezekani hiyo ni kodi yetu Watanganyika.
   
 11. O

  Old ManIF Senior Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama tetesi hizi zitakuwa ndio ukweli wenyewe (uhalisia wa mambo) basi hii ndio changamoto ya uongozi itakayo wakuta hao cdm, hivyo wanatakiwa watafute ufumbuzi wa nini watakachofanya katika hilo, hiyo ndio kazi ya kuongoza si lelemama. Nitawashangaa hawa chadema kama hawaku anticipate kuwa ccm watatumia uwingi wao kuwavurugia mipango yao. Wanatakiwa wajue ni jinsi gani ya kuyapatia ufumbuzi mambo kama hayo, siwategemei kabisa kuanza kulalama tu. Lazima wajue kuwa baadhi ya misimamo yao itakuwa na gharama zake, hii ni moja ya gharama ambayo dawa haitakuwa kulalamika ila nikuitafutia dawa. Dawa ya kwanza kwa kuwasaidia ni kuwashitaka hawa kwa wananchi, yaani kuwaeleza wananchi na hasa wenye ulelewa wa haya kwa hali ya chini kabisa ni vipi maamuzi kama haya yanavyo wazuru katika ustawi wa maisha yao.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  na ndio maana watu hawakujisumbua kujitokeza kupiga kura!.
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Hizo ni kamati but still KUB na kaimu wake na baraza lote ni CDM, wenyeviti watakaochaguliwa wata-riport kwa KUB na watafanyakazi kwa maelekezo ya KUB wakifanya madudu KUB anawawajibisha CCM wanachagua wengine na mchezo unaendelea kama alivyowajibishwa Cheyo.
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Hivi sisi watanzania tunajifanya taahira kweli!
  Ni nani asiyejua kuwa bado Tanzania inaongozwa kwa misingi ya chama kimoja kama Taifa..nani halijui hili?

  Vyama vilivyopo ni vyama vya kuisindikiza CCM. Ndio maana ni muhimu vyama hivi CDM, CUF, NCCR,TLP, UDP vishirikiane viweze kuubadilisha huu mfumo kutoka Chama kimoja kwenda mfumo wa vyama vingi.(Katiba mpya)

  sasa hivi watu wanafanya maslahi tu, kuganga njaa...ni wachache sana ambao wako kwa kuwatumikia walalahoi, wananchi wa kawaida.
  kumbuka siasa TZ ni short cut ya kukimbia makali ya njaa!!kwa kisingizio cha kuwatumikia wananchi.
  Marando anataka kuwatumikia wananchi? Mbowe anataka kuwatumikia wananchi? Mrema huyu wa leo anataka kuwatumikia wananchi? Hamad rashid anataka kuwatumika wananchi? Mzee mapesa anataka kuwajaza watu mapesa?...wote hawa wanataka wapate fungu katika kodi zetu...TZ bado hatujaweka mfumo kwa viongozi tunaowachagua kuwajibika kwa wananchi...ni wachumia tumbo na kujaza mifuko yao tu.

  kama una mifano ya wasio waganga njaa.. au wabinafsi weka orodha yao hapa!!
  Pengine "beautiful ones are not yet born!!!"
   
 15. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkinga alisema,nyerere akisema anachukia rushwa mwili mzima unaoneka kwamba anachukia rushwa,mikono yake,macho yake,na hata safu ya mawaziri wake wanalioneka.linganisha na juzi kikwete alivyokua akijitetea juu ya dowans,machon pake na mikono yake utajua huyu mzee anahusika.kama angetamka mimi kama rahsi dowans haitalipwa bas kidogo ningemkubali.narudi kwa sitta na mwanyembe wakisema wanapinga dowans kweli macho yao na miko yao inadhirisha,ila mlete makamba,rostam,ngeleja,makinda na wengine wanaonekana hata kwa utendaji kazi.rudi kwa slaa,mbowe,lema,lisu,mdee,mnyika wanaonekana kwa matendo yao hata kwa matamsh yao.nafikiri mkuu sinasababu ya kuzama ili umelewa nin namaanisha
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  kama hizi hela zilienda Pemba basi zilifanya kazi yake, nimesikia majimbo yote Pemba yalichukuliwa na CUF au?
  Pia last time I checked Pemba ilikuwa ni Tanzania au imekuwa sehemu ya Kenya sasa?
  Pia ninavyojua ni kuwa TRA inafanya kazi Zanzibar pia...TRA wanakusanya nini? mawe?

  hata mimi sikubaliani kuwa CDM isusie kambi ya upinzani ila ningefurahi kama itawashirikisha wa vyama vyengine pia.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  nimezungumzia kuwatumikia wananchi,kuganga njaa na ubinafsi..wewe umekuja na habari ya rushwa...ndio tutaelewana hapa?
   
 18. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nadhani umefika muda wakuondoka Jf, maana naweza kufa kabla ya wakati....

  Max na Invisible, pls naombeni mnipe Ban ya week 1..
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Umesema ya week 1 au mwaka 1 rudia tena hawajasikia.
   
 20. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni ya SIKU 7 tu.
   
Loading...