Kamati yashauri Mikataba DP World itakayosainiwa Itaje Muda wa Utekelezaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeshauri mikataba ya utekelezaji itakayosainiwa itaje muda maalumu wa utekelezaji wa miradi ambao utazingatia maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.

Ushauri huo umetolewa leo Jumamosi Juni 10, 2023 bungeni Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso wakati akitoa maoni ya kamati kuhusu azimio la Bunge kuridhia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.

“Kamati inasisitiza kwamba uhai wa mikataba ya utekelezaji itakayosainiwa itaje muda maalumu wa utekelezaji wa miradi ambao utazingatia maslahi mapana ya nchi." - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

"Vilevile, mikataba hiyo iwe na kipengele kinachoelekeza wabia kufanya tathimini ya utekelezaji wa miradi ya uwekezaji, na kuvunja makubaliano iwapo utekelezaji huo hautafanyika kama ilivyokusudiwa" - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

"Kamati imeona ni muhimu Serikali ikayazingatia kwa lengo la kuweka mazingira mazuri kwenye uandaaji wa mikataba ya utekelezaji ili kuwa na tija na kukidhi matakwa ya wananchi" - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

"Kamati inashauri mikataba ya ubia kati ya mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), DP World na kampuni nyingine izingatie maslahi ya nchi. Pia, amesema Serikali iendelee kusimamia usalama kwa kuzingatia kwamba bandari ni sehemu nyeti." - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

Kamati imesisitiza kwamba Serikali iendelee kukaribisha wawekezaji wengine katika maeneo ambayo hayajapata wawekezaji.

"Kwa kuwa makubaliano yanayopendekezwa kuridhiwa na yana sura ya ubia, hivyo basi, Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kwamba ajira za Watanzania zinalindwa na kuweka mfumo thabiti wa mgawanyo wa ajira baina ya nchi wabia." - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

"Kuwepo na utaratibu wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa bandari kwa lengo la kuhaulisha ujuzi, maarifa na teknolojia; na kushirikisha kampuni ya Kitanzania katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji" - Mhe. Selemani Kakoso, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

kamatipiic.jpg
SetHq6hD.jpg
 
Kwa kawaida mikataba kama hii haiwezi kuwa ya muda mfupi hapa tunaongelea 30+ years kwa port zetu, hao waarabu ni wafanyabiashara siyo watoa msaada na sijasikia kuwa mkataba ukiisha tunabaki na uwekezaji waliofanya ama wanafungua kila kitu na kuondoka navyo, vyovyote ilivyo hapa kuna miaka zaidi ya 50
 
Back
Top Bottom