Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Yatembembelea Chanzo cha Umeme wa Treni ya Kisasa Kinyerezi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
✔️Yasema watanzania wanataka kuona Treni ya Kisasa inafanya kazi

✔️Vituo vya gesi kuboreshwa ili kuongeza uzalishaji

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imesema Watanzania wanataka kuona Treni ya Kisasa (SGR) inaanza kufanya kazi kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea Kituo cha kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Kinyerenzi ambacho ni chanzo cha umeme utakaotumika katika uendeshaji wa Treni ya Kisasa, tarehe 13 Desemba 2023.

Sillo amesema wametembelea kituo hicho na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali hivyo kilichobaki sasa ni kwa watanzania ni kuona Treni ya Kisasa inafanya kazi ili kuthibitisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali kweli zimetumika kwa kile kilichokusudiwa.

“Tumekuja kuangalia chanzo cha umeme unaoendesha Treni ya Kisasa tumeona kazi imefanyika kubwa sana tunaipongeza Serikali kwa kazi hii, pia tumeelezwa kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi imekamilika kwa asilimia 100 na imetumia shilingi Bilioni 76.23, na ya Pili imetumia shilingi Bilioni 97.75 na imekamilika kwa asilimia 99. Kama kamati inayoidhinisha matumizi ya fedha za serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kijamii tunaipongeza Serikali kwa kazi hii kubwa na nzuri “, alisema Sillo.

Sillo amelisisitiza Shirika la Reli nchini (TRC) kukamilisha maeneo machache yaliosalia licha ya kuanza majaribio kwa kipande kilichokamilika kutoka Dar es salaam Kwenda Morogoro.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema Kamati imeishauri Wizara kuongeza uzalishaji wa Gesi kwa matumizi ambayo yataongeza na kuchagiza uchumi wa wananchi.

Pia imeshauri kuwekeza kwenye gesi ambayo inatumika katika magari, ambapo kwa sasa kuna vituo vitatu tatu vya kujaza gesi kwenye magari na mpango wa Serikali ni kujenga vituo vingine vitatu huku ikishirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeza ujenzi wa vituo vingi zaidi ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi na kuweza kubadilisha mifumo ya magari yao.

“Wizara na Sekta Binafsi tunaendelea kuboresha matumizi ya Gesi kwenye magari kwa kuweka vituo vingi zaidi kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa wepesi zaidi ili kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza Matumizi ya Nishati safi na rahisi zaidi”, alisistiza Mhe. Kapinga.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Serikali inaongeza uzalishaji wa gesi katika visima vya kuzalisha gesi kwa kufanya maboresho katika visima vya Songosongo kuanzia sasa hadi mwezi wa Aprili 2024 kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa gesi kufukia futi za ujazo Milioni 30.

Pia kuchimba visima viwili na kufanya ukarabati katika visima vya Mnazi Bay ifikapo Desemba 2024 ili kufikia uzalishaji wa Gesi futi za ujazo Milioni 25 pamoja na kuviunganisha vituo vya Ntoria na Madimba itaongeza futi za ujazo Milioni 40 hadi 60.

Uboreshaji wa vituo hivyo kutaongeza uzalishaji na kusafirishwa gesi kutoka Madimba hadi Dar es salaam, ambapo viwandavinavyotumia gesi vitapata gesi nyingi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli( TPDC) na viwanda vyote vya Petro Kemikali pia vinapata gesi.

Amesema marekebisho hayo hayataathiri upatikanaji wa umeme nchini zaidi yataongeza upatikanaji wa gesi.

GBPdqH5WAAIsfKP.jpg
GBPdqH5WAAgH3bF.jpg
GBPdqH2WAAMPa7C.jpg
GBPdo4pWAAYLNLS.jpg
 
Back
Top Bottom