Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuketi kikao maalum Jumamosi (20/03/2021). Yatangaza siku 21 za maombolezo

Kamati kuu ya CCM itakutana kwa dharura tarehe 20/03/2021 siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mwenyekiti ndugu Magufuli.

CCM imetangaza siku 21 za maombolezo sawia na tangazo la serikali.

Source Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
Itakuwa tofauti na ile ya Rais samia siku 14 aliyoitangaza
 
Kamati kuu ya CCM itakutana kwa dharura tarehe 20/03/2021 siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mwenyekiti ndugu Magufuli.

CCM imetangaza siku 21 za maombolezo sawia na tangazo la serikali.

Source Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
Na kifo hakina vyama....!!!

Leo akifa wa CCM, kesho atakufa wa ACT wazalendo au chama chochote kile.

Hiyo ndiyo Demokrasia ya Mungu ambayo CCM hawataki kuisikia. Hakika Mungu hana upendeleo!!
 
Kamati kuu ya CCM itakutana kwa dharura tarehe 20/03/2021 siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mwenyekiti ndugu Magufuli.

CCM imetangaza siku 21 za maombolezo sawia na tangazo la serikali.

Source Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
Kamati kuu ya Ccm white house na kamati kuu ya Ccm ya Ndugai mjengoni nao watakaa kujadidi dhuluma zao.. Mungu hutulipia visasi.
 
Salamu Watanzania,

Naomba tusome andiko hili kutoka katika Biblia. Daniel 5: 19-21 na mstari wa 25 hadi 28.

Na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.

Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.

Akafukuzwa mbali na wanadamu moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda - mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu aliye juu ndiye anayewatawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.

Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii;

MENE - Mungu ameuhesabu Ufalme wako na kuokomesha.

TEKELI - Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

PERESI - Ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.
 
Mmekutana ili mcheze ngoma ya CDM maana ndio waliowabana kutangaza kifo na Leo mmebanwa kuomboleza siku 21 wakati serikali chini mvunja katiba Samia imemnyima marehemu siku Saba zaidi kwa kutangaza siku 14 tu. Eti polepole anadhani akisema sambamba na tangazo la serikali ndio ataivalisha nguo. Hovyo kabisa
Samia aliteleza maana lilikuwa ni tangazo gumu sana kwake ni siku 21.. Si kila jambo kuponda.
 
Leo chama cha mapinduzi kimetoa taarifa rasmi ya kifo cha Dkt. John Magufuli ambae amekuwa mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Taarifa hiyo imesomwa na Humphrey Polepole.

========

Polepole: Chama cha mapinduzi, safu yake ya uongozi na wanachama tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakuu wa chama waliopo, mzee Philip Mangula, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na mzee Ali Mohammed Shein, makamu wa mwenyekiti wa Tanzania Zanzibar wameshaurianana kukubaliana kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum siku ya Jumamosi ya tarehe 20 ya mwezi huu Machi mwaka 2021 saa nane mchana katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Aidha taarifa inatolewa kwamba chama kitakuwa katika maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo la serikali, wakati wote huo bendera za chama cha mapinduzi zitapepea nusu mlingoti.

Kutakuwa na kitabu cha salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi ya makao makuu ya CCM, 'White House' hapa jijini Dodoma lakini kitakuwepo pia kitabu cha kupokea salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi zetu za chama

Uongozi wa chama unawaomba sana wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, watanzania wote kwa ujumla kuwa na moyo mkuu, kuendelea kuwa watulivu, kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee na wa kihistoria kwa Taifa letu wa ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa inatolewa pia kwamba shughuli za chama zile zihusianazo na uchaguzi ndani ya chama zinasimama kwa muda mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani ndugu John Pombe Joseph Magufuli, Amen.

Asanteni kwa kunisikiliza
Mungu wao amekufa
 
Aliteleza? Alifuata Ganda la ndizi? Muwe mnateleza huko Lumumba mkitoka nje muwe mnakuja na akili kubwa msidhani sisi Ni wapuuzi wenzenu hapa
Psychiatric disorder will kill you.... kumuattach Samia bila reason inathibitisha hilo....
 
Daah very sad kwa kweli Magufuri amefariki akitupigania tulikua tushadungwa hiyo Zeca sijui kama huko Rwanda na kwingineko ambayo imeanza kupigwa marufuku....
Chanjo wamepewa watu million 17 na walioathirika hawafiki 400!! Below 0.00% kma tu ambavyo hta tukiwapa Insulin watu laki 1 huwezi kosa watu hta buku watakaopata side effects.

Au mwenzetu tuambie ni dawa gani haina side effects kwa walau 1% ya watumiaji wote.
 
Lazima utachanganyikiwa mzee. Mungu amsaidie mama yetu aendeleze gurudumu kwa haki.


Chadema muwe wapole, uraisi mtausikia tu
Poleni sana ila ndio ameshalala mavumbini hapo alipo anatolea mahesabu ya madudu yote aliyofanya. Trust me anajuta mnoo ila hivo hana fursa tena ya kuomba radhi maana huko kuzimu hakuna cha nlikua Rais wala jemedari.

Fundisho ni kwamba duniani tunapita tu usijikweze ukadhani una hati miliki ya maisha yako....... watu walifika stage wakadai atawale milele.

All in al msiba uliniuma sana na nilitoa chozi usiku but haibadili ukweli he was a monster.
 
Back
Top Bottom