Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuketi kikao maalum Jumamosi (20/03/2021). Yatangaza siku 21 za maombolezo

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
550
1,000
Leo chama cha mapinduzi kimetoa taarifa rasmi ya kifo cha Dkt. John Magufuli ambae amekuwa mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Taarifa hiyo imesomwa na Humphrey Polepole.

========

Polepole: Chama cha mapinduzi, safu yake ya uongozi na wanachama tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakuu wa chama waliopo, mzee Philip Mangula, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na mzee Ali Mohammed Shein, makamu wa mwenyekiti wa Tanzania Zanzibar wameshaurianana kukubaliana kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum siku ya Jumamosi ya tarehe 20 ya mwezi huu Machi mwaka 2021 saa nane mchana katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Aidha taarifa inatolewa kwamba chama kitakuwa katika maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo la serikali, wakati wote huo bendera za chama cha mapinduzi zitapepea nusu mlingoti.

Kutakuwa na kitabu cha salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi ya makao makuu ya CCM, 'White House' hapa jijini Dodoma lakini kitakuwepo pia kitabu cha kupokea salam za rambirambi na maombolezo katika ofisi zetu za chama

Uongozi wa chama unawaomba sana wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, watanzania wote kwa ujumla kuwa na moyo mkuu, kuendelea kuwa watulivu, kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee na wa kihistoria kwa Taifa letu wa ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa inatolewa pia kwamba shughuli za chama zile zihusianazo na uchaguzi ndani ya chama zinasimama kwa muda mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani ndugu John Pombe Joseph Magufuli, Amen.

Asanteni kwa kunisikiliza
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
680
1,000
Kamati kuu ya CCM itakutana kwa dharura tarehe 20/03/2021 siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mwenyekiti ndugu Magufuli.

CCM imetangaza siku 21 za maombolezo sawia na tangazo la serikali.

Source Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
Serikali tangazo la msiba kwa siku 14 sio 21 kama ulivyoandika hapa kwamba /sawia na tangazo la serikali'
 

Blackjew

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
653
1,000
Mmekutana ili mcheze ngoma ya CDM maana ndio waliowabana kutangaza kifo na Leo mmebanwa kuomboleza siku 21 wakati serikali chini mvunja katiba Samia imemnyima marehemu siku Saba zaidi kwa kutangaza siku 14 tu. Eti polepole anadhani akisema sambamba na tangazo la serikali ndio ataivalisha nguo. Hovyo kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom