Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Mkuu,
hawa watu wanaharibu kwa kukosa maarifa.
haiwezekani unajua kabisa swali flani formula yake ni xxxx alafu unaingia
kwenye mtihani bila kuifanyia kazi hiyo formula,.....
ukifeli una lalamika kuonewa na mwalimu.
Huo mfano wako wa fomula ni irrelevant una maana usipojua fomula ndio usifanye mtihani unaweza ku struggle usiku na mchana still fomula usielewe lakini at the end of the day lazima uingie kwenye mtihani.

Kwenye siasa ni ndoto kusubiri kila kitu kiwe sawa au kitayarishwe na chama tawala then uitwe njoo sasa tumeshabadilisha, you have to fight and struggle for it, sometimes force things to happen don't wait things to happen.
 
vyama vingi vimeweza kuweka vitengo mbali mbali lakini tatizo ni kuwa hakuna chama chochote katika Tanzania walioweka kamati ya uchaguzi ambayo ni endelevu wakati wote, vingi vinaunda kitendo hiki kwenye chaguzi tu, na hili ni kosa kubwa litaloendelea kuvigharimu vyama vya siasa.

chama chochote kinachohitaji ushindi ni lazima kiwe na kitengo kinachoshughulika na uchakuzi siku zote na kiwe macho wakati wote na kifanye tathmini wakati wote na tafiti maeneo yote ili chama kijue kwanini kimeshinda jimbo fulani na kwanini kimepoteza jimbo fulani

ukifanya uchunguzi kwanini umepoteza jimbo ukaacha kwanini umeshinda jimbo fulani basi umepoteza 50% ya mipango ya baadae
Umeongea vema mkuu..........
 
Chadema ni zimamoto sana, wanasubiri mpaka uchaguzi utangazwe ndiyo wanaanza harakati. Kinachotokea ni kushindwa vibaya na kuilaumu CCM wameiba kura, kumbe wenzao wamejipanga.

Chacha Wangwe alikuwa na mikakati mzuri wa kujenga chama kuanzia shinani. Inashangaza, chama kikubwa cha upinzani kinakosa ofisi maeneo makubwa kama Gairo, Newala, Kibaigwa, Kinesi, Silari, Kimamba, Mafinga, Ubaruku, Kondoa, Kwamafunchi, Tandahimba n.k halafu eti kina ndoto ya kuchukua nchi.

Wapiga kura wanatoka chini na ni lazima mtumie hela za ruzuku kuimarisha chama chenu angalau mtalingana na CCM
 
Mkuu,
hawa watu wanaharibu kwa kukosa maarifa.
haiwezekani unajua kabisa swali flani formula yake ni xxxx alafu unaingia
kwenye mtihani bila kuifanyia kazi hiyo formula,.....
ukifeli una lalamika kuonewa na mwalimu.

Huo mfano wako wa fomula ni irrelevant una maana usipojua fomula ndio usifanye mtihani unaweza ku struggle usiku na mchana still fomula usielewe lakini at the end of the day lazima uingie kwenye mtihani.
Kwenye siasa ni ndoto kusubiri kila kitu kiwe sawa au kitayarishwe na chama tawala then uitwe njoo sasa tumeshabadilisha, you have to fight and struggle for it, sometimes force things to happen don't wait things to happen.

Nilidhani wewe usie tumia masaburi kufikiria una akili sana kujua nilicho andika ni nini?
sikusema asiingie uwanjani,ila anapo ingia hajui formula afu akategemea kushinda huo
ni ujuha,...

Sikusema wasigombee,nacho ongelea mimi ni uhakika kwamba
chadema haishindi igunga,....kwasababu HAWANA SABABU YA KUSHINDA IGUNGA,...
 
Chadema ni zimamoto sana, wanasubiri mpaka uchaguzi utangazwe ndiyo wanaanza harakati. Kinachotokea ni kushindwa vibaya na kuilaumu CCM wameiba kura, kumbe wenzao wamejipanga. Chacha Wangwe alikuwa na mikakati mzuri wa kujenga chama kuanzia shinani. Inashangaza, chama kikubwa cha upinzani kinakosa ofisi maeneo makubwa kama Gairo, Newala, Kibaigwa, Kinesi, Silari, Kimamba, Mafinga, Ubaruku, Kondoa, Kwamafunchi, Tandahimba n.k halafu eti kina ndoto ya kuchukua nchi. Wapiga kura wanatoka chini na ni lazima mtumie hela za ruzuku kuimarisha chama chenu angalau mtalingana na CCM

Kwa mara ya kwanza umeongea point,ingawa umerusha jiwe kwa
wapinzani wako ila ndo ukweli.

Chadema walidhani kushinda 2005 kule tarime ilikua ndoto tu ya siku moja,..
wala mgogoro ulio kuwa ndani ya ccm haukuchangia,rasi aliijenga chadema long
time kabla ya kushinda kule na alipokufa sasa,.....

Waitara hakuna anafanya,ni pombe pombe na kujikojolea kila sehem,...ndivo anavo ijenga chadema
tarime,...afu wanategemea kuja kushinda huku?

Umenifurahisha kweli na msemo wa zima moto,but sometimes kuna watu unawasaidia,...
ngoja chadema iendelee kuzima moto labda one day watatoka......

Kushinda inataka maandalizi ya mda mrefu sana..
 
Chadema ni zimamoto sana, wanasubiri mpaka uchaguzi utangazwe ndiyo wanaanza harakati. Kinachotokea ni kushindwa vibaya na kuilaumu CCM wameiba kura, kumbe wenzao wamejipanga. Chacha Wangwe alikuwa na mikakati mzuri wa kujenga chama kuanzia shinani. Inashangaza, chama kikubwa cha upinzani kinakosa ofisi maeneo makubwa kama Gairo, Newala, Kibaigwa, Kinesi, Silari, Kimamba, Mafinga, Ubaruku, Kondoa, Kwamafunchi, Tandahimba n.k halafu eti kina ndoto ya kuchukua nchi. Wapiga kura wanatoka chini na ni lazima mtumie hela za ruzuku kuimarisha chama chenu angalau mtalingana na CCM
Kolimba alikuwa na mikakati mizuri ya kukijenga chama masikini akambulia kuondolewa sauti sasa mmeanza kuvuana bukta wenyewe tuone mtaishia wapi bado siku 10 ila kwa Lowassa havuliwi mtu pale.
 
Waitara hakuna anafanya,ni pombe pombe na kujikojolea kila sehem,...ndivo anavo ijenga chadema
tarime,...afu wanategemea kuja kushinda huku?
Am afraid my friend you are going too low .........
 
Mpaka hapo tu maana yake kwa Watanzania Wana-Igunga ni kwamba CHADEMA tumewasikia kilio chenu cha kutoweza kujichagulia mwakilishi chaguo-la-wananchi bungeni kwa zaidi ya miaka 20 hivi sasa na hivyo KAMATI KUU tumewafikia hapa hapa nyumbani kwenu hivi sasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wananchi kaeni Mkao wa KUKOMBOLEWA hivi sasa hapo Igunga; msione kitendo hiki cha nadra sana kimefanywa na uongozi wa juu wa CHADEMA. Si bure; tunayo maana yetu na maana yenyewe ni kwa taifa hili la Tanzania kamwe haliwezi kupiga hatua bila kwanza kuzika kabisa vitendo vya UFISADI na mawakala wake.

Na ili zoezi zima lifanikiwe ni sharti CHADEMA tukaanze kwa kungoa kwanza KIZIKI CHA UFISADI NCHINI hapa Igunga ndipo mbio hizi sasa zipate kuenea nchi nzimiiiiiima!! Hakika wenye kuelewa na tayari wameng'amua kwa CHADEMA hakina ajizi hata kidogo kwa vita hivi dhidi ya UFISADI nchini ndipo sasa kukaamuliwa KOSOGEZA KWA KARIBU ZAIDI MOTO MKALI WENYE PILIPILI NDANI ili Mafisadi Papa waliowahi kuchua mateka Igunga wakapate muziki wao kwa jirani zaidi.

Big up CHADEMA!!! Big Up sana Mhe Regia!!! Mpaka kieleweke Igunga lakini kwa misingi ya ushirikiano zaidi toka kwa kambi zima ya upinzani nchini kuwa kitu kimoja.

Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.
 
Hongereni kwa jitihada zote. Tunawaomba mjipange vizuri ili kupata mgombea anayekubalika ukizingatia kwamba wagombea wa CDM ni zaidi ya kumi.

Kwa kifupi tunataka mabadiliko kutoka kwenye mfumo wa kibwanyenye kuelekea uhuru na utawala wa watanzania wa kawaida wanaolazimika kukubali kuitwa walalahoi. Viva comrades viva!
SDC11466.JPG
 
I love this about JF,kila anae leta argument kuhusu chadema
huyo ni mwana CCM,CUF etc,.....mimi ni mwanachama na shabiki wa TANZANIA
sina chama chochote!!!
Speaker vita kubwa ni ya 'generation' na kwa bahati mbaya ccm hawajaelewa wanafikiri wanapambana na cdm ila ukweli ni kizazi kipya kinataka kuchukua majukumu ya kiutawala.

Hata ukiangalia ndani ya ccm kina Makamba na Nape wako kwenye vita vya ndani, dunia imebadilika kimfumo, kiutawala, kifikra na kiteknolojia lakini viongozi wengi wamekataa kubadilika na dunia inasonga mbele. Hebu jiulize kila aliyejiunga JF ni cdm? Ukweli wote sio cdm na JF haisajili wanachama wake kwa kuangalia vyama vyao ila cdm wanakidhi angalau kwa sehemu kubwa hitaji la kizazi kipya, wanagusa nyoyo za kizazi kipya ndio maana mambo yanakwenda hivi, vita ya 'generation' inaitesa sana ccm na ndiyo itakayoiondoa madarakani
 
Chadema ni zimamoto sana, wanasubiri mpaka uchaguzi utangazwe ndiyo wanaanza harakati.

hiyo RED kama ingekuwa kweli ninaimani ungekuwa na furaha maana una mapenzi na CHADEMA sasa iweje unataka chadema hisiwe zimamoto ili kushinda chama chako
 
hiyo RED kama ingekuwa kweli ninaimani ungekuwa na furaha maana una mapenzi na CHADEMA sasa iweje unataka chadema hisiwe zimamoto ili kushinda chama chako
I am a critic with positive vision.
 
Wakuu, tujulisheni maamuzi ya cc ya chadema, juu ya maamuzi ya mgombea na budget, please Regia and otherz we need to knw as wakati mnaenda! Thanx... Who knwz?
 
Wakuu, tujulisheni maamuzi ya cc ya chadema, juu ya maamuzi ya mgombea na budget, please Regia and otherz we need to knw as wakati mnaenda! Thanx... Who knwz?
Mgombea wa chadema ni mwl. Joseph Kashindye.
 
Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha. Kila la heri Kamanda.
Ni jambo zuri je anakubalka au mmetoa muwakilishi da REGIA hili linahitaji maelezo na ushuhuda wa picha kutoka kwa makamanda wenzetu vijana waliotangulia.
 
Tunaomba 'maelezo binafsi' (CV) ya wagombea: historia zao, uzoefu, na uwezo wao kuwakilisha na kusimamia matatizo ya wanajimbo. Msichakachue - taarifa sahihi tafadhali!
 
WEWE Regia mTema umechanganyikiwa, Igunga utaisikia hewani na usizani kelelel za chura zinamzuia mbuzi kunywa maji.Igunga itabaki kuwa jimbo la ccm na kama kutoka kwa rostam kumewafanya mzani jimbo liko wazi mmechelewa jimbo linawenyewe.

M/kiti wako naye alisema hivyo hivyo "kelele za mlango hazimnyimi usingizi mwenyenyumba", mbona alianza kupiga kelele tena "Oooh, CDM wanataka kupindua nchi". Utaiona NGUVU ya UMMA Igunga ndo utalijua jiji!
 
Back
Top Bottom