Kamati Kuu ya CHADEMA Kukutana Kesho Kupitisha Wagombea BAVICHA

Kila la heri cdm, jamani vijana busara itawale ubabe ujeuri na roho mbaya vishindwe. Mungu bariki cdm tegemeo la watz!
 
join date....................
ushindwe na ulegeee we gamba sugu
Mchange anafaa kwa sababu ni Muislam,Greyson pia ni kutoka kanda nyingine. Saanane hafai kwa sababu chama kitaonekana kimedhamiria kukumbatia uchagga.

Hata akichaguliwa atakuwa na makundi,atalipa visasi kwa watangulizi wake na wapinzani wake hasa hawa wabunge vijana ambao hawajamuunga mkono. Anaweza kuwalipizia kisasi kwenye uchaguzi wa ubunge 2015. Nimesoma nae india namjua
.

Pia kuna mdau huku anaitwa Sizinga,mtetezi wangu nilipofungiwa na mods huku wengi mkiwa kimya.Ilikuwa ni njama ya kumlinda huyu jamaa nisimwage dataz zake,na siku hiyo kwenye uchaguzi nakujaHata kama ana CV nzuri,hatutaki tena tuonekane chama cha wachagga.

Kwenye masters yake ya international Relations hana first class, nimesikia mtu mmoja akiwa anasema huyu jamaa ana first class kwenye international Relation,huo ni uzushi.

Ukweli ni kwamba kwenye uchumi ana First class.Kwani masters moja ilikuwa haimtoshi hadi akaenda kujiharibia CV? Nitamwaga dataz zote. Uchafu wake wa Kuvuruga chaguzi za watu wa kenya tutauweka hapa. Kwanza inabidi mumwangalie sana kwenye uchaguzi huu,hasa kesho. Hizo ndizo mbinu zake
 
Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali hapa JF zinazojaribu kuonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wana wagombea katika uchaguzi wa vijana. Sitaki kuwasemea wenzangu. Isipokuwa mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. Mgogoro uliotokea wakati wa David Kafulila baada ya kuwa amemshinda ndugu John Heche na hatimaye Kafulila kuondoka katika chama ulikuwa ni mgogoro mkubwa ambao ulikiyumbisha chama. Niliapa kwa mungu wangu kutojihusisha tena na kwa namna yeyote ile na makundi ya chama ili chama kiwe salama na tujiandae vema na uchaguzi ujao.
Ninaomba nisihusishwe kabisa na uchaguzi wa BAVICHA. Wagombea wote waliokuja kuniomba msaada nimewaambia kuwa sitaki kwani sitaki makundi. Kama kuna wengine na hasa wabunge wanasaidia baadhi ya wagombea miye siwezi kuwasemea.

Kuhakikisha sijihusishi na uchaguzi huu, niliamua kutohudhuria kikao chochote cha chama kitakachojadili majina na sijahudhudhuria na hata Kamati Kuu ya suala hilo sijahudhuria. Pia niliamua kutohudhuria uchaguzi wenyewe ingawa mimi ni mpiga kura. Sitahudhuria.

Nitafanya kazi na kiongozi yeyote ambaye vijana watamchagua kwa matakwa yao na nainaomba watu wanaogozwa na mazoea tu kuwa Zitto na Mbowe wana makambi waondokane na mawazo hayo kwani mimi sina kambi wala kundi and i have submitted myself to the existing leadership.

Wenye ugonjwa wa Zittophobiasis watafute dawa tu as i wont give you the lines to attack. All my efforts are directed towards party building.

Mgombea yeyote ambaye atajisema eti ni wa Zitto nawaomba vijana wamkatae na wachague mtu wa CHADEMA na sio mtu wa kundi lolote.

Nawatakia wagombea wote ushindi mwema na ninawatakia vijana wote wa CHADEMA uchaguzi makini utakaoonyesha sura chanya ya chama chetu.

Zitto Kabwe
Naibu Katibu Mkuu Taifa
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Lakini si ni haki yako kufanya hivyo!
 
Zitto,

Umeonyesha njia.Huo ni ukomavu wa hali ya juu kisiasa.Sasa wengine watoe misimamo yao ili kuepusha Makundi yasiyo na Tija,hatutaki speed governor katika harakati hizi za kuchukua Dola 2015
 
UCHAGUZI WA BAVICHA KIZUNGUMKUTI.

-UCHAGUZI WA BAVICHA NI KIZUNGUMKUTI....nasema ni kizungumkuti kwa sababu unawagawa vijana wa chadema katika mapande manne mpaka sasa na hii inatokana na VIONGOZI WA JUU kupigana vikumbo katika nafasi ya MWENYEKITI WA TAIFA KATIKA UCHAGUZI UNAOKUJA waliorudisha fomu wengi wao wanabebwa na MAFISADI WA CHAMA.

1. BERNAD SAANANE

2.JOHN HECHE

3.EDWIN SOKO

watajwa hapo juu ni wateule wa mwenyekiti wa chama FREEMAN HAIKAEL MBOWE ndiye anapanga taratibu za kuhakikisha miongoni mwa vijana hao mmoja anakuwa mwenyekiti wa BAVICHA ili iwe rahisi kwake kupambana na MAHASIMU wake mbele ya safari, ngoma nzito hiyo kazi ipo watachakachuana mpaka wataota mbigili, sijui itakuaje maana HECHE aliwapiga vita sana akina HALIMA MDEE, LUCY OWENYA, SUZAN LIYMO, ANNA KOMU ili kuwepo na uchaguzi wa huru na wahaki viti maalum ubunge 2010 inasemekana alizunguka nchi nzima kuwa maliza na alfanikiwa maana timbwili timbwili kila mtanzania alilisikia na kuliona mwaka jana, sasa je atasalimika na ho ni wajumbe wa kamati kuu ya chadema? tusubiri.........yetu sie mijicho..............na misikio....................

1.HABIB MCHANGE.

2.GREYSON NYAKARUNGU.

3.MASOOD S. SULEIMAN.

-WATAJWA hapo juu hawa ni madogo wa KABWE ZUBIRI ZITTO yeye alipigania miongoni mwa vijana hawa mmoja awe ndie mwenyekiti wa BAVICHA sijui watasuguana namna gani, suala la ukanda linaweza wasaidia itategemea watakavyojieleza katika mkutano wa uchaguzi wao hiyo 28 may 2011 siku ya jumamosi, najua wabunge wengi wapya wachadema wanamsaidia HECHE KUCHUKUA HIYO NAFASI maana alisaidia pia kutetea japo kisirisiri ila kwa fitina kubwa iliyomtingisha FREEMAN HAIKAEL MBOWE mpaka sasa hajui hatma yake ya baadae maana KABWE ZUBERI ZITTO KESHA SEMA 2015 atagombea urais ndani ya CHADEMA.

-HALIMA MDEE/LUCY OWENYA/JONH MNYIKA/ wameunda timu yao ya kuhakikisha GREYSON NYAKARUNGU jina halipiti ndani ya kamati kuu kwani alihongwa na FISADI NIMROD MKONO asigombee musoma vijijini na zengwe linaendelea kwa kasi kubwa maana kikao kilichokaliwa cha siri siku mbili zilizopita kimepanga siku ya kikao cha kesho kuamsha moto wa ukweli juu ya kijana huyo.

-BERNAD SAANANE ni kijana lakini inaonekana hakubaliki na vijana wengi wa CDM maana anaonekana ni mgeni na MBOWE ana siri kubwa na kijana huyo watamalizana wenyewe hawa CDM, CV YAKE IMEJAA UZUSHI mwingi ambao akipatikana kijana aliyesoma India anaweza kuweka wazi baadhi ya mambo aliyoyaeleza.

-chadema hamna jipya mshatokota
 
Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali hapa JF zinazojaribu kuonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wana wagombea katika uchaguzi wa vijana. Sitaki kuwasemea wenzangu. Isipokuwa mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. Mgogoro uliotokea wakati wa David Kafulila baada ya kuwa amemshinda ndugu John Heche na hatimaye Kafulila kuondoka katika chama ulikuwa ni mgogoro mkubwa ambao ulikiyumbisha chama. Niliapa kwa mungu wangu kutojihusisha tena na kwa namna yeyote ile na makundi ya chama ili chama kiwe salama na tujiandae vema na uchaguzi ujao.
Ninaomba nisihusishwe kabisa na uchaguzi wa BAVICHA. Wagombea wote waliokuja kuniomba msaada nimewaambia kuwa sitaki kwani sitaki makundi. Kama kuna wengine na hasa wabunge wanasaidia baadhi ya wagombea miye siwezi kuwasemea.

Kuhakikisha sijihusishi na uchaguzi huu, niliamua kutohudhuria kikao chochote cha chama kitakachojadili majina na sijahudhudhuria na hata Kamati Kuu ya suala hilo sijahudhuria. Pia niliamua kutohudhuria uchaguzi wenyewe ingawa mimi ni mpiga kura. Sitahudhuria.

Nitafanya kazi na kiongozi yeyote ambaye vijana watamchagua kwa matakwa yao na nainaomba watu wanaogozwa na mazoea tu kuwa Zitto na Mbowe wana makambi waondokane na mawazo hayo kwani mimi sina kambi wala kundi and i have submitted myself to the existing leadership.

Wenye ugonjwa wa Zittophobiasis watafute dawa tu as i wont give you the lines to attack. All my efforts are directed towards party building.

Mgombea yeyote ambaye atajisema eti ni wa Zitto nawaomba vijana wamkatae na wachague mtu wa CHADEMA na sio mtu wa kundi lolote.

Nawatakia wagombea wote ushindi mwema na ninawatakia vijana wote wa CHADEMA uchaguzi makini utakaoonyesha sura chanya ya chama chetu.

Zitto Kabwe
Naibu Katibu Mkuu Taifa
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Asante sana Hon. Zitto kwa maneno yako ya busara kuwa safari hii hutajihusisha na uchaguzi wa BAVICHA kwa vile uchaguzi uliopita ulivurugika na wewe kuhusishwa na vurugu hizo, umesema tena toka mchakato uanze hujahudhulia kikao chochote na hutahudhulia uchaguzi wenyewe ni uamuzi kweli mzuri.

Lakini kwa upande mwingine huoni kwa kufanya hivyo unaonekana kususia shughuli za chama? kama kila kiongozi atafanya hivyo Mbowe, Mtei, Slaa na wengine nani basi atakuwa jasiri wa ku face the reality na kubadili mambo akiwa katika utendaji? mimi nafikiri kiongozi jasiri si yule anayesusa ni yule anayeonyesha kabadilika kwa vitendo ndani ya shughuli yenyewe, mfano kuna watu wanam lable Lema kuwa ana vurugu lakini sijaona anasusa kwenda kushughulikia masuala ya chama (Nyamongo) kwa kuogopa ataambiwa amesababisha vurugu. Nakuomba Zitto fikiria upya kitendo chako cha kutohudhulia uchaguzi sioni kama kitasaidia sana zaidi ya kuongeza minong'ono kwa wanachama na wapinzani wako, watu huwa wanasema the absence matters than the presence umejifunza nini kwa kuwepo kwako kwenye mikutano ya Nyanda za juu na kutokuwepo kwako mikutano ya Kanda ya Ziwa.
 
Tusichague dini, tuchague mtu atakayeweza kuongoza. Kama mkristo anaweza achaguliwe na kama muislamu anaweza achaguliwe. Hapa hakuna ukanda pia tuangalie mtu mwenye uwezo wa kuongoza, hata kama wote watatoka kanda ya kati sisi tunachojali ni uongozi bora. Asante.
 
Zitto,

Umeonyesha njia.Huo ni ukomavu wa hali ya juu kisiasa.Sasa wengine watoe misimamo yao ili kuepusha Makundi yasiyo na Tija,hatutaki speed governor katika harakati hizi za kuchukua Dola 2015
Ben ni ukomavu gani unaosema Zitto kaonyesha kususia mchakato ni ukomavu na wewe ukichaguliwa halafu baadae ukasusia vikao unataka tukuone ni mkomavu kisiasa, na kama viongozi wote wakitoa msimamo kama huo nani basi atasimamia uchaguzi wenu. Mimi naona Zitto kaonyesha weakness fulani au ana kinyongo kutokana na matokeo ya uchaguzi uliopita kiongozi/kamanda huwa hasusii wapiganaji wake.
 
Nami nimesikia nikashangaa!
Zitto unanifurahisha kweli kwa nini unashangaa Juliana Shoza kutajwa au ulikuwa na maana gani tuseme basi kuna watu wako ambao unataka washinde ndiyo maana unashangaa kusikia mwingine akitajwa...........umeshangaa kusikia jina la Juliana na mimi nakushangaa unavyoshangaa..............
 
Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali hapa JF zinazojaribu kuonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wana wagombea katika uchaguzi wa vijana. Sitaki kuwasemea wenzangu. Isipokuwa mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. Mgogoro uliotokea wakati wa David Kafulila baada ya kuwa amemshinda ndugu John Heche na hatimaye Kafulila kuondoka katika chama ulikuwa ni mgogoro mkubwa ambao ulikiyumbisha chama. Niliapa kwa mungu wangu kutojihusisha tena na kwa namna yeyote ile na makundi ya chama ili chama kiwe salama na tujiandae vema na uchaguzi ujao.
Ninaomba nisihusishwe kabisa na uchaguzi wa BAVICHA. Wagombea wote waliokuja kuniomba msaada nimewaambia kuwa sitaki kwani sitaki makundi. Kama kuna wengine na hasa wabunge wanasaidia baadhi ya wagombea miye siwezi kuwasemea.

Kuhakikisha sijihusishi na uchaguzi huu, niliamua kutohudhuria kikao chochote cha chama kitakachojadili majina na sijahudhudhuria na hata Kamati Kuu ya suala hilo sijahudhuria. Pia niliamua kutohudhuria uchaguzi wenyewe ingawa mimi ni mpiga kura. Sitahudhuria.

Nitafanya kazi na kiongozi yeyote ambaye vijana watamchagua kwa matakwa yao na nainaomba watu wanaogozwa na mazoea tu kuwa Zitto na Mbowe wana makambi waondokane na mawazo hayo kwani mimi sina kambi wala kundi and i have submitted myself to the existing leadership.

Wenye ugonjwa wa Zittophobiasis watafute dawa tu as i wont give you the lines to attack. All my efforts are directed towards party building.

Mgombea yeyote ambaye atajisema eti ni wa Zitto nawaomba vijana wamkatae na wachague mtu wa CHADEMA na sio mtu wa kundi lolote.

Nawatakia wagombea wote ushindi mwema na ninawatakia vijana wote wa CHADEMA uchaguzi makini utakaoonyesha sura chanya ya chama chetu.

Zitto Kabwe
Naibu Katibu Mkuu Taifa
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Just be confident with what your soul tells to do; dhamira njema ni taa ya miguu yako, dont be moved by other people's wishes. I pray for your success in whatever you plan to do. May you realise your destiny as earlier as it could be. May the Peace of God rest and abide with you forever more!
 
Ben ni ukomavu gani unaosema Zitto kaonyesha kususia mchakato ni ukomavu na wewe ukichaguliwa halafu baadae ukasusia vikao unataka tukuone ni mkomavu kisiasa, na kama viongozi wote wakitoa msimamo kama huo nani basi atasimamia uchaguzi wenu. Mimi naona Zitto kaonyesha weakness fulani au ana kinyongo kutokana na matokeo ya uchaguzi uliopita kiongozi/kamanda huwa hasusii wapiganaji wake.

Hivi huyu Zitto ameumbwa na moyo wa chuma? Please give him a break! Ameeleza kwanini hajajihusisha kwamba anahisi his involvement inaweza tumiwa vibaya na wengine wenye evil thoughts na hivyo kuamua kufanya hivyo kwa dhamira njema kabis ili chama kisije ingia tena kwenye malumbano. Bado mna msukuma huku na kule as if yeye five senses zake zimetiwa ganzi. Achane hizo bwana mpeni nafasi na yeye ana moyo wa damu na nyama na kuona kuwa anathaminiwa na kupewa nafasi ya ku express feelings zake hasa kama alishapata bad experience ni sehemu ya demokrasia na uongozi uliotukuka. Ndiyo maana watu wakiwa na conflicting interest wana eleza na wanapewa nafasi ya kujiondoka katika involvement ya hizo issues. Tuache too much nagging, night picking and unecessary complains kwenye mambo ambayo yako wazi na yakueleweka na watu wazima.
 
Zitto unanifurahisha kweli kwa nini unashangaa Juliana Shoza kutajwa au ulikuwa na maana gani tuseme basi kuna watu wako ambao unataka washinde ndiyo maana unashangaa kusikia mwingine akitajwa...........umeshangaa kusikia jina la Juliana na mimi nakushangaa unavyoshangaa..............

Hivi ni vigumu hivyo kuuelewa mfuatano wa maelezo haya??Feedback vip?

mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. ..

Taarifa zilizopo; 1. Juliana Shonza 2. .......

Nami nimesikia nikashangaa!
 
Wakuu zangu,
labda nwafahamishe tu kwamba vyama vyote duniani viongozi wa juu huwa na makundi ndani ya chama na mara zote kila mmoja wao huwa ana pendekezo lake. Msiwe wachawi ktk maadili ya demokrasia, hivi kweli wewe unaweza piga kura kumchagua mtu unayemjua pasipo kupendelea mtu huyo achukue madaraka? hivi kweli mnataka Zitto achague mtu kutokana na sifa gani kama sii kumjua vizuri mgombea!.. mbona vijana wa Chadema mna mizengwe isiyokuwa hata na maana...

Ni lazima na inamlazimu Zitto na viongozi wote wa Chadema kuwa na mapendekezo yao ktk nafasi zote za uoongozi hata iwe kuchaguana wao wenyewe. Na kama Zitto hampendi Mbowe au Dr.Slaa wachukue Uenyekiti haina makosa na ndiyo denokrasia yenyewe kwa sababu ni haki yake ya kimsingi kama ilivyo haki kwa wengine watakao mchagua Mbowe au Dr.Slaa. Na iIjwe kwao hao wengine wasiwe na makundi ikiwa nao watapendekeza majina ya watu wengine?

Kusema kweli Chadema na uongozi wake walifanya makosa makubwa sana ya kikatiba na demokrasia kwa Kafulila na Zitto kwa sababu ati Zitto alimpigia pande Kafulila sasa mlitaka iweje?.. Kila mjumbe mpiga kura anatakiwa kuwa na chaguo lake, hata iwe mtu wake wa karibu na kundi moja kwa sababu ndani ya chama kuna issues ambazo kila mgombea huwa ni vipaumbele vyake na ndivyo vinavyoweza kumvutia mpiga kura au hata kuwa kundi moja..Haiwezekani watu wote ndani ya chama kuwa na msimamo mmoja -haiwezekani na kama inawezekana basi hakuna sababu ya uchaguzi wa kura bali wagombea wangeteuliwa.

Acheni upuuzi wa kumtafuta mtu ili hali kasema Zitto basi kila mtu anatafuta kusema ovyo... Kajitoa maneno tena mnayakoroga kisawasawa. angebakia tayari mmeshampachika kundi lake - Hivi mnataka Zitto afanye nini ili mfurahi?...
Huyo Mbowe, Mnyika, dr.Slaa na wengine wote ndani ya Chadema wana vijana ambao wanataka washike wadhifa fulani kutokana na jinsi wanavyokubaliana nao na sii lazima hawa viongozi wote wawe na chaguo moja, unless kuwepo na uchakachuaji au makubaliano kabla ya uchaguzi. Hii haitakuwa uchaguzi halali hata kidogo, isipokuwa hawa vijana wanatakiwa wafanye kampeni zao kuwavuta hawa wajumbe na mara nyingi uwezo wao kutambulika kabla ya hizi kampeni.

Jamani hata Obama na mama Clinton walikuwa na Senators ambao waligawanyika ktk makundi ya kumpa support mmoja wao vile vile wao wenyewe Obama na Clinton walikuwa na Senators ambao walikuwa kundi moja iweje huko pasiwe na tatizo isipokuwa Chadema?.. Hizi ni siasa za CCM, chama ambacho lazima ukubaliane na mtawala laa sivyo utatupwa nje kama kina Abdallah Kigoda..Haifai siasa za chuki!

Na hakika kwa mtazamo wa kiitikadi
 
Hivi huyu Zitto ameumbwa na moyo wa chuma? Please give him a break! Ameeleza kwanini hajajihusisha kwamba anahisi his involvement inaweza tumiwa vibaya na wengine wenye evil thoughts na hivyo kuamua kufanya hivyo kwa dhamira njema kabis ili chama kisije ingia tena kwenye malumbano. Bado mna msukuma huku na kule as if yeye five senses zake zimetiwa ganzi. Achane hizo bwana mpeni nafasi na yeye ana moyo wa damu na nyama na kuona kuwa anathaminiwa na kupewa nafasi ya ku express feelings zake hasa kama alishapata bad experience ni sehemu ya demokrasia na uongozi uliotukuka. Ndiyo maana watu wakiwa na conflicting interest wana eleza na wanapewa nafasi ya kujiondoka katika involvement ya hizo issues. Tuache too much nagging, night picking and unecessary complains kwenye mambo ambayo yako wazi na yakueleweka na watu wazima.
Sawa lakini kama ameamua kujitenga na mambo ya uchaguzi kwa nini basi anashangaa anaposikia majina ya wengine yakitajwa tajwa kama yuko neutral kwa nini asikae kimya kusubiri matokeo? au alitaka asikie jina la nani ndipo asishangae, anapowashangaa wagombea wengine ina maana hayuko neutral hiyo ndiyo implication yake yeye kama kiongozi anapeleka ujumbe gani kwa Juliana na wagombea wengine kuwa Juliana hafai na Juliana atakuwa anamfikiriaje kiongozi wake Zitto.
 
Chadema mzee Mtei ametutoa mbali mamluki kwetu mwiko_Ole wao watakao ingia kwenye uongozi wa BAVICHA kwa kashfa na kama watakuwa Mamluki sisi kitengo muhimu cha CDM hatutavumilia kwani sisi tunaona Chama pekee ambacho kinatupatia uhuru na haki,amani na mwanga wa maisha ya baadaye ya watoto wetu ni CHADEMA.Nipo tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya Uhai wa chama changu.NAOMBA WAGOMBEA WOTE WA UONGOZI NDANI YA BAVICHA KAMA KUNA YEYOTE ALIYETUMWA BASI AJIENGUE Mwenyewe kabla ajaingia kikaangoni.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU WABARIKI VIJANA WA TANZANIA Na MUNGU IBARIKI CHADEMA Amen.

Mkuu naheshimu sana, ulichosema na kwa hisia kali sana!
Pia nadhani kuna msisitizo zaidi uwekwe,
Kwamba ole wake atakayekihujumu CHADEMA na kukidhohofisha.
Na kusababisha ndoto zetu za 2015 zikatoweka na kukwama.
Ole wa huyo mtu!
BAVICHA ni moyo wa chama, ni chombo kitakatifu sana​
 
Sawa lakini kama ameamua kujitenga na mambo ya uchaguzi kwa nini basi anashangaa anaposikia majina ya wengine yakitajwa tajwa kama yuko neutral kwa nini asikae kimya kusubiri matokeo? au alitaka asikie jina la nani ndipo asishangae, anapowashangaa wagombea wengine ina maana hayuko neutral hiyo ndiyo implication yake yeye kama kiongozi anapeleka ujumbe gani kwa Juliana na wagombea wengine kuwa Juliana hafai na Juliana atakuwa anamfikiriaje kiongozi wake Zitto.

Feeback ndugu yangu, hebu cheki post ya mwisho ya "Butola"
Pia mwanzoni sikuelewa kama wewe ila naona "Butola" amenisaidia sana,
Nimeelewa mtiririko wa conversation kati ya Zitto na Mdau.
Kama kweli una nia ya kuelewa basi ukicheki hapo utaelewa vizuri sana.
 
Ngoma inayochezwa na Zitto na Kitila….
Mkakati wa Zitto na Kitila kuweka viongozi vibaraka katika BAVICHA ulianza siku nyingi sana...Mathalani, waliweza kuteka mchakato mzima wa uanzishwaji wa tawi la CHADEMA katika elimu ya juu, ambao mojawapo ya waanzilishi wake, Mnyika, Suzan Lyimo na Mdee waliwekwa pembeni kinamna… Zitto na Kitila waliizunguka Kamati Kuu, ambayo ilitakiwa kutoa baraka zake; kwa kuiingiza mkenge kwamba kinachozinduliwa ni Tawi wakati ukweli ni kwamba ilikua ni Association...Ikumbukwe mwanzoni kabisa alitumiwa kijana mmoja kuuza wazo hili kwa vijana na wanaharakati wengine wa CHADEMA...Kijana huyu (Emanuel); ambaye kwa kuweka kumbukumbu sawa; ni yule ambaye baadae gazeti la Mwanahalisi liliwahi kuripoti kwamba aliomba kazi ya kuiua CHADEMA…Kijana mwingine aliyeshiriki hatua za awali za mkakati huu anaitwa Mwakajila, ambaye kwa sasa ni katibu wa Zitto…
Muendelezo huu haikuishia hapo, uzinduzi wa CHASO uliweza kumsimika kama mwenyekiti, dada aitwaye Juliana Shonza, ambaye taarifa za kuaminika zinadai kwamba ni kimada wa Zitto na aliunganishiwa na Kitila…dada huyu alionekana pia katika Operesheni iliyoisha ya CHADEMA katika Nyanda za Juu Kusini, ambapo katika tukio zaidi ya moja, Zitto alimtambulisha “kiaina” katika hali ambayo iliyoashiria kama kumpigia kampeni…zipo taarifa kwamba, alitumia muda mwingi akiwa na Zitto na pia aligharamiwa pesa na usafiri…mwingine katika mpango wa Zitto/Kitila anatajwa kuwa ni Habib Mchange, mgombea nafasi ya mwenyekiti BAVICHA na mojawapo ya wagombea ubunge wa 2010 waliopata fursa ya kupigiwa kampeni na Zitto toka jimbo la Kibaha…
Uswahiba wa Kitila na Zitto unatajwa kama ni wa kimkakati zaidi, lakini mojawapo ya habari za nyuma ya pazia ni kwamba wote kwa pamoja, au kwa utofauti, wanajipanga kwa ajili ya nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA…baadhi ya wadau wamekua wakihoji pia uwezo alionao Kitila wa kusimamia michakato ya kisiasa ya CHADEMA na pia ya Taifa kwa ujumla, hasa midahalo mbalimbali toka Chuo Kikuu, kwani wamekua wakiamini kwamba kwa kufanya hivyo, angeingia katika utata na serikali, ambayo wakati wote, imekua ikiminya uhuru wa wasomi maarufu walio katika ajira yake kuiamsha jamii, hali haiko hivyo kwa upande wa Kitila...Zitto yeye tayari ana tuhuma kadhaa za kutenda au kusema tofauti na chama chake, hali ambayo katika siku za karibuni, imepelekea kushuka kwa kasi kwa umaarufu wake, hasa kwa vijana walio wengi...(taarifa nyingine za kuaminika ni kwamba katika mkoa wa Mbeya, kuna eneo mojawapo ambalo vijana walijipanga kumkataa endapo angepanda jukwaani,lakini hakutokea)…Hivyo basi, wachunguzi wa mambo wanaangalia kwa makini sana mchakato unaoendelea BAVICHA, na muelekeo wa CHADEMA kwa ujumla.

Haya ni zaidi ya matapishi unayoleta humu jf...mbona huulizi juhudi za lema kumtunza na kumnadi heche waziwazi huku uongozi ukijua na hauchui hatua, zito kashasema yeye hataki kujihusisha na uchaguzi huu, je umetumwa na nani utupe ogoro wako huu.
Je unajua juhudi za mdee na kiwelu juu ya bavicha au unaropoka kwa kukariri tu.
 
Back
Top Bottom