Lowassa, ninaamini ni kama enzi zile Kitine, bado haelewi vizuri bongo na siasa zake, lakini very soon ataelewa manaa na Salmin naye wakati fulani alidhani ana nguvu sana na anaweza kujipa term ya tatu, mpaka siku moja alipoitwa cc na kuambiwa ajitoe na ujinga,
Lowassa, ameharibu jina lake kwa kujiuzulu kutokana na ripoti mbaya dhidi yake, kama kweli angekuwa na akili kubwa ya siasa, basi angeizuia ripoti mapema kwa ku-negotiate surrender hata kabla kamati ya Mwakyembe, haijaundwa au hata ilipoundwa angetumia nafasi yake kisiasa na kiserikali, kumuomba muungwana amuondoe kistaarabu mapema kabla ya kufikia mwisho wa ripoti, ripoti isingekuwa na nguvu sana as long as Lowassa, angekuwa ametoka mapema, huenda hata isingepelekwa bungeni, kwa sababu marafiki zake wangeweza ku-negotiate isitolewe kabisa since alishajiuzulu au kutolewa na rais mapema, lakini kusubiri mpaka mwisho halafu ndio aanze kampeni za kujisafisha anapoteza hela zake bure masikini ya Mungu, na wabongo they are very good at playing na watu wenye hela za mchezo kama huyu, huku wakijua kuwa wanachomfanyia ni impossible,
Hawezi kurudi tena kwenye power haitakuja kutokea, hata akiingia upinzani hakuna wa kumfuata huko kati ya mawaziri walioko kwenye power sasa, kosa lingine kubwa sana alilolifanya ni kukosa umakamu wa ccm, maana angekuwa nao, sasa hivi asingekuwa na tatizo la kurudi kwenye power ccm, ukweli ni kwamba he is done maana kina Pinda watampa vipi hiyo nafasi? cc haingii tena sasa unakuwaje powerful bongo kama huingii cc? Six naye sasa nasikia anataka urais pia, na mkuu pale nje naye nasikia yumo njiani, wenziwe wote bado wako kwenye power, yeye tu ndiye yuko nje halafu wampe nafasi ya kurudi?
Mimi ningemshauri,apumzike kwanza ili siasa zimfuate na sio yeye kuzifukuzia kiasi hiki, mbona kina Diallo wametulia kimyaaa!