Kamati Kuu ya CCM fanyeni maamuzi magumu. Mpumzisheni Rais Samia, Serikali yake ni kigeugeu!

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,529
17,441
Alianza kwa kasi Sana na tuhuma za ugaidi Hadi nchi yetu ikaanza kujulikana kwa tishio la ugaidi kwa mataifa ya nje, na kesi akamfungulia mtuhumiwa Mwisho wa siku kesi ikayeyuka na mtuhumiwa hatari wa ugaidi KILA siku anakaribishwa ikulu Sasa unajiuliza Mbowe aliyekuwa Gaidi Ndio huyu wa kwenda Ikulu?

Kifupi alichemka Sana! Makada tukaugulia aibu kubwa ya kubezwa kwamba hatuna consistence kwenye maamuzi.

Akacheza royal tour kwa mabilion Ili yavutie watalii. Hatukusikia hao watalii waliovutiwa waliingiza sh. Ngapi na zinafanya Nini Hadi leo! Ndio KWANZA Tozo zikaingizwa kwenye mzunguko na Maisha yakawa magumu Hadi leo na Royal tour imekufa kibudu kama hivyo na imeshasahaulika kama ilokuwepo maana kinachozungumzwa ni Tozo tu!

Haya akaja kwenye bei ya mafuta Sasa! Hapa tukaambiwa mafuta yatashuka Bei! Wakaingiza kama Bilion 100 Ili zishushe mafuta lakini wapi mafuta hayakushuka na wananchi tunavosoma namba kweli kweli!akafeli Tena!

Juzi akaja na Tozo kwa wananchi tumekamuliwa weeeeeh!Sasa malalamiko yamekuwa meeeengi Sana leo wanajisifu tena KWA kuondoa Tozo KWA asilimia 50.sasa sisi tunajiuliza haya maamuzi anayatoa wapi ambayo hayana TIJA KWA NCHI yangu Tanzania?

Wakaja na kauli ya 23% ambayo Mwisho wa siku ikawa 2.3% yaani hakuna consistence kwenye MAAMUZI yaani hakuna mwendelezo wa maamuzi ni kama Wana beti tu hawana uhakika kwenye maamuzi.

Sasa rudini chimwaga sasa maana hatuwezi kuongozwa na watu wanaobeti kwenye maamuzi bila kuwa na uhakika nao!

Hata huyo makamu nae hatoshi juzi amebwatuka na kuleta taharuki tena bila uchunguzi wa kina!

Niiombe KAMATI kuu ikapige kura na kuja na mbadala mambo hayapo sawa kabisa!

Namalizia hivi

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Ngoja narudi muda siyo mrefu maana wewe unautani na sisi watanzania juu ya Rais wetu mpendwa mama samia Suluhu Hassan tunayempenda na kumkubali kwa utumishi wake uliotukuka na uliogusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti, kumgusa au kumsema vibaya mh Rais wetu mpendwa Ni sawa na kufifisha sauti zetu, mama ndio sauti yetu mamilioni ya watanzania
 
Jibu hoja

Hapo ndio vijana wa ccm mnachemka Sana, Yan hamjui kujibu Hoja

Ww unaleta masifa meeengi ya hewani wakati mwenzako amekuja na vitu vinashikika
 
Hahaaaaa!!! Shida Iko pale kwenye kofia mbili!!!

Yaani aongoze aongoze kikao Cha kumuondoa Yeye mwenyewe!!!

Labda Chama Cha Mapinduzi kujipindue chenyewe kama Jina lao lilivyo.
Lolote linawezekana!kama wenye viti wa ccm mkoa mzima wanaweza toa matamko ya kutokuwa na imani Nae halafu kinana aka type BARUA ya kujiuzulu uenyekiti wa Mama wa ccm!si TAYARI wanamalizia tu KAZI!!!?
 
Mwigulu ndio pekee anastahili kuondolewa. Watu wanaondoa pesa zao benki, Sasa raia wasipoweka pesa benki serikali itajuaje ukubwa wa currency in circulation?

Waulize voda na tigo watakuambia Hali ni tete kule Mpesa, kisa MTU mmoja anayesema ana PhD ya economics lkn Mambo madogo kabisa anashindwa kuyaelewa.

Siwezi ruhusu mwanangu asomee PhD alikosoma Mwigulu.
 
Serikali ya mama inajing'atang'ata.

Ishu ya mishahara walikuja na mbwembwe wakaishia kuzingua

Ishu ya tozo za mabenki tulitegemea wangeziondoa, wao wamefanya cosmetic changes. Tozo za benki ziondoke, ni double taxation kwa sababu pesa zetu tayari zinakatwa 18% VAT, na kwa wale wa mishahara ya serikali tayari zishakatwa PAYE
 
Ngoja narudi muda siyo mrefu maana wewe unautani na sisi watanzania juu ya Rais wetu mpendwa mama samia Suluhu Hassan tunayempenda na kumkubali kwa utumishi wake uliotukuka na uliogusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti, kumgusa au kumsema vibaya mh Rais wetu mpendwa Ni sawa na kufifisha sauti zetu, mama ndio sauti yetu mamilioni ya watanzania
Sauti yenu dhidi ya Nani? Una maana kinachozungumzwa na watanzania walio wengi hakipo? Ukiwa Pro-goverment jitahidi kupima uzito wa jambo unalolizungumza au kuandika mbele ya umma! Vinginevyo watu watadhindwa kutofautisha werevu na ujinga waki
 
Serikali ya CCM ndio sauti ya watanzania wanyonge, ndio sauti ya wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu ,Tumaini kwa waliokata Tamaa na faraja kwa walio na huzuni
 
Kamati kuu haina uwezo wa kusema chochote kuhusu Rais ambaye ni Mwenyekiti wao. Anayeweza kuongea kitu ni Mkuu wa majeshi tu kama kuna umuhimu huo na akasikilizwa hao kamati wanafuata mwenyikiti anachofikiri - ni utamaduni wao mwenyekiti hapingwi.
 
Back
Top Bottom