Kamati Kuu (CCM) yawaonya wataka urais

Kamati Kuu (CCM) yawaonya wataka urais

Waroho wa madaraka ni CCM bara mbona wenzao wa visiwani wametulia huwezi ukawasikia wanapigana vikumbo kwa ajili ya urais.Ulafi wa madaraka utaipeleka CCM pabaya.Kama CCM ni watenda haki na wanaoheshimu taratibu walizojiwekea wenyewe wawamwage CCM bara wote wanaopigana vikumbo kwa ajili ya urais wawatendee haki CCM Zanzibar kwa kuwapa nafasi ya kuwakirisha chama chao kwenye urais kwani ndio waliotimiza vigezo vyote vinavyotakiwa na CCM.
 
Maccm yanatapatapa tu! Yameshachoka yakachakaa tuyapumzishe tu 2015
 
Wanataka URAHISI wa Tanzania wakati hawajui hata sheria, taratibu na kanuni za chama chao!!?? Kwa kweli Watanzania tuna kazi kubwa sana na hawa maCCM!!
JK amefanya Urais kuonekana ni kitu kisicho na maana kabisa. Kuna watu wanachukulia Urais wa Tanzania sawa na biashara ya Uji wa Ulezi... Hata kwa mtaji wa Elfu mbili unaweza kuifanya.
 
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)

Umeniacha hoi Mkuu kwa uchambuzi wako murua - Asante sana.
 
Ni kawaida kwa magamba kila mtu kusema la kwake, ngumu sana kuwaelewa, ya Askofu Kakobe yanatimia - mnara wa Babeli.
 
Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)

Kila siku wanaongea wasichomaanisha. Kuvua gamba, oh mara Mangula kasema walotoa rushwa atawaondoa, mara maisha bora kwa kila mtanzania, mara reli itajengwa upya, mara uwanja wa ndege wa kimataifa misenyi! Duh! Usishangae wakaja wakaibuka na kauli kuwa waliokuwa wanatangaza kugombea walikuwa wanatekeleza imani ya chama
 
Miccm ikiongea hata usiisikilize maana wakiongea leo kesho yake wanaikana kauli yaani ni kama wana mipepo kila mmoja likimpanda anakuja na kauli yake yaan ovyo ovyo tu.
 
Mr Zero itakuwaje hawajui sharia na wamezutunga wenyewe. Bora useme wanavunja sheria, na utuwekee hiyo sheria waliyoivunja inasemaje

Sasa mtu kama Wasira atasema anazijua sheria eti amehusika kuzitunga wakati mudawote kasinzia?
 
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)
Ipo kwenye ilani hii kuwa na mitizamo mingi ndani ya chama
 
Majina ya wajumbe saba wa kamati kuu (CC) ya CCM kutoka Bara ni:
1. Pindi Chana
2. Adam Kimbisa
3. William Lukuvi
4. Dk. Emmanuel Nchimbi
5. Jerry Slaa
6. Prof. Anna Tibaijuka
7. Stephen Wassira

Kutoka Zanzibar, wajumbe saba katika CC ya CCM ni:
1. Shamsi Vuai Nahodha
2. Dk. Hussein Mwinyi
3. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dk. Salim Ahmed Salim
5. Dk. Maua Daftari
6. Samia Suluhu Hassan
7. Hadija H. Aboud

Kwa utaratibu wa CCM, wajumbe wa CC ndiyo wenye rungu la kuchuja majina ya wagombea wote wa urais kupitia chama hicho ambapo mwishowe hupeleka majina ya mwisho ya wale wote wenye sifa kwenye mkutano wa halmashauri kuu (NEC) ili hatimaye kubaki na mgombea mmoja anayepeperusha bendera ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu.

Hivyo, ni wajumbe hawa 14 ndiyo watakaoamua hatma ya wagombea urais wa CCM, kwani wanao uwezo wa kufyeka jina la mgombea yeyote kwa sababu watakazoona kuwa zinafaa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 utakapoanza kwa kusaka wagombea ndani ya vyama, kikiwamo CCM .Kwa muktadha huo ni nini hatma ya mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru?

Vipi kuhusu ushawishi wa Mkuu wa kaya JK juu ya kamati hii katika kupitisha jina la mgombea urais kwa tiketi ya CCM? ni nani yupo kwa nani na kwa nini?

Nini msimamo/uthabiti wa kila mjumbe linapokuja suala la hela? Mathalani kuhongwa ili apitishe jina fulani?

Tujadili.
 
Hiyo Kamati Kuu ya CCM niya mwaka gani katika msingi wa Katiba ya CCM ya mwaka gani?.

Unapotaka kuleta hoja ambazo zinabebwa na documents, jaribu kufanya homework kabla ya kuibuka hapa Jamiiforums.

Nani amekuambia Kamati Kuu ya CCM ina wajumbe 14?.

Are you BAVICHA in making?
 
Kama wajumbe ndio hao, ninakuhakikishia 100% Lowassa ndio mgombea urais wa CCM. Mtu pekee ambaye sio kambi ya Lowassa kwa uhakika hapo ni Salim Mohamed Salim.
 
Back
Top Bottom