Majina ya wajumbe saba wa kamati kuu (CC) ya CCM kutoka Bara ni:
1. Pindi Chana
2. Adam Kimbisa
3. William Lukuvi
4. Dk. Emmanuel Nchimbi
5. Jerry Slaa
6. Prof. Anna Tibaijuka
7. Stephen Wassira
Kutoka Zanzibar, wajumbe saba katika CC ya CCM ni:
1. Shamsi Vuai Nahodha
2. Dk. Hussein Mwinyi
3. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dk. Salim Ahmed Salim
5. Dk. Maua Daftari
6. Samia Suluhu Hassan
7. Hadija H. Aboud
Kwa utaratibu wa CCM, wajumbe wa CC ndiyo wenye rungu la kuchuja majina ya wagombea wote wa urais kupitia chama hicho ambapo mwishowe hupeleka majina ya mwisho ya wale wote wenye sifa kwenye mkutano wa halmashauri kuu (NEC) ili hatimaye kubaki na mgombea mmoja anayepeperusha bendera ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu.
Hivyo, ni wajumbe hawa 14 ndiyo watakaoamua hatma ya wagombea urais wa CCM, kwani wanao uwezo wa kufyeka jina la mgombea yeyote kwa sababu watakazoona kuwa zinafaa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 utakapoanza kwa kusaka wagombea ndani ya vyama, kikiwamo CCM .Kwa muktadha huo ni nini hatma ya mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru?
Vipi kuhusu ushawishi wa Mkuu wa kaya JK juu ya kamati hii katika kupitisha jina la mgombea urais kwa tiketi ya CCM? ni nani yupo kwa nani na kwa nini?
Nini msimamo/uthabiti wa kila mjumbe linapokuja suala la hela? Mathalani kuhongwa ili apitishe jina fulani?
Tujadili.