Kamati Kuu (CCM) yawaonya wataka urais

Kamati Kuu (CCM) yawaonya wataka urais

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)
 
Wanataka URAHISI wa Tanzania wakati hawajui hata sheria, taratibu na kanuni za chama chao!!?? Kwa kweli Watanzania tuna kazi kubwa sana na hawa maCCM!!
 
Huyu JK bana sijui nani mshauri wake..mbona Pinda hajaonywa maana naye amekutana na wazee na kakubali kuchukua form..
 
Ccm itahandle kwa utaratibu muhafaka na mambo yatatulia. Kule kwetu cdm hapa watu washaanza kufkuzana
 
Tafadhari bwana ................... hata Pinda anautaka URAHISI wa nchi hii!!
 
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)

We mselewa hatukushangai we ni mchumia tumbo tushakuzoeya,habari umekimbia kuileta humu jamvin wakati haijakamilika,daima we nshakuzoeya ni mchumia tumbo namba moja
 
Ccm itahandle kwa utaratibu muhafaka na mambo yatatulia. Kule kwetu cdm hapa watu washaanza kufkuzana

Utaratibu upi? Ule wa alioufuata Januari, Nape alisema upo sahihi na leo amegeuka!! Shtuka!
 
We mselewa hatukushangai we ni mchumia tumbo tushakuzoeya,habari umekimbia kuileta humu jamvin wakati haijakamilika,daima we nshakuzoeya ni mchumia tumbo namba moja

We kweli kiloriti!
 
Last edited by a moderator:
We mselewa hatukushangai we ni mchumia tumbo tushakuzoeya,habari umekimbia kuileta humu jamvin wakati haijakamilika,daima we nshakuzoeya ni mchumia tumbo namba moja

Mkuu kiloriti aka Kibaraka wa Lowassa,habari hii haijakamilika wapi? Kama wewe ni mchumia tumbo,si wote. Mimi nimesoma na kupata kazi kwa uwezo wangu.Napata mshahara halali. Si kama wewe ambaye huli hadi uweke bandiko humu jamvini
 
Last edited by a moderator:
Wote hao ni wafanya harambee mtu sahihi ni magufuli
 
Wanataka URAHISI wa Tanzania wakati hawajui hata sheria, taratibu na kanuni za chama chao!!?? Kwa kweli Watanzania tuna kazi kubwa sana na hawa maCCM!!

Mr Zero itakuwaje hawajui sharia na wamezutunga wenyewe. Bora useme wanavunja sheria, na utuwekee hiyo sheria waliyoivunja inasemaje
 
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)

hawa CCM wanaogopa kauli ya mwanaume mmoja anaitwa Lowasa
 
Mkuu kiloriti aka Kibaraka wa Lowassa,habari hii haijakamilika wapi? Kama wewe ni mchumia tumbo,si wote. Mimi nimesoma na kupata kazi kwa uwezo wangu.Napata mshahara halali. Si kama wewe ambaye huli hadi uweke bandiko humu jamvini

Mselewa afadhali ya mimi kibaraka wa lowassa kuliko wewe kibaraka wa hawara ya mbowe joyce mukya.jipange kaka acha kukurupuka umesoma lakin shule uliyo nayo haukusaidia
 
Last edited by a moderator:
Mselewa afadhali ya mimi kibaraka wa lowassa kuliko wewe kibaraka wa hawara ya mbowe joyce mukya.jipange kaka acha kukurupuka umesoma lakin shule uliyo nayo haukusaidia

Uliowataja wote hata hawanijui.Nami nawaona kwenye luninga na magazetini tu. Mkuu kiloriti,katika habari yangu hii kipi kimekuchoma?
 
Last edited by a moderator:
Yawataka wanaotaka kugombea Urais wafuate Sheria,Kanuni na Taratibu za chama kinyume na hapo wote wataenguliwa kutoka katika mchakato wa kichama. Ni Nape Nnauye tena aliyeibuka na tamko hili baada ya kunukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini akisema kuwa Januari Makamba hakuwa amevunja taratibu zozote kutangaza nia ya kuutaka urais mapema. Pia,Kamati Kuu imeiagiza Sekretarieti kuchambua utekelezaji wa adhabu ya akina Lowassa,Wassira na Ngeleja.

Kutoka CCM,cha kushika ni tabu sana. Kila siku kuna kauli mpya na lengo jipya. Ngumu kupata uelewa

Chanzo: DW Radio (George Njogopa)

mleta mada umevurugwa nyuma
 
Afya ya Dr. Mwakyembe na Prof. Mwandosya zaimarika wakati ya Lowasa inazidi kuzorota.
Dah....nawaza sana kuhusu hâta mambo
 
Back
Top Bottom