Tetesi: Kamata kamata michango ya ujenzi wa shule Kagera

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,763
35,731
Mabibi na mabwana hii imekaa je.

Pana habari tokea pande za wilaya ya Ngara kuwa wanakamatwa watu hovyo kisa 10,000/= michango ya ujenzi wa shule hasa pande za kule Rusumo.

Sheria zipi zinazohalalisha unyanyasaji huu? Au ni moja ya zile amsha amsha katika ziara ya lile jembe letu mkoani Kagera katika mitano hii?

Kulikoni hizi sera hatuoni zinapaka matope kwenye ile mitano tena hasa pale tunaposubiria midege mingine tuliyokwisha lipa kwa cash money?

Ikumbukwe pia kuwa wengi wa hawa wanaokamatwa ndiyo wale waliopiga kura za ndiyo kweli kweli.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
1610952570384.png




Nguvu zilizowaweka madarakani ndizo wanazotumia kuendesha nchi.
 
Wanawakamata na kuwapeleka wapi?
Huo mchango Ni lazma au hiari?

Iuzwe dream liner tujenge madarasa.

Wana selo. Huko ndiko inakoarifiwa wengine wamelala.

Walioshindwa kulipa wamelazimika kutimua mbio kwenda mafichoni.

Boda boda imebidi kughairi kazi.

Mitano ya ukweli!
 
Naomba kujua mchango serikali kuu janga tetemeko Kagera, Waingereza walitoa pole kwa kutujengea upya Ihungo sekondary.
 
Kuna vitu. Mnanalalamika kumbe wamekaa wenyewe na wakakubaliana kabisa alafu mnaleta lawama huko pambanane na hali zenu
 
Back
Top Bottom