Kamari imekuwa mkombozi wa Taifa

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Ukweli lazima usemwe bila woga bila kamari nchi hii hakuna maisha, iwe kwa vijana au wazee wake kwa waume! Kamari imekuwa tegemeo la uchumi na mapato ya serikali.

Bila kamari vyombo vyote vya habari ikiwemo TBC haviwezi kulipa mishahara ya watumishi wao. Bila kamari serikali haiwezi kulipa mishahara ya watumishi wake.

Hakika kamari ni ukombozi wa Taifa!
 
Umekuwa unawaza Kama Mimi mkuu.
Kamali imekuwa kazi lasmi.ila kwa mbali sisi wasee wa kubeti same time inatuokoaga ila kwa mahesabu ya mbaaaali ili usiwe mlevi WA hizo kazi.

Mpaka TBC TAIFA🙃🤣🤣🤣🤣Nnilichoka mkuu.

Acha tuendelee mkuu,maana kwa Sasa kampuni za bet ndo zenye mkwanja mlefu kuzidi hadi taasisi za Bank huwezi amini.
Tatizo ni pale vijana watu wamegeuza vyanzo vya mapato ambapo ni hatari kubwa Sana.
Kipindi Cha nyuma,nilikuwa cjui pale nikisikia mtu analalamika eti "Daah wasenge Hawa wamenichania mkeka wangu".
Nikakua nikajua kutafuta hela,weeeeeeeeeeeeeeee,mikeka niliijua kuzidi masomo niliyowahi kusoma class😄😄😄😄😄😄.
Sio mbaya ila ni mbaya.
Taifa lijitafakari.
 
Nilikuwa naangalia kituo kimoja cha luninga kwenye kipindi chao kimoja hivi walipomaliza wakaishia kutangaza watu wacheze bahati nasibu yao watapata fedha za sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka. Wengine kila baada ya taarifa ya habari wanahamasisha watazamaji wao wacheze bahati nasibu yao. Wacheza kamari wapo wamewapata wawachezeshe, sie wengine hatuna muda wa kucheza kamari hizo na hatutaki kuchezea hela zutu
 
Kama hii
Ilibidi usindikize na kapicha ka vijana kwa wazee wakichambua mikeka.
tapatalk_1674496590971.jpeg
 
Back
Top Bottom