Kamarade Mkili Gervas ametutoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamarade Mkili Gervas ametutoka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by omarilyas, Sep 7, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nasikitika kuwataarifu wanahrakati wote wa UDSM miaka ya mwishoni mwa 90's na mwanzoni mwa 2000's kuwa rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi wetu mpendwa Kamarade MKILI GERVAS ametutoka jana Jumapili asubuhi baada ya kupata mshtuko wa moyo. Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Salasala, Dar Es Salaam karibu na kanisa la TAG na mwili wa marehemu utasafirishwa leo jioni kwa mazishi kijijini kwao katika wilaya ya Kahama mkoni Shinyanga. Hadi anapofariki, Mkili alikuwa mkuu wa shule ya Green Acres iliyopo Mbezi Salasala.

  Tunamkumbuka Mkili kama mpambanaji makini na madhubutu ambaye alituongoza katika mapambano mengi hapo mlimani. Namkumbuka Mkili kama kiongozi niliyempinga katika uchaguzi wa urais wa DARUSO na baadaye kumpigania nafasi ya Ukatibu Mkuu ambapo aliweza kusiamama nasi hadi mwisho bada ya yule tuliyemuamini kwa Urais kutuacha solemba tukiwa Nkurumah.

  Mkili hakukata tamaa na kuendelea na mapambano hata pale tulipokuwa wanted na baadaye kusimamishwa chuo miezi sita ambapo Mkili alikula miezi tisa na baadaye kuwekwa ndani kwa kesi ya uchochezi ambayo ilipelekea mogomo mwingine uliofanikiwa kushinikiza kuachiwa kwake na wenzake waliokuwa wakielekea kutimuliwa chuo kutokana na mwenendo wa kesi yao.

  Mkili alikuwa ni kiongozi madhubutu na mwenye nidhamu ya hali ya juu ambaye neno uoga halikuwemo katika fikira zake.

  Wapambanaji wengi wamepitia na kukomaa katika siasa za UDSM, Mkili anasimama kama mmoja wa vinara wake ambao mapambano yao yalikuwa ni ya dhati na sio kujitengenezea CV kama ambavyo wengi tuliwaona na tunaendelea kuwaona.

  Kwa taarifa zaidi na michango yenu wasiliana na Goodluck 0713 322058 au Galani 0713 505941

  Rest in Peace


  Omarilyas
   
 2. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  RIP Mkili. Nakulilia. Wewe ni mmoja wa wazalendo halisi wa TZ. Nenda nyota. Kawasalimu Nyerere na Sokoine. Waambie tuko ktk mapito tu kwa sasa. Hatimaye tutaipeleka nchi kunakostahili. Kwenye neema ya kweli kwa watanzania wote. Ari yenu ndiyo yatutia moyo wapiganaji na vita hii ya kuikomboa nchi toka mikononi mwa mafisadi, wezi, wala rushwa na vibaraka wa wazungu TUTAISHINDA!
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa mwili wa marehemu unaagwa nyumbani kwake halafu utapelekwa Green Acres Secondary ambako alikuwa Mkuu wa Shule kwa ajili ya wanafunzi na wengi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuanza safari ya kahama....

  omarilyas
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  R.I.P. Comrade, tangulia kamanda na wapiganaji wote wanakuombea makao mema huko uendako, Amen!
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  R.I.P brother
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  RIP Mwalimu Mkili.
  Tutamis sana harakati zako, hasa uliposimama kidete kutetea ongezeko la boom pale USDM ukishirikiana na Emil Kivugo, Zitto Kabwe na wengine wote waliojali maslahi ya wana-UDSM.
  Tutamis sana mchango wako. Nakumbuka sana ulivyosalitiwa na John Kusaja pale DARUSO na yaliyokufika baada ya hapo!

  Mungu akuweke pema!
   
 7. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  R I P Mkili Gervas.

  Utakumbukwa kwa mengi sana uliyoifanyia nchi yako Tanzania.
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  R.I.P Mkili Gervas. Nisaidieni jina la mke wake maana nachanganyikiwa kama ni yule ninayemfahamu au laa!!
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  what? kweli Mungu anachagua watu wazuri, huku wabaya wakiacha waendelee duniani.
   
 10. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wewe maane unataka jina la mke wa marehemu la nini? Kwa nini usiulizie watoto ambao ndo watahitaji msaada zaidi?
   
 11. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duh mzee R.I.P man!namkumbuka John Kusaja alimuachiaga mzigo huyu jamaa,kipindi cha mgomo wa boom,duh alipata shida sana na dola ikiwa ni kusimamishwa masomo etc,but aliprove yeye ni kamanda,hata green acres pako vizuri kwani walikuwa na kamanda kweli!
   
 12. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  alikuwa kiongozi wetu mahiri sana wakati wa chuo...alisota mahabusu sana na mwenzio Dr. Deo kwa kupigania haki zetu....poleni sana wafiwa!!!
   
 13. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omarilyas, Poleni na huo msiba, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Omarilyas, asante kwa taarifa, R.I.P, Mkuu Mkilli, Gervas. Ee Mungu Mkuu mweza wa yote mweke mahali pema Ndugu yetu Gervas Mkilli. Lakini tunakuomba baba, Mungu mwenyezi ulijawa huruma, utuondolee hawa mafisadi na wezi wa mali yetu uliyotujalia, Amen.
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jamani poleni wafiwa wote na watanzania wote kwa ujumla, hasa wale tuliokuwa tunatimuliwa pale UDSM kwa sababu ya kudai haki, tukiongozwa na Mkilli. Mungu tunakuomba umwadhibu John Kusaja kwa usaliti alioufanya.
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  Sep 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ndo huyohuyo unaemjua wewe...kama uamini nenda nyumbani kwake kaulize ...."jina la mke wa marehem Mkili ni nani..? "
  RIP Mkili.
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  R.I.P Brother you will surely be missed.
   
 18. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Magezi rafiki, leo umegeuka kuwa shehe wa jino kwa jino?

  Mathayo 5:43-44

  43. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
  44. lakini mimi (YESU) nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

  =========================

  Poleni sana wafiwa (hasa mke wake mpenzi) na faraja ya MUNGU wa mbinguni iwe juu yenu. Na sisi tulio tungali hai MUNGU atusadie kuzichunguza njia zetu kujua kama zinampendeza au la.
   
 19. O

  Omumura JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  R.I.P Gervas Mkili, poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wote!
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Namkumbuka sana Mzee Mkili tulipokuwa Mazengo (PCB), tulikuwa tuna-study pamoja huku tukigeuza bafu kama sehemu ya kujisomea huku walimu wakituzuga tu. Pamoja na kusomea bafuni tuliweza kufaulu vizuri kuingia Mlimani.

  Hili ni pigo kubwa kwa familia pamoja na kwa wapiganaji.
  Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...