Kamanda Sirro: Tutamfungulia Zitto kesi ya uchochezi

Kamanda Sirro: Tutamfungulia Zitto kesi ya uchochezi

Hahahah na Zitto akiwashinda aombe fidia ya kupotezewa muda
Hivi hawa wabunge Wa upinzani wanahangaika nini? Si walishapewa kula wale nchi isonge mbele. Wenzao Wa CCM wana kula kwa raha zao Na wananchi wanawapa kura. Yuko wapi mtetezi Kafulila? Ushauri wangu kuleni tulieni acheni maneno. Mtakuja Pauka kama Mrema.
 


Kamanda wa polisi wa jiji la Dar Simon Sirro amesema sasa hivi wanaendelea na upelezi wa makosa ya kichochezi aliyoyafanya Zitto Kabwe na upelelezi utakapokamilika watampeleka mahakamani.
Amesema hawatawavumilia watu kufanya uchochezi kwa sababu ya siasa kwa kuwa bila utulivu hakuna siasa








Hili ni moja ya tamko lililokosa weledi na linalodhihirisha namna jeshi letu la police lilivyokubali kwa hiari( limetii bila shuruti) kuwa tawi la chama cha mwendokasi(ccm),kinachoitwa uchochezi ni ukweli mchungu ambao viongozi wetu hawataki kuambiwa.Nini tafsiri ya uchochezi kwa jeshi la police?Ni ukweli usiohitajika kusemwa au ni kuruhusu watawala kujigeuza miungu isiyohojiwa?

Vipi kuhusu ile kauli ya mkubwa kwamba kuna meli ziliingia nchini zikiwa zimesheheni mizigo na zilipakuwa shehena na kuondoka bila kulipia ushuru,haikuwa ya kichochezi iliyolenga kuvichonganisha vyombo vyetu vya ulinzi vionekane vinaihujumu serikali yatu?Kauli ya kuwaambia baadhi ya wananchi kuwa wanaishi kama malaika na kutamka watashushwa ili waishi kama mashetani yenyewe si uchochezi unaolenga kuleta msuguano wa kijamii kwa watu masikini kuwachukia matajiri?

Kutamka hadharani tena bila ushahidi kuwa wafanyakazi wa TANESCO wanafungulia Maji toka kwenye mabwawa ya kuzalisha Umeme ili kulihujumu Taifa haikuwa ya kichochezi?

Kuwaambia waendesha mashtaka wetu kuwa walizembea katika kesi ya Samaki wa Magufuli na kusababisha serikali ishindwe kesi haikuwa ya kichochezi dhidi ya wataalamu wetu wa sheria?

Alipowaagiza majaji wahakikishe serikali inadhinda kesi zote za ukwepaji kodi ili serikali ipate mapato haikuwa kauri ya kichochezi inayojaribu kuuzima Uhuru wa mhimili wa mahakama?

Kuwaita wapinzani kuwa ni ma.lo.fa na wa.pu.mba.vu,na kuwaita watoto wa masikini waliokosa fursa ya kupata Elimu bora kuwa ni V.L.A.Z.A si uchochezi wa kiwango cha PhD?

Taifa letu kwa makusudi linalazimishwa kufikishwa katika nukta ya Mwisho ya uvumilivu wa kisiasa,badala ya kujenga siasa za maridhiano,serikali inaamua kutumia dola kuzima mawazo kinzani.Hili halikubariki na kamwe hatutakubali kuona wapiganaji wetu makini wananyanyasika eti kwa sababu hawapo upande wa serikali na wamekataa kuitikia pambio za sifa zinazoisifu serikali.

Taifa hili si la Magufuli,hii ni nchi yetu sote,si sahihi huikabidhi nchi mikononi mwa mtu mmoja na kumfanya kuwa Mwenye mamlaka ya Mwisho.Taifa huongozwa kwa maridhiano,hatuwezi kuliongoza Taifa kihisia na visasi halafu tukabaki salama.Wanaonyanyaswa na kunyimwa fursa ya kutoa mawazo yao ni viongozi wa watu,ni wawakilishi wa watu,wana kundi kubwa lililopo nyuma yao,tuliwaamini na kuwayuma watusemee,kuwapuuza wao ni kuupuuza Umma wa Watanzania uliowatuma,hili ni jambo la kichochezi zaidi kuliko uchochezi wenyewe.Hatuwezi kukubali upumbav.u wa kiwango hiki cha mwendokasi.
 
Hapo sasa!Mbona sasa hivi kuna utulivu na hakuna siasa?

Tena wakati huu Tanzania inasifiwa kuwa ni nchi ya amani na utulivu; yaani kisiwa cha amani.

Swali ni je, zaidi ya wakati huu wa utulivu hizo siasa zisubiri wakati gani kufanywa na wanasiasa aina ya akina Zitto et al...?
 
Zitto alifanya upotoshaji mkubwa kwenye swala la kodi za miamala ya pesa kwenye simu na ATM, anatakiwa ajifunze kucriticize bila kupotosha.

Kwani liko vipi hio kodi
 
And we (ACT) are going to be victorious on that case

Hahaha na msisahau kuongeza madiwani kutoka 10 nchi nzima atleast wafike 50 Mkuu na wabunge atleast 5 tu tosha kabisaa
 
Walipaswa kumkamata kwanza anyee debe ndipo wamfungulie mashtaka
 
Ndugu yangu Zitto kamwe hutoweza kupambana na serikali!
Mandela aliweza kuwashinda makaburu, pamoja na kumfunga jela miaka 27. Serikali hata iwe na nguvu kiasi gani haiwezi kupambana na nguvu ya UMMA. Huyu Magufuli wako ana nguvu kuliko alizokuwa nazo Marehemu Ghadafi?
 
Walipaswa kumkamata kwanza anyee debe ndipo wamfungulie mashtaka
Kwani Jela ziliwekwa kwa ajili ya wanyama? Nani anakudanganya kuwa mpigania haki anaogopa jela?
Nyie vijana waoga waoga ndio mnaogopa!
 
Zitto alisema Kagame ni Dikteta sasa watampeleka akajibu huko Rwanda kwa mjibu wa sheria ya Rwanda udikteta wa Kagame.

Ni pale Kagame atakapo Request prosecution dhidi ya Zitto ndo zitto aka prove huko Rwanda kwenye mahakama ya Rwanda.

Yawezekana alibambikiwa maneno ya kumuita Kagame dikteta, sasa ngoja watafute audio za ushahidi ili akatae hakusema alibabikiwa.

Vitisho vya kizee kwelikweli.
 
Mandela aliweza kuwashinda makaburu, pamoja na kumfunga jela miaka 27. Serikali hata iwe na nguvu kiasi gani haiwezi kupambana na nguvu ya UMMA. Huyu Magufuli wako ana nguvu kuliko alizokuwa nazo Marehemu Ghadafi?
Sasa wewe kwa akili yako unadhani makosa ya Zitto yanaweza kuamsha nguvu ya umma? Watanzania sasa wamebadilika. Si wa kupelekwshwa na kutumiwa tu kama mipira ya kiume
 
Kwani Jela ziliwekwa kwa ajili ya wanyama? Nani anakudanganya kuwa mpigania haki anaogopa jela?
Nyie vijana waoga waoga ndio mnaogopa!
Hahahahahaaaaa! Kwa hiyo siku hizi mmeungana na Zitto ama siyo?
 
Hahahahahaaaaa! Kwa hiyo siku hizi mmeungana na Zitto ama siyo?
Mimi binafsi naungana naye, hata wewe unakaribishwa, jambo analolifanya Zitto lina maslahi kwa taifa kwahiyo lazima tumuunge mkono kwa kuwa tuna mapenzi mema na Taifa letu.
 
Nyerere pia alishtakiwa Mahakamani na wakoloni kwa kesi ya uchochezi.

Kwahiyo watu wote wenye akili timamu tunajuwa tafsiri ya neno mchochezi ni nini!!
 
Back
Top Bottom