Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Mmoja wa makamanda wa juu kabisa wa kikundi cha ugaidi cha Boko Haram aitwae Amir Adamu Rugu Rugu amejisalimisha siku ya Alhamisi jioni kwa majeshi ya Nigeria.
Rugu Rugu alijisalimisha akiwa na wake zake watatu na watoto katika mji wa Gwoza ndani ya jimbo la Bono ambako ndipo vikosi vya jeshi la Nigeria vyaendesha operesheni iitwayo Hadin Kai.
Kamanda huyo ambae anasifika kwa ukatili na mauaji ya wananchi kadhaa katika maeneo ya milima ya Mandara na msitu mnene wa Sambisa aliamua kujitokeza baada ya mashambulizi ya anga na ardhini ya majeshi ya Nigeria.
Katika operesheni hiyo ya Hadin Kai majeshi ya Nigeria yalikazania kushambulia sehemu ya kaskazini ilipo misitu hiyo ya Sambisa na milima ya Mandara mfululizo.
Mpaka sasa magaidi wa Boko Haram wapatao 1000 na familia zao wamejisalimisha, 51 wamekamatwa na wananchi wapatao 29 wameokolewa na majeshi hayo.
Katika operesheni hiyo pia idadi ya majambazi 13 wakiwemo waporaji wa kutumia silaha pamoja na magaidi wamekamatwa.
Operesheni hiyo inahusisha majeshi ya Nigeria na vikosi mbalimbali vya usalama.
Chanzo:
Vyombo mbalimbali vya habari vya Nigeria likiwemo jarida la Vangard.