Maelfu ya wanamgambo wa Boko Haram wajisalimisha Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

Jeshi la Nigeria linasema karibu wanamgambo 6000 wa Boko Haram wakiwemo makamanda , wapiganaji na familia zao wamejisalimisha kwa mamlaka katika muda wa wiki chache zilizopita.

Cameroon pia ilikuwa imetangaza kujisalimisha kwa mamia ya ya wanamgambo Boko Haram nchini humo hivi karibuni.

Jeshi la Nigeria linasema kujisalimishwa kwa wingi kwa wanachama wa Boko Haram kunatokana oparesheni kali ya kijeshi inayoendesha dhidi ya wanamgambo hao kaskazini mashariki mwa nchi.

Kifo cha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau mwezi Mei huenda kumechangia hali hiyo.

Baadhi ya wafuasi hao huenda wamejisalimisha kwa mamlaka au walijiunga kundi pinzani la wapiganaji- Islamic State Afrika Magharibi, ISWAP.

Mamlaka nchini Nigeria zinasema sasa wanatoa wasifu kwa wale ambao wamejisalimisha kwa lengo la kuwapa ushauri nasaha.

Lakini Wanigeria wengine wana wasiwasi juu ya kuwaunganisha tena wapiganaji wa zamani katika jamii- wakitaja hatari zinazoweza kutokea.

Kulingana na Umoja wa Mataifa uvamizi wa Boko Haram ulianza 2009 -umesababisha vifo vya watu 300,000 na mamilioni ya wengine kuachwa bila makao Nigeria na nchi nyingine kadhaa katika eneo la Ziwa Chad.

1630679821062.gif
 
Kuna dalili la kundi hili la boko haram kuparaganyika baada ya tetesi kuwa kiongozi wao mkuu Abubakar Shekai kufariki na kuripotiwa wapiganaji wake wapatao 6000 kujisalimisha kwa kwa serikali ya Nigeria na nchini Cameron ikiripotiwa mamia ya wapiganaji wa Boko Haram kujisalimisha.
Screenshot_20210904-100612_Chrome.jpg
BOKO-HARAM.jpg
 
Kuna dalili la kundi hili la boko haram kuparaganyika baada ya tetesi kuwa kiongozi wao mkuu Abubakar Shekai kufariki na kuripotiwa wapiganaji wake wapatao 6000 kujisalimisha kwa kwa serikali ya Nigeria na nchini Cameron ikiripotiwa mamia ya wapiganaji wa Boko Haram kujisalimisha.View attachment 1923195View attachment 1923198
Hawa watu ni wa ovyo sana,wameua watu wengi sana,wamebaka,wameporwa mali n.k. kwa kutumia dini,eti sasa wanajisalimisha!

Wanyongwe tu au kufungwa maisha maana hawana tofauti na shetani ibilisi
 
Hawa watu kujisalimisha ni labda kwa sababu wana agenda yao maalum au hii ni dalili tosha kwamba dunia inakaribia mwisho.
We better brace for impact.
Mkuu kwa hapo uliposema huwenda wana ajenda yao, nikweli ndio maana wanigeria wengi wana wasiwasi na tukio hili kwa kudhani kuwa inaweza ikawa ni mbinu ya hujuma zidi ya jeshi.
 
Back
Top Bottom