Kamanda Mpinga tunaomba ufafanuzi

Kamanda Mpinga tunaomba ufafanuzi

Nashindwa kuattach picha hapa, wengi tunachanganya kati ya Spot Lights na Fog Lights.

Fog Lights zipo kwenye magari mengi tu, na si kitu unaweza ng'oa kwa urahisi. Ni vile vitaa vidogo vinakaa chini kabisa ya show ya mbele ya gari.
 
Attachments

  • Screenshot_2017-01-20-16-58-54.jpg
    Screenshot_2017-01-20-16-58-54.jpg
    34 KB · Views: 30
  • Thanks
Reactions: bdo
Hivi uwa kuna spotlights na sport lights eh?

Mkuu;
Si neno la kiswahili chetu hivyo kila mtu huijua atakavyo. Wapo wanaosema tu na mwenye kuuza anaijua hivyo anamletea. Mbona wengine wanasema; Jamaa kanideep nikampigia, wewe unamwelewaje? Kuwa ni mtu alim beep au ali m deep? Mengi tunaenda nayo vivyo hivyo. Wengine wanasema site mirror, side mirror, sight mirror. Tunaenda nao hivyo hivyo bora tunamuelewa
 
GARI NYINGINE ZINA HIZO TAA TOKA ILIPOTOKA HUKO UGHAIBUNI. NA UTAGUNDUA USIKU USIPIZOWASHA MWANGA UNAKUWA MDOGO SANA KWA KUONA MBELE. UKWELI SIO MWANGA KAMA WA HIZO WALIZOUNGANISHA HAPA NCHINI. JE NI SAWA KUUTOZA FAINI? NADHANI MATRAFIKI WAANGALIE KWANZA KAMA TAA NI ZA KUUNGANISHWA HAPA NI KAMA HILI SWALA LA NGAO ZA KWENYE MAGARI

Kweli kabisa mkuu ila tatizo ni hawa watoto wa Mpinga, hawana nafasi ya kuja kuchungulia aina ya taa. Haswa wakiwa tiyari weshaishika leseni yako mkononi mwao. Watakuchefua mno ukiangalia safari yako ilivyo ya muhimu na wanakupotezea muda bure. Tumuombe Kamanda awaambie wabadilike waache kujifanya kuwa neno lao ndio mwisho
 
Hilo ndiyo kosa kubwa madereva wengi hufanya, inakuaje unakurupuka kutoa leseni wakati Traffic Act inaruhusu kabisa kuwasilisha leseni hiyo ndani ya saa 24, ndiyo maana wanawageuza watakavyo hata kama huna kosa.
 
Mawazo yako mazuuri sana lakini sijui ka weye umewahi kusafiri siku za karibuni na gari yako. Kama ni kweli basi safari yako haikuwa ya haraka wala ulazima uendako.
Jaribu fikiri; Akusimamishe, akuweke pale, usote pale kwa muda wa zaidi ya saa nzima, huku leseni unayo mfukoni. Sijui, labda mimi nina kasoro kichwani kwani kitendo cha kusimamishwa pale na kijana mtoto tu naonaga ngumu kumesa.
Huwa natamani niondoke kwa nguvu nione watanifanya nini ila najirudi.
 
Unang'oa vipi taa za kiwandani..
Haiingi akilini..
Sheria ni sheria.
Na standard za taa za magari ni za kimataifa.
Huwezi ng'oa taa za "manufacturers standard specifications" unatoa za ziada na urembo tu
 
Mkuu;
Mawazo yako mazuuri sana lakini sijui ka weye umewahi kusafiri siku za karibuni na gari yako. Kama ni kweli basi safari yako haikuwa ya haraka wala ulazima uendako.
Jaribu fikiri; Akusimamishe, akuweke pale, usote pale kwa muda wa zaidi ya saa nzima, huku leseni unayo mfukoni. Sijui, labda mimi nina kasoro kichwani kwani kitendo cha kusimamishwa pale na kijana mtoto tu naonaga ngumu kumesa.
Huwa natamani niondoke kwa nguvu nione watanifanya nini ila najirudi.
Siku utakapoijua haki yako ndipo utakapojua kudeal na hao unaoita vijana wadogo.
Wengi nimewasaidia kupata japo nakala ya traffic act imewasaidia.
Endelea kuchangia serikali hata kwa kosa ambalo silo la kuchangia serikali.
 
Siku utakapoijua gaki yako ndipo utakajua jua kudeal na hao unaoita vijana wadogo.
Wengi nimewasaidia kupata japo nakala ya traffic act imewasaidia.
Endelea kuchangia serikali hata kwa kosa ambalo silo la kuchangia serikali.

Please naihitaji hiyo act na mm
 
Back
Top Bottom