shinyangakwetu
JF-Expert Member
- Jun 25, 2015
- 2,487
- 2,394
Mtakumbuka kuwa kamanda ulitangaza taa zote za ziada za mwanga mkali ziondolewe ktk magari haraka sana,sasa Jana nimepita na ka rav4 kangu kana taa(spotlight) ambazo Zimekuja na gari toka japani,taa hizi siitumii maana wajuvi wa masuala ya magari wanasema zinatumika wakati wa ukungu,na pia kwa sasa haziwaki.sasa hawa vijana wako kamanda wamemkamata na kusema hizo ni mojawapo wa taa ulizoagiza zitolewe na wameniandikia faini elfu 30,mpaka sasa sijalipa kwani kwa uelewa wangu hizi taarifa hazihusiani na zile alizolenga kamanda mpinga.kamanda kama unapita humu au kama kuna mwenye kuweza kutoa ufafanuzi naomba na pia nashauri kabla ya kukamata na kupiga faini elimu itolewe kwa SS wenye magari na pia Askari waelimishwe ni nini hasa cha kufanya maana umekuwa kero sana.