Kamanda mkuu wa Ukraine akasirishwa na ahadi hewa za NATO huku askari wake wakiangamia

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,192
10,926
Kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine generali Valery Zaluzhny amesema nchi yake ina makubaliano maalum na Pentagon na kwamba wana mawasiliano ya masaa 24 juu ya namna vita vinavyoendelea,hata hivyo amekasirishwa sana na ahadi hewa za Marekani na washirika wa NATO.

kilichomkera zaidi na kutoa matusi kwa Pentagon ni kutokana na lawama kwamba mapigano ya kukomboa maeneo hayaendi vizuri kama yalivyotegemewa. Huku Akifoka Zaluzhyn akasema “p----d me off”.

Akaongeza kwa kurudia maneno ya raisi wake kwamba vita hivyo si mchezo na kwamba kila mita inayokombolewa basi ni kwa kumwagika damu nyingi sana..Mimi sitaki ndege 120 bali ni ndege chache tu za F16.

kama hatukupata risasi 100,000 za kuingiza kwenye mizinga basi watu 1000 watakufa.Akamalizia kwa kusema jeshi lake halina uwezo kabisa wa kupigana na nguvu kubwa ya jeshi la Urusi kutoka angani.

1688197101035.png
 
Wale nato WA Buza watapita Kimyakimya
Hali kwa NATO ni tete sana. Namkumbuka mbabe mmoja wa kimya kimya mtaani kwetu.Siku moja aligombana na kijana mmoja mpiga debe machachari.Kijana akaamua kumpiga yule mbabe mzee.Nililoliona mpaka leo limebaki akilini mwangu. Kijana alianza kwa ngumi za nguvu zote zikatolewa nje.Akakasirika na kutumia kitu cha ncha kali akanyang'anywa bila kudhuriwa.Akaenda kuokota mawe akarusha kutoka mbali yote yakakwepwa akarudi tena mwilini akapewa ngumi moja nzito akadondoka chini.Yule mbabe hata hakuhema yuko pale pale.
 
Kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine generali Valery Zaluzhny amesema nchi yake ina makubaliano maalum na Pentagon na kwamba wana mawasiliano ya masaa 24 juu ya namna vita vinavyoendelea,hata hivyo amekasirishwa sana na ahadi hewa za Marekani na washirika wa NATO.

kilichomkera zaidi na kutoa matusi kwa Pentagon ni kutokana na lawama kwamba mapigano ya kukomboa maeneo hayaendi vizuri kama yalivyotegemewa. Huku Akifoka Zaluzhyn akasema “p----d me off”.

Akaongeza kwa kurudia maneno ya raisi wake kwamba vita hivyo si mchezo na kwamba kila mita inayokombolewa basi ni kwa kumwagika damu nyingi sana..Mimi sitaki ndege 120 bali ni ndege chache tu za F16.

kama hatukupata risasi 100,000 za kuingiza kwenye mizinga basi watu 1000 watakufa.Akamalizia kwa kusema jeshi lake halina uwezo kabisa wa kupigana na nguvu kubwa ya jeshi la Urusi kutoka angani.

View attachment 2674860
Huyu anaenda kufia vitani.. ..
 
Back
Top Bottom