Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Mel. Alphonce mawazo umeuwawa kinyama, inaumiza sana. Jamani hata Kama tuna tofautiana itikikadi tusifikie hatua ya "Kutoana Uhai" wewe uliyebeba Panga, shoka na silaha yoyote ile "Embu kabla ya tukio hili ungetafaka Watoto wa Mawazo, Mke, wazazi na ndugu wanamtegemea"
Kisasi ni kazi ya Ibilisi, fanyeni siasa za Hoja kwa Hoja na si kuana.
Poleni sana Wa TZ wenzangu. This is bad sign for our peace.
 
maneno ya kichochezi kama haya ktk uzi huu yapingwe. Kuanzia ya Lema na wachangiaji wengine, kila aandikaye "anadhani" waliotenda hivyo ni akina fulani pasipo chembe ya uhakika...... MTACHIMBA SHIMO NA MTATUMBUKIA WENYEWE

Ungekuwa na hekima kama ungewambia ccm waache siasa za chuki.
 
Waliofanya tuko hili wakamatwe Mara moja na sheria ichukue mkondo wake,
Kwani hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mwenzake.

Police fanyeni kazi yenu kwa weredi wenu na kwa kutumia intelijensia yenu kuwanasa wote waliohusika na tukio hilo.
Ili kuondoa mtazamo hasi juu ya jeshi letu lenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao.
Siasa hizi za mauaji zikomeshwe Mara moja kuendelea kuzifumbua macho ni kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko.
Wananchi wote tuwe watulivu wakati jeshi la police likifanya kazi yake.

Polisi wa nchi gani watakaopoteza muda kutafuta wauaji wa Alphonce Mawazo!??

Nchi imejaa wasanii,wanahadaa ulimwengu kuwa ni nchi ya amani na utulivu....madaraka yamewafikisha kutothamini uhai wa binadamu wenzao!! Si ajabu mauaji haya nyuma yke kuna mtu anaepita maeneo mbali mbali na kwenye vyombo vya habari akikemea uhalifu!!!!

Mungu kama uishivyo,ni wakati sasa wa kushusha adhabu dhidi ya hawa wadhalimu,Mungu tumekosea nini,kaka Mawazo kakosea wapi Mungu?

Ni kweli kosa hilo kama lipo adhabu yake ni KIFO! tena cha mapanga na mashoka? Mungu uliewaokoa Paulo na Sila, machozi haya ya watanzania wanaoonewa,wanaodhalilishwa na kuuliwa ndugu zao bila sababu yasipotee bure Jehova!

Shusha adhabu kali Mungu,tumechoka sasa,tumechoka sasa,tumechoka Jehova Yire,kama kuwa CD,ACT,CUF,NCCR na vyama vingine vya upinzani ni dhambi Mungu,basi tunakuomba ukvifutilie mbali vyama hivyo na kibaki chama kitakatifu Mungu! Bali kama si dhambi,Mungu ni wakati sasa wa kujitukuza,tenda maajabu Mungu.

Hapa tunahitaji utetezi wako Mungu,waumbue wanafiki wote wanaopita kuhadaa umma kwa maneno ya amani huku wakipanga mauaji Jehova. Mungu tutee wewe,nchi haina amani tena ni uwongo na hadaa kubwa kusema amani imejaa,huu utulivu uliopo isichukuliwe kuwa amani. Mungu wetu tutee wewe.
 
Tunahitaji viongozi wa kisiasa wenye uwezo wa kujenga hoja na sio wenye kuijaza chuki jamii...!

Wako baadhi ya wenye dhamana ya ulinzi wa jamii wakishirikiana na wanasiasa au wafanyabiashara wa madini wanaendesha mauaji ya kikatili dhidi ya jamii mfano albino.

Hili ni tatizo msingi linalotakiwa kushughulikiwa.Nilidhani Lema unaliongelea hili.

Maoni yangu ni kuwa na utulivu na uvumilivu wa hali ya juu kama kiongozi kwani ubaya hulipwa kwa wema zaidi...!!!

Anayeuwa Albino ni Msukuma nenda kamkamate mbona liko wazi.
 
uncleben_ na Tariq boy hiyo mada yenu kwa mustakabali wa ukombozi wa nchi yetu ni kama vile kuulizana kati ya Yai na Kuku kimeanza nini? Kuvumilia hadi lini? au tupigane dhidi ya nani na faida yake ni nin? lakini ni lazima tutafute ufumbuzi wa hili jambo!

Mkuu uvumbuzi umeshindikana kwa njia ya kidemokrasia ,na siku zote mwanadamu anapobanwa kwa njia moja hutafuta nyingine ,binafsi sipendi tumwage damu za watanzania ila hao pia wanouwawa ni watanzania na tufike mahali tuseme sasa basi
 
Kwa vyote iwavyo...kifo kinauma kwa kila mtu..hapa tusije na mihemuko ya kisiasa...


R I P mawazo..! Mungu akupe pumziko la milele
 
Lema, i think kwa hili umewahi sana kutoa tamko.... Bado hujawa mbunge and anything can be done to stop you contesting

jaribu kubana pumzi kidogo tu ili upate nguvu zaidi ya kusukuma gurudumu

Hakuna kinachoweza kuzuwia wananchi ndyo wenye maamuzi ya mwisho.
 
Ni masikitiko sana kupoteza binadamu ambaye nchi bado inahitaji mchango wake.

Mungu akuweke pema peponi Kamanda Mawazo.

Nashangaa umeanza kutoa tuhuma mapema kabla hata ya uchunguzi haujafanyika. Nadhani Mtu ambaye aliwahi kuwa Mbunge atakuwa anafahamu maana ya sheria.


Na wewe Lema ni kati ya wanasiasa wanaosaidia wauwaji wasifahamike na waendelee kuwepo mitaani!

Kama mmoja wa viongozi wa CHADEMA walivyoueleza ulimwengu, kwa sasa una mkanda ambao unaonyesha watu waliofanya mauwaji katika mkutano Arusha kwenye viwanja vya Soweto! Kinachoshangaza na kusikitisha ni kuendelea kukaa na mkanda wa video badala ya kuvipa vyombo vya habari ili vihabarishe dunia kuhusu wauwaji hao kwa sababu kuna uwezekano wanaendelea kufanya maovu wakati una mkanda unaonyesha sura zao.

Inaeleweka Vyombo vya habari ni muhimili mwingine wa nchi na taasisi zake zinafanya kazi kubwa ya kuelimisha na kupasha habari. Nchi kama Uingereza wananchi wanatumia vyombo vya habari kama BBC kuhabarisha jamii kuhusu watenda maovu walionaswa kwenye video (Crimewatch).

Kama hamuwezi kuwapa polisi/serikali huo mkanda, vipeni vyombo vya habari ili viwafichue watenda maovu.

Kuna familia mpaka sasa hazifahamu kilichotokea mpaka kupotelewa na ndugu, jamaa na marafiki. Kwa familia hizi kufahamu nani aliyetenda maovu ni njia ya kuponya makovu ya masikitiko.

Maisha ya binadamu ni zaidi ya siasa. Hata kuwafahamu kwa sura wauwaji ni moja ya justice kwa familia. Wapeni haki ndugu, jamaa na marafiki.

Sheria zipi wakati polisi wamekuwa wakikaji wa sheria. Tafakali kama uko ccm endelea huko huko maana police wataheshimu chama chako si haki yako.
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.

Hata kama alitenda uhalifu,iko wapi sheria inayohusu kuua?ukiachilia mbali siasa huyu ni baba wa watoto,watoto hawa leo wanabaki yatima bila baba,nani atagharamia elimu yao?maisha yao yatakuwaje bila baba?huyu kaacha mke,baba,kaka na dada zake,wajomba nk,kisa ni ujinga na uwendawazimu wa mtu mmoja au genge la wahuni wachache,hata kama alikuwa na makosa,kila anaekosa ni lazima kuuawa?Napata wasiwasi sana na watu wa kanda ya ziwa,mauaji ya albino,vikongwe nk na sasa siasa za namna hii,tuamke watanzania.
 
Siyo lazima kuamini kitu kisichokusaidia, kamwe uwezi kulazimisha ukubalike uovu unaofanywa na sisiemu sasa umepitiliza, duniani hakuna amani, amani iko kwa mmoja naye bi mungu,
 
Hivi Godbless Lema unapokuwa unaandika huwa unakuwa umelewa, umevuta bangi au huwa unakuwa ndotoni?

Mlipomuua Chacha Wangwe mlisingizia Ccm na Polisi. Leo mmemuua Mawazo unakurupuka tena na kulihusisha Jeshi la Polisi. Cha kushangaza hutoi sababu za kwanini polisi wanahusika zaidi kupiga porojo.

Ni polisi hawa hawa ambao mnawadhihaki kila kukicha na ambao wamewalinda kwenye mikutano yenu yote ya kampeni lakini leo mnawazushia uongo wa wazi kabisa.

Hivi kifo cha Mawazo kina uhusiano gani na kununuliwa kwa magari ya Polisi? Au unataka kutuaminisha kuwa magari hayo ndio yaliyomuua?

Lema mkeo ni mtu makini sana na ana busara na hekima ya hali ya juu hebu uwe unamuomba ushauri wakati fulani kabla hujaandika mambo haya. Kwake naamini ni fedheha kubwa sana. Badilika kaka.

Lema kuilaumu polisi ni sawa . Highness na Machemli walivyocharangwa mapanga mpaka leo hakuna aliyechukuliwa hatua, walioua Arumeru mpaka leo, Walioua Tarime mpaka leo, walioua Mwz mpaka leo, Waliopanga mauaji ya Tunduma mpaka leo, Waliocharanga wana CDM mashoka ( 2010)mbeya mpaka leo .etc

Na hata hili la Geita utaambiwa wauaji hawajulikani na ndio msimamo wa polisi mpaka sasa. Lakini inapotokea kinyume chake wanaonyesha ( polisi)misuli yake mapema sana

Katika uchaguzi huu uliopita matukio ni ya kuuawa wana CDM na si vinginevyo hivyo unapofanya ushabiki uangalie na reality .
 
Nina kila sababu ya kuamini kuwa waliotekeleza tukio hili ni CHADEMA wenyewe. Kwanza wanasema kuwa Alphonce alikuwa na mkutano wa ndani kata ya Katele kuwaapisha mawakala. Wakiwa kwenye mkutano, walipata taarifa kuwa mkutano wao ulikuwa unarekodiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wana CCM ambao walikuwa nje ya ukumbi huo. Walipotoka nje ndipo kundi la wana CCM walipowavamia na kuwajeruhi baadhi ya wafuasi wa CHADEMA. Cha kushangaza eti Alphonce Mawazo amekutwa umbali wa nusu kilometa kutoka eneo la mkutano na eti wenyewe wanashangaa aliondokaje kwenye eneo hilo na alivamiwa na watu eti asipate msaada wowote.

Lema naye anakuja na figisu zake eti wahusika si CCM bali ni polisi. Cha kushangaza kwenye andiko hilo haelezi moja kwa moja jinsi polisi walivyohusika bali anasema eti wanawakumbatia wahalifu. Huu ni uhuni wa hali ya juu sana
 
Ni mara chache sana nimesoma maandiko ya kikakamavu kama hili , asante kamanda lema kwa kunifuta machozi , mawazo ameniumiza sana ! Lakini sitalia tena .
 
YATQKUWA KAMA YA MWandishi MWANGOSI NA DR ULIMBOKA CCM HOVYO KABISA LAZIMA NCHI INAHITAJI UKOMBOZI HUU NI UHUNI
CCM haina siasa chafu za mauaji. Inashinda kwenye ballot box
 
Back
Top Bottom