Kamanda Lowassa ndani ya Singida, Afanya mkutano Manyoni

Kamanda Lowassa ndani ya Singida, Afanya mkutano Manyoni

Upinzani upi wewe Manyoni majimbo yote ni ya CCM wala hakuna upinzani wa kusumbua. Manyoni magharibi Lupaa alikua ana nafasi ya kushinda kama angepitishwa Lwanji na kwa kweli mwaka 2010 alishinda ila walimchakachua na yeye pia aliuza ushindi ila mwaka huu mtu anayegombea naye hamuwezi hata kidogo.

Pili kwa taarifa yako huyo Lupaa ni mtu wa System nyie hamjui tu, mwaka 2010 kwa upande wa urais alikuwa anampigia kampeni Rais kikwete na ndo maana baada ya kushindwa ameteuliwa kama Katibu Tawala Wilaya (DAS-Mbulu) umeona wapi mtu akagombea kwa tiketi ya upinzani na akashindwa na kupewa cheo Serikalini?

Umepanic eeeee
 
Haya Sio Mapenzi tena, Ni mahaba!......


LOWASSA ndio Rais, hilo halihitaji mjadala tena! Sasa tuna uhakika 100% Kuwa mgombea wetu ndiye anakuwa mshindi!

Asanteni sana watanzania, kweli Takwimu haziongopi!!!

VIVA LOWASSA! VIVA UKAWA, VIVA TANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
lowasa uwe na huruma ccm wana mioyo ya nyama sio chuma,
wahurumie mzee
 
Wakuu samahani kwa kuchelewa kuwapa picha za Lowassa akiwa Singida Leo kwa hapa Jamii Forums ni kwa sababu nilipata matatizo ya kuibiwa simu mchana wa leo ila mwana wa lowassa nimerudi tena. Balaa la Lowassa linaendelea na Leo ni historia kwa mkoa wa Singida
asante sana mkuu .
 
Wakuu samahani kwa kuchelewa kuwapa picha za Lowassa akiwa Singida Leo kwa hapa Jamii Forums ni kwa sababu nilipata matatizo ya kuibiwa simu mchana wa leo ila mwana wa lowassa nimerudi tena. Balaa la Lowassa linaendelea na Leo ni historia kwa mkoa wa Singida
Asante kamanda ila uwe u.aweka na vidioz tunakuomba
 
European Union makao makuu yake Ni Brussels,Belgium sio Athens.
statement rasmi inayotolewa na European union inatolewa kutoka Brussels na European union commissioner au European union president au European union speaker au European union spokesperson
hii statement unaweza kuwa ya kufoji au maoni ya mtu binafsi.

Mwandishi na mtoa Statement hawafahamiki hata na Google, ndo ujue kweli magamba wamechanganyikiwa, wanashindwa ku update propaganda zao!
 





Wadau wa Singida wakitafuta namna ya kupata taswira ya Mgombea wao, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.

Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa mji wa Singida leo.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrance Masha akionyesha Ilani ya Chama chao kwa Maelfu ya wananchi wa mji wa Singida, waliofurika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.

Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.




Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.

Mabango yenye jumbe mbali mbali kwenye Mkutano huo.


Mkali wa Propaganda, Tambwe Hizza akisema yake kwenye Mkutano huo.





Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA wa Jimbo la Singida Mjini, Mgana Msindai "CRDB", katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.






























http://4.bp.blogspot.com/-7akzD4Kxc1A/VfRN1brABqI/AAAAAAAAByc/HLdWELwGSqo/s1600/OTH_1705.jpg











​














































































source: Mtaa kwa Mtaa Blog - Othman Michuzi
 
Back
Top Bottom