Kamanda Lema ndani ya Arumeru

Jaman yashafika huko; Nakumbuka wakati TENDWA amemshauri Lema kuomba msamaa watu tulimponda sana humu ndani; na kama haitoshi akaibuka bwana mmoja ambaye pia ni Kiongozi wa wameru pande zile na kusema hakuna Tamko lolote lililotoka labda ni mtu mmoja tu yeye kama yeye kaamua kufunguka na huo uzushi wake ila tu wazee hawakupenda kauli za Mh Lema alizozitoa wakat wa msiba wa Mh Sumari; sasa yamefikaje ya kuandaa PLATOON YA ULINZI hivi hamuoni kama tunaandaa mazingira ya kuraruana sime?

Haya yote ni matunda ya uchochezi wa Tendwa
 
Mungu atuepushe na vita kati ya morani dhidi FFU na Green guard hasa wakati wa kampeni za uchaguzi:lol:

Inatakiwa ifike mahali viongozi wa serikali kama Tendwa wachunge ndimi zao kabla ya kuropoka hovyo.Aulize kwa nini viongozi wa Kenya wapo the Haugue?
 
Kama Mh. Lema yupo kwenye hili jamvi TAFADHARI kwa roho safi tu kama kweli hiyo kauli ilitolewa na wazee kule Meru ningependa aweke kando uheshimiwa wake akawaombe Msamaha wazee wake na kwa kufanya hivyo wala hapungukiwi na lolote na wala haimgharimu chochote zaidi zaidi nadhani atakua anazidi kujieka juu KISIASA na kuonyesha ukomavu thabiti kuliko kujipanga kuyakabiri mashambulizi ambayo labda yataibuka wakati kuna uwezekano wa kuyacounter na tuwe na kampeni zisizo na vurugu"
 
Ila hawa polisi wana mambo mtu katishiwa kuuwawa wanasema hawawezi fuatilia mpaka Lema apeleke shauri khaa!
With my common sense mtu anapotishia kutaka kumuua public figure kama Lema polisi should be on the neck of the individual.
Naona kuna double standard apo!
 
CDM mnaipeleka wapi Arumeru? Kila mtu akiwa warlord kama Somalia, akawa na wanamgambo wake, na silaha zake, si uchaguzi utageuka chanzo cha vita vya wanamgambo?

Msituletee mambo yenu ya shari, lazima usalama ulindwe na Polisi....full stop!

Mshari ni nani hapo? Tendwa alishabikia maneno ya uaji badala ya kuchukua hatua na huyu Tendwa na jeshi la polisi ni kitu kimoja kwa hiyo kama hamna jeshi la polisi kwa nini watu wasiunde la kwao
 
Kamanda Lema ana Mungu ayempigania kamwe hao panya wadogo CCM na hao wazee hawawezi kumfanya chochote! Kama hao Polisi wao siku zote ni CCM hatuwaitaji ulinzi wao hata kidogo,mana sisi Chadema tuna Mungu anayetugiani wakati CCM wana Pesa na Polisi.
 
Msitake kutishia Watu nyie,wameru labda miaka ya zamani ndio walikuwa wanawababaisha wanakijiji wenzao,hawana lolote. Nyie ngojeni madume ya CCM yatue huko Kama hao morani went hawakushikishwa ukuta. Hi ndio tatizo la JF,Watu wana mkwara babu kubwa wakati hakuna lolote.
 
Mkuu hii ni Tanzania wanayoitaka iwe. By the way, kwa mtu aliyepewa dhamana na title ya u-jaji aropoke vile, unategemea watu wenye kuta 28 za elimu maishani mwao wafanye nini?
Shame on you Tendwa.

Mkuu, nakuunga mkono kwa mchango wako.
Nadhani pia polisi wetu badala ya kutumia intelijensia yao kama ambavyo wamezea kufanya,wangemwita Mhe. Tendwa awathibitishie kauli yake ya tishio la kuuawa Mhe. Lema na kuwataja pia, ili waliotoa kauli hiyo mbele yake nao pia wapate kuhojiwa.
Wanaposema mpaka mtu aende kulalamika kwao ndipo wafanye uchunguzi???!!! kwangu ninaona si hatua sahihi kwa jeshi linalotakiwa kufanya upelelezi kwa kila tishio inalosikia au kuambiwa.
Only in Tanzania!
 
Naanza kuona dalili kubwa sana za umwagikaji damu...Ee Mungu utuokoe na utusaidie hima...
 
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.

Hizi ndiyo siasa mnazopenda CCM hasa mkiishiwa ushawishi. Police hawana legitimacy kwenye hili, wangetaka kujenga uhalali wao wangemkamata Tendwa na kumwambia awataje wazee waliomwambia watamuua Lema, then operation ingeenda na kuwatia nguvuni wote waliotoa tishio la kuua. Hapo Lema na vijana wangekuwa hawana haja ya kujilinda kwani waliopewa dhamana hiyo kikatiba wanatekeleza wajibu wao.
 
Msitake kutishia Watu nyie,wameru labda miaka ya zamani ndio walikuwa wanawababaisha wanakijiji wenzao,hawana lolote. Nyie ngojeni madume ya CCM yatue huko Kama hao morani went hawakushikishwa ukuta. Hi ndio tatizo la JF,Watu wana mkwara babu kubwa wakati hakuna lolote.
Mwaka juzi ni zamani umesahau wale polisi wastaafu akiwemo Yohane walivyoongoza wananchi kuvamia mashamba, kama huamini tukutane kesho Kikatiti uwaone vijana toka Mbuguni wao huwa wanajiita nyoka. Hizi ndizo siasa CCM wanazozitaka.

images
 
Hizi ndiyo siasa mnazopenda CCM hasa mkiishiwa ushawishi. Police hawana legitimacy kwenye hili, wangetaka kujenga uhalali wao wangemkamata Tendwa na kumwambia awataje wazee waliomwambia watamuua Lema, then operation ingeenda na kuwatia nguvuni wote waliotoa tishio la kuua. Hapo Lema na vijana wangekuwa hawana haja ya kujilinda kwani waliopewa dhamana hiyo kikatiba wanatekeleza wajibu wao.

Ni kweli mkuu umenena vema
 
Mbona 300 ni wachache uki compare na green guard wa ccm, police, usalama wa ccm, tendwa et al? Wangefanya at least 1000 na kuendelea!!
 
Mbona 300 ni wachache uki compare na green guard wa ccm, police, usalama wa ccm, tendwa et al? Wangefanya at least 1000 na kuendelea!!

Wanatosha mkuu kwa sababu hawa watakuwa wanalinda kila mkutano na kuambatana na Lema kila atakapokuwa ili watu ambao Tendwa amesema watamuua wasifanikiwe lengo lao
 
CCM, ni mufilisi na mzee Tendwa naamini kauli zake anajutia, frankly CCM wawe wapole tu na wafuate taratibu zote za uchaguzi zaidi ya hapo yatakua mengine
 
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.

Ni kama vile haujui kuwa polisi wa Tanzania kazi yao kubwa ni kulinda serikali na viongozi wa Magamba? Polisi wa Tanzania wanachojua ni kuilinda CCM tu; hawaaminiki. Big up morani wa Kimeru maana Tanzania italindwa na watanzania wenyewe
 
Tusiitane shetani. Tanzania makabila ni mengi na majina au maneno yanaingiliana. Kikwetu NGOROMIKO maana yake ni KIONGOZI WA KIMILA.

Ok mkuu ila Kikwetu ni shetani! labda basi mila yenu yaongozwa na shetani sijui!! Kabila gani mshimiwa? lol!:shetani: naichukia hii kitu
 
Back
Top Bottom