Kamanda Lema ndani ya Arumeru

Nashangaa mmeshindwa hata kuwa vua magamba.....

Kaka achana na hawo magamba nape lazima akamsaidie gamba kumpigia mkwe wa magamba kampeni Lema alikuwa sokoni one kufungua shina sasa alikuwa anaelekea Arumeru kufungua matawi matano alikuwa na mbunge anaye subiria kuapishwa Nassari
 
Tendwa sasa auza jimbo la Aremeru Mashariki bei chee kwa CHADEMA kutokana na uzushi wake wa karne kisiasa kuwasingizia wazee wetu wale wa ukoo (washili) madai mazito ya kupanga kumuua mtoto wao wenyewe, Kamanda Lema.
 
Wakuu muda si mrefu nimemuona mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema maeneo ya Kikatiti. Alikua ndani ya gari na alisimama ili kusalimia watu ambao walianza kulizunguka gari lake kumsalimia baada ya kumtambua.
Hakukaa sana eneo hili kwani mara baada ya kusalimiana na raia alishika barabara ya kuelekea Maroroni.
Haya sasa wale wazeee wa kimeru waliosema watamfanya vibaya, Lema huyooo Arumeru!

Wana JF hasa wale wapenzi wa CDM,
Ile maneno alizungumza John Tendwa a.k.a Msajili wa Vyama ilikuwa ni PROPAGANDA ZA CCM tu hakuna kingine hapo. Kwa Great Thinkers tumeligundua hilo. John Tendwa anatumiwa na CCM ili kutaka kuvuruga Kambi ya upinzani.

Kama nji hii ingelikuwa na UTAWALA WA SHERIA basi John Tendwa alitakiwa sasa hivi apandishwe kizimbani na ashtakiwe kwa habari za UCHOCHEZI ambazo zaweza kuhatarisha Amani kwenye eneo la Uchaguzi jimbo la Arumeru East.
Bado tutasikia mengi sana. Bado NEC hawajaanza manjonjo yao. Naona this time vituko vitakuwa maradufu ya vile vya Igunga RA.

Kaeni mkao wa kula maana mengi yanakuja.
 
nchi yetu wote.katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 inampa haki kila raia kukanyaga eneo lolote ndani ya tz.kwhyo lema ucogope tuko pamoja endleza harkati.tunakuamini .UOGA NI DHAMBI.
 
Vijana 363 katika jimbo la Arumeru Mashariki, wilayani Arumeru, wameandaliwa kwa ajili ya kumlinda mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (CHADEMA), katika kampeni za ubunge Arumeru Mashariki kutokana na tishio la wazee wa kimila wa kabila la Wameru (Washiri).

Hatua hiyo imefikiwa siku chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kumtaka Lema awaombe radhi wazee wa Washiri kwa madai kuwa aliwaudhi wakati wa mazishi ya Jeremiah Sumari.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, vijana hao kupitia viongozi wao, walisema kuwa licha ya kuchukua hatua hiyo ya kumlinda Lema pia wanasubiri kuona Jeshi la Polisi litachukua hatua gani dhidi ya wazee hao kwa kutishia kuua.

Walisema kuwa kama polisi haitamchukulia hatua mwenyekiti wa Washiri, aliyetoa tamko hilo, wao watawapiga marufuku wabunge wote wa CCM na viongozi ambao hawaishi Meru, kuonekana katika jimbo hilo kuanzia Machi 9 mara kampeni zitakapoanza.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Yohane Kimuto (51) mkazi wa Sing'isi Meru, alisema kuwa ili kumhakikishia ulinzi Lema, tayari wameandaa kundi la vijana (Morani wa Kimeru) wapatao 363, kwa ajili ya kumlinda kila atakakopita wakati wote wa kampeni.
Kimuto alisema kuwa maandalizi ya vijana hao yamekamilikana wako tayari kwa ulinzi wa mbunge wao, ambaye wanamhitaji kwa hali na mali kwenye kampeni za Arumeru Mashariki.

Alisema kinyume na hapo kampeni hizo hazitakuwa salama, kwa sababu tayari kutakuwa na makundi mawili ya kumlinda Lema na lingine linalotaka kumuua na hapo amani itatoweka.

"Lazima ikumbukwe Meru tumekuwa kwenye vita tangu wakati wa vile vya kidini walipouawa wamisionari na ikajirudia tena mwaka 2009, katika mashamba ya Madira na watu kuswekwa gerezani na wengine kupoteza maisha, hili sasa hatutaki lijirudie," alionya Kimuto.

Aliongeza kuwa kwa niaba ya Wameru wenzake wanamtaka mwenyekiti wa Washiri, aliyetoa tamko hilo ajiuzulu mara moja, kwa sababu anafanya kazi ya siasa na kuacha kazi yake ya kuratibu mila na jadi za Kimeru.
Akizungumzia sakata hilo Kaimu Kamanda wa Polisi, Akili Mpwapwa, alisema mpaka sasa hawana wa kumchukulia hatua kwani hakuna mtu aliyekwenda kushtaki kutishiwa maisha.

"Ninachofahamu mimi ni kuwa mtu anapotishiwa maisha lazima atoe taarifa polisi ili apatiwe ulinzi na hivyo hadi sasa hakuna aliyetoa taarifa kuhusiana na vitisho vya Washiri," alisema Mpwapwa.

Source:Tanzania Daima
 
ukitaka kujua siasa za:
1.Haki
2.Uwazi
3.kutokuogopana
4.kuchukia na kupinga rushwa.

Hapa arumeru ndo nyumbani kwao.
Rasharasha ndo hizo.mvua itaanza kunyesha mda si mrefu.
 
Ewe mola tuepushe na hili balaaaa! Morani zaidi ya 300 si ni zaidi ya platoon 5! Hivi Moran wa Kimeru wana tofauti na wale wa Kimasai kwa maana ya ubebaji wa silaha kama sime na marungu?

Mkuu hii ni Tanzania wanayoitaka iwe. By the way, kwa mtu aliyepewa dhamana na title ya u-jaji aropoke vile, unategemea watu wenye kuta 28 za elimu maishani mwao wafanye nini?
Shame on you Tendwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom