masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,773
- 14,865
Tunaomba Kamanda Kova achukue hatua madhubuti za kuongeza ulinzi pale Mlimani City, sasa pamekuwa uwanda wa kutesa kwa vijana wa pikipiki za aina ya Boxer kwa watu wanaotoka mabenki yaliyopo.
Katika siku za karibuni ujambazi wa kuwapora wateja wa mabenki yanayohudumia wateja pale Mlimani City yameongezeka.
Kuna ambao wala hawasemi au kufungua majalada kwa vile viwango vya pesa zinazoporwa ni kidogo.
Tutakumbuka hivi karibuni jamaa aliuwawa hapo akitoka benki akiwa na fedha taslimu milioni 40.
Juzijuzi kijana mmoja akitoka benki, ametoka tu nje ya yale mageti kakzingirwa na vijana wawili walioshurutisha kutoa mfuko uliokuwa na fedha.
Kweli kijana alikuwa na shilingi laki tano, na akiwaona vijana wenyewe wadogo akataka kupambana nao, Kosa.
Hao majambazi mmoja akatoa bastola nakumlenga huyo kijana na kufyatua risasi.
Kilichomwokoa yule kijana ni kitendo cha kuona akiitoa bastola , hivyo akamrushia fuko la fedha na kuinamisha kichwa haraka , huku risasi ikipita juu ya kichwa!
Tunasema hivi, jeshi la polisi liokoe jahazi kwa kuimarisha ulinzi pale Mlimani City, kabla hapajakuwa uwanda wa mauaji yanayojirudia kila wakati.