Rais Mstaafu Kikwete kwa Umri wako na Hadhi yako kwa sasa haipendezi Kuhudhuria Matamasha ya Usiku ya Vijana Mlimani City

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,553
108,889
Yaani Unaacha Kupumzika Kwako na Kucheza na Wajukuu zako Kibao ( Wengi ) bado tu unapenda Mambo ya Vijana na unataka Kulazimisha kuwa Wewe bado hujawa Mzee na unaweza Kujichanganya katika Kumbi za Starehe au kwenda pale palipokuwa Kijiweni Kwako Saigoni kupiga Soga na Masela, Wahuni, Wadau na Watoto wa Mjini.

Hivi kweli Rais Mstaafu Kikwete Wewe ni wa kwenda katika Tamasha la Kijana Mlimani City Siku ya Jumamosi hii ijayo?

Hivi nyimbo za huyo Kijana zina Maadili kwa Jamii yetu na kwa Hadhi yako kama Rais Mstaafu ni Heshima Kwako kwenda Kuhudhuria ukichanganya na huo Umri wako unaochanja Mbuga kwa sasa?

au unaenda Kuhudhuria hilo Tamasha kwakuwa huyo Kijana ni Mwananchi ( mwana Yanga SC ) Mwenzako na kuna Wimbo kaisifia sana Yanga SC yako huku akiikandia Simba SC?

au labda una Mpango wa Kugombea tena Urais wa Tanzania hivyo unatumia mbinu za Kujichanganya na Watu mbalimbali ( hasa Wasanii ) ili Jina lako lizidi Kung'aa na labda mwaka 2025 umuombe Mama akuachie hiyo miaka Mitano ( 5 ) ijayo ili utupige zaidi kwa Madili mbalimbali kama ulivyotufanyia mwaka 2005 hadi 2015 kiasi kwamba aliyechukua Kijiti chako alikuta kule Jikoni Kiuchumi hakuna Kitu?

Mbona Wastaadu wenzako wengi tu ( achilia mbali wale waliokuwa Marais kama Wewe ) bali hata waliokuwa Makamu wa Marais, Mawaziri Wakuu, Makatibu Wakuu ( CS's ), Mabalozi na Wakuu wa Majeshi hawana Shobo na Viherehere vya kutaka Kung'ang'ania Mambo ya Vijana na Ujana na badala yake Wametulia tu huku wakimtumikia zaidi Mwenyezi Mungu Kimaombi?

Hivi huwa haujishtukii tu Sometimes?
 
Ungekuwa unamjua huyo mzee usingeandika uzi wako. tuache tunao mfahamu mzee wamagomeni aka msoga.

Mtu wa amani sana na furahaa mda wote na kila kijana anataka kuwepo karibu naye.

ningepata babu au baba wa hivi nisingekuwa chizcom. nigekuwa naitwa chizbilion
 
Acha ujinga we dogo

Unataka asikuze Sanaa za vijana kumbuka vjana wanapambana kutafuta riziki n jambo jema kwa viongozi kuwaunga mkono vjana wapambanaji

Umetokeo kijijini na umeaminishwa mziki n uhuni kitu ambacho s kweli

USA mziki unachangia pato la 12% la taifa Hilo Sasa wakiutelekeza unadhan itakuwaje

Mbona wakat wa kampen mnawatumia Hawa vjana kujaza viwanja?

Mkuu badilika dunia ya Sasa siyo ile ya BUNDA ulikoishi miaka ya ujima

Wasalimie kawe ya BUNDA
 
Kwa JK simshangai. Amekua hivyo tangu hajawa Rais na hadi akiwa Rais walikua wanamdaka mlangoni kwasababu ya protocol tu. Anapenda maisha ya kujichanganya ndo maana huoni kama kachoka. Mi naona ni maisha yake. Namkubali sana kwakweli sasa maisha yake binafsi tusiyaingilie sana
 
Back
Top Bottom