kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
Kamanda Kova amedai atamfikisha mahakamani muda mfupi ujao mwenyekiti wa BAWACHA,Mh. Halima Mdee.
Chanzo: Startv magazeti
My take;
UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NI JAMBO JEMA
Kabla hajamfikisha Halima Mdee mahakamani ni vema akatuambia kwanza juu ya wale waliokamatwa kuhusika na kifo cha Dr. Mvungi hadi sasa kesi imefikia wapi na je zile Kofia na Bendera za CHADEMA alizotuonyesha kipindi kile na kusema kuwa walikamatwa nazo watuhumiwa na kujinathibisha kuwa ni wafuasi wa CHADEMA tunaomba atuthibitishie na hilo pia.
- Na picha ya Kwanza hapo chini inajionyesha wazi kwa mbele kuna mtu aliyekaa ambaye amevaa nguo za CCM (Kijani) ni vema tukaambiwa ni nani na alikwenda hapo kwa ajili ya nini
Hivi ni vifaa alivyotuonyesha KOVA kuwa walikamatwa navyo wale watuhumiwa wa mauaji ya Dr. Mvungi.