Kamanda Kova: Tutamfikisha Halima Mdee mahakamani

Kamanda Kova: Tutamfikisha Halima Mdee mahakamani

Kamanda Kova amedai atamfikisha mahakamani muda mfupi ujao mwenyekiti wa BAWACHA,Mh. Halima Mdee.

Chanzo: Startv magazeti

My take;

UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NI JAMBO JEMA
Kabla ya kumfikisha Halima Mdee mahakamani kwa hilo kosa analoliita kuandamana bila kibali cha polisi, ni vyema sasa kwa spidi hiyo hiyo akawaburuza mahakamani wale wote waliokwapua zile bilioni 200, kwenye akaunti ya Escrow pale benki kuu.

Hapo ndipo tutakapompa bigup kamanda wetu.
 
Wewe hujui siasa kama vile CDM na ndiyo maana mtalalama lakini ikulu mtaambulia kualikwa kwenda kunywa juisi siku ambayo mshindi wa CCM atakapoamua kuwaalika. Kiongozi wa siasa kazi yake ni kuhimiza wananchi washiriki kwenye shughuli za maendeleo siyo kufanya mwenyewe, bali katika kuhamasisha lazima awe karibu na wananchi kitu ambacho CDM na wapinzani wengine kimewashinda. Wananchi wenyewe wanajua hilo hawahitaji hata kukumbushwa. CDM wenyewe wanaandama tu kwenye barabara za lami ambazo zimejengwa na serikali ya CCM huku wakiidharau na kuikejeli. Hawataki kwenda kujenga mizizi ya chama karibu na wananchi. Hivyo walie tu.


Umetapeliwa mkuu ! Si kila anayeshika tofali anajenga , hebu nionyeshe mradi wowote alioshiri kinana uno exist .
 
Kinana anashiriki kujenga zahanati, maabara za shule, visima vya maji etc kwa ajili ya wananchi, CDM wanajenga nini humo barabarani?
Kinana ni muhuni huwezi igiza kitu katika maisha ya wetu anafrustration za kukamatwa meli zake na kujulikana kwamba ndio mmliki wa mtandao wa wavuna meno ya Tembo
 
Wewe hujui siasa kama vile CDM na ndiyo maana mtalalama lakini ikulu mtaambulia kualikwa kwenda kunywa juisi siku ambayo mshindi wa CCM atakapoamua kuwaalika. Kiongozi wa siasa kazi yake ni kuhimiza wananchi washiriki kwenye shughuli za maendeleo siyo kufanya mwenyewe, bali katika kuhamasisha lazima awe karibu na wananchi kitu ambacho CDM na wapinzani wengine kimewashinda. Wananchi wenyewe wanajua hilo hawahitaji hata kukumbushwa. CDM wenyewe wanaandama tu kwenye barabara za lami ambazo zimejengwa na serikali ya CCM huku wakiidharau na kuikejeli. Hawataki kwenda kujenga mizizi ya chama karibu na wananchi. Hivyo walie tu.
Angejua kuhimiza basi deni la taifa lingepungua na umasikini wa wananchi ungepungua anafanya vile kwa kamera hana lolote kama wanahela za kuwasaidia wananchi kwa nini wameanza kuuwa watu ili wachangie maabara
 
Matusi hayasaidii, mnamdanganya tu huyo Mdee, watakaohangaika ni familia yake wala sio wewe.

Familia ya Mdee ni sisi wana CDM ndio mana hatukubali wala hatutakubali asumbuliwe wala kuhangaishwa hata kukerwa kwa namna yeyote ile tuko vizuri sana.
 
Ukishaona thread wameingia Lizaboni na MSALANI basi ni inabadilika na kuwa Uchafu
 
Last edited by a moderator:
Familia ya Mdee ni sisi wana CDM ndio mana hatukubali wala hatutakubali asumbuliwe wala kuhangaishwa hata kukerwa kwa namna yeyote ile tuko vizuri sana.

Sasa mbona umekaa kwenye kompyuta unaandika andika ovyo tu!
 
Ndugu, polisi hawatoi go ahead wanataarifiwa tu kwa maandamano ya amani.. Hiyo ya go ahead inatokea tu kwa sababu ya watu ku-avoid fujo na polisi na kupata taarifa endapo njia watakazotumia tayari zina shughuli nyingine kama misafara ya viongozi n.k.
Ndugu,
Haya siyo maneno yangu bali ni maneno ya sheria.

Soma Sheria ya Jeshi La Polisi Na Huduma Saidizi [Sheria Kuu], Sura ya 322 katika Ibara ya 43 ambayo inasema,
43. (1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-

(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;

(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na

(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa
mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.

(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.

(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.

(4) Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au mwendelezo wa mkusanyiko au maandamano katika hadhara/sehemu za umma ambayo yanaitishwa, kusanywa, kuundwa au andaliwa vinginevyo tofauti kulingana na taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kutokana na kwamba maelezo yaliyoainishwa na Waziri chini ya aya (c) ya kifungu kidogo cha (1) yamekiukwa au yanakiukwa , na anaweza, kwa dhumuni lolote lililotajwa, kutoa amri kama atakavyoona ni lazima au inafaa , ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya mkusanyiko wowote au maandamano kama ilivyotajwa hapo juu.

(5) Waziri anaweza, kwa amri, kutangaza kwamba masharti ya kifungu hiki hayatatumika katika mkusanyiko au maandamano yaliyoitishwa, kusanywa, kuundwa au kupangwa pasipokuwepo na sababu moja au zaidi au muungano wa sababu moja au zaidi kama itakavyoweza kuainishwa katika amri hiyo.

(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya 25 ya kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.
 
Mdee haya mavurugu sijui kafundishwa na nani.. BAWACHA wamemuharibu sana
 
Back
Top Bottom