ieleweke wazi kuwa sitetei wahalifu , ila kimfumo, makundi ya panya road, mbwa mwitu , watoto wa mbwa na wamarekani weusi ni matokeo ya ufisadi wa muda mrefu unaofugwa na kuenziwa na genge la magamba , ni hivi , kama Anna Tibaijuka,Werema na Chenge wanachota 1.6 billion za umma kila mmoja na kudeposit kwenye akaunti zao binafsi unategemea wabongo wengine 48 millioni people watapataje mzunguko wa pesa walizochukua , unategemea dawa zitatoka wapi hospitalini na unategemea wengine watapata wapi hela ya kula? na unategemea pesa za kuwezesha elimu bure zitatoka wapi ? na hawa watoto wa mbwa waliokosa elimu technically watakosa na ajira na sasa ndo hao wanaturudi mchana kweupe! hawana cha kupoteza manake wana njaa na hawana namna ya kupata chakula kihalali! sera za magamba zimeshindwa kufanya kazi! nafikiri huu ni wakati watanzania wanatakiwa wasifanye kosa uchaguzi mkuu ujao, tujaribu na wengine hawa wameshindwa kwa miaka hamsini! inatosha! Nyerere alisema nchi ina maadui watatu, ujinga , maradhi na umaskini , na sasa maadui badala ya kupungua wameongezeka, adui wa nne ni ufisadi! watanzania tuamke tuseme imetosha. nitafurahi watanzania wenzangu tukijaribu wengine! amini nawaambia wana JF wenzangu, magamba wameiba sana na walifikiri hakuna kitakachotokea sasa na wanajionea kwa macho matokeo ya wizi wao kwa kuzalisha watoto hawa wa mbwa! haya sasa na tuwapige mabomu na tuwafunge watoto wetu wenyewe tuliowanyima elimu na ajira kwa kuiba mali zao za umma!safari ni ndefu , kwa tathmini zangu ndogo za sosiolojia ya Mlimani bomu ni kubwa sana hapa bongo kuliko tunavyodhani na tutegemee makubwa zaidi ya sasa ya watoto wa mbwa kama social and economic conditions za bongo hazitachange hasa unequal distribution of resources! nadhani huko tuendako tutahitaji wanajeshi kabisa kushughulikia na kudhibiti wasio na ajira! ni mtazamo tu!