Lakini hapo hapo akasema wamewakamata viongozi wao wawili na wanatoa onyo kwa wale wooote ambao hawajakamatwa kujisalimisha.
Mwisho akatuomba wananchi tukiwakamata "Panya Road" waliofanya fujo Jana tusiwaue,maana ni vijana waliokata tamaa!Sasa kama hawapo sijui hayo maneno ya Kova ya nini?Kanikasirisha Sana Jana...
Mi nilikuwa Sinza na hawa wahuni wamefanya yao,Kova akiri tu jeshi lake ni dhaifu na yeye ameshindwa kuwadhibiti hawa wahuni.
Talk about issues, unapochanganya tukio na siasa unashindwa kueleweka. Naamini jina lako tu linaonesha wewe ni wa chama gani
Wana JF kwanza kabisa ieleweke wazi kuwa kamwe sitetei wahalifu hata siku moja , ila kwa mtazamo wangu kimfumo, makundi ya panya road, mbwa mwitu , watoto wa mbwa na wamarekani weusi ni matokeo na zao la ufisadi wa muda mrefu unaofugwa na kuenziwa na genge la magamba , ni hivi , kama Anna Tibaijuka,Werema na Chenge wanachota 1.6 billion za umma kila mmoja na kudeposit kwenye akaunti zao binafsi 4.5 billion Tsh unategemea wabongo wengine 48 millioni watapataje mzunguko wa pesa kubwa namna hiyo walizochukua? , kwa kutumia akili ndogo tu ya kukaa kijiweni kwa kukosa ajira unaweza kujiuliza kama genge la magamba lina watu lukuki walio ofisini na waliostaafu na wote kwa miaka hamsini ya kuwaletea umaskini wabongo , wanakula bata Masaki kwa kutumia mabilioni ya pesa za umma na kusomesha watoto wao nje ya nchi , sie tunaonana na watoto wao huku! sasa kwa namna genge zima wanaendesha maisha ya kifahari tunayoyaona na wanatumia mali ya umma sasa unadhani dawa zitatoka wapi hospitalini na unategemea maskini wa bongo kama hawa watoto wa mbwa watapata wapi hela ya kula? na unategemea pesa za kuwezesha elimu bure zitatoka wapi? na hawa watoto wa mbwa tuliowanyima elimu bora technically watakosa na ajira na sasa ndo hao wanaturudi mchana kweupe! hawa hawana cha kupoteza manake hawana elimu, hawana ajira , hawana wazazi na wana njaa na hawana namna ya kupata chakula kihalali! kwa mawazo yangu sera za magamba zimeshindwa kufanya kazi! nafikiri huu ni wakati watanzania wanatakiwa wasifanye kosa uchaguzi mkuu ujao, tujaribu na wengine hawa wameshindwa kwa miaka hamsini! inatosha! Nyerere alisema nchi ina maadui watatu, ujinga , maradhi na umaskini , na sasa maadui badala ya kupungua wameongezeka, adui wa nne ni ufisadi! watanzania tuamke tuseme imetosha. nitafurahi watanzania wenzangu tukijaribu wengine! amini nawaambia wana JF wenzangu, magamba wameiba sana na walifikiri hakuna kitakachotokea na sasa wanajionea kwa macho matokeo ya wizi wao kwa kuzalisha watoto hawa wa mbwa! haya sasa na tuwapige mabomu na tuwafunge watoto wetu wenyewe tuliowanyima elimu na ajira kwa kuiba mali zao za umma kwa miaka hamsini ya umaskini! ninaamini safari ni ndefu , kwa tathmini zangu ndogo za sosiolojia ya Mlimani bomu ni kubwa sana hapa bongo kuliko tunavyodhani na sio kwamba ninaombea itokee ila kimantiki na tutegemee makubwa zaidi ya sasa ya watoto wa mbwa kama social and economic conditions za bongo hazitachange hasa this unequal distribution of resources iliyokithiri bongo manake gap la walio nacho na masikini ni kubwa sana kwa sasa! hebu angalia Chenge ameiba 1.6b na anazo kwenye akaunti na mwingine hana 200 ya kunywa chai asubuhi! nadhani kama hatutadeal na current situation kwa namna inavyopasa na si kinafiki na kwa jazba basi huko tuendako tutahitaji wanajeshi kabisa kuingia vitani kushughulikia na kudhibiti watoto na vijana wasio na elimu na ajira! ni mtazamo tu!
kwani ITV ni telvision ya taifa? iweje aende itv wakati kuna chanel ya taifa TBC?
Hakuna cha paka wala panya ni uoga wa kike tu
hivi hizi kauli za "polisi" tunazozisikia kila kukicha za "KUTOA ONYO KWA WAHALIFU, NA KUWATAKA WAJISALIMISHE", ...hivi hili si ni dua la kuku? TANGU LINI MHALIFU AKAOMBWA KUJISALIMISHA! ...watuweke wazi tu kwamba wamezidiwa mbinu!!