Kamanda Chagonja amtisha na kumkejeli Dr. Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Chagonja amtisha na kumkejeli Dr. Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 30, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu Mkuu wa operesheni anashangaza kweli kweli. Amenukuiwa leo na gazeti la M<ajira (na mengineyo) akisema polissi wana haki ya kuwakamata madaktari wanaogoma na kuwashitaki mahakamani, kwani wanakiuka amri ya mahakama ya kutogoma.

  Hajui kwamba amri yoyote ya mahakama inayotokana na hukumu yake (iliyotokana na ombi kutoka AG) hutekelezwa tu kwa mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa waliokiuka. Hivyo kabla ya kuwakamata madaktari waliogoma, ni lazima serikali iombe tena mahakama hiyo itoe hati ya kuwakamata.

  Polisi wetu wanaboronga tu mambo kwa kauli zao za vitisho za kuwalamba miguu wakubwa, na siyio katika kusimamia haki.

  Isitoshe kamanda huyo huyo amesema kuwa jeshi la polisi halighusiki kabisa na utekwa na kupigwa kwa Dr Ulimboka. kisha toia hukumu tayari -- kwani yeye ni mahakama, au uchunguzi tayari umekamilika?

  Watu kama hawa ndiyo husababisha vurugu nchini.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyu nilimdharau tangu wakati wa mauaji ya raia wasio na hatia Arusha.Huyu ni mwanachama hai wa CCM
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kazi yake kubwa ni kufunika makashfa ya wakubwa waliomuweka. wakisha mtumia watamtupilia mbali -- wewe subiri tu. Hakuna polisi aliyewahi kuangukia u-RC au u-DC baada ya kustaafu.
   
 4. M

  MTK JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  chagonja anatetea tumbo lake na huo ndio wajibu wake kimsingi; mwacheni atimize wajibu wake na madaktari watafanya lililo ndani ya haki yao ya msingi kama professionals na binadamu, swali ambalo Chagonja anatakiwa ajiulize ni kama kuwakamata madaktari na kuwafikisha mahakamani je atakuwa ametatua tatizo katika mahospitali!?; kwa sababu ndio hicho tu anachoweza kufanya kwani hawezi kuwaua wote akawapeleka msitu wa Zombe mabwepande!! la hasha, kengele imeshalia muhanga ni Dr Ulli pekee zaidi ya hapo mambo yatageuka 360%
  Hii sio Tanzania ya mwaka 47, Bi Fatou Bensouda na ICC kule The Hague wapo kwa ajili hiyo; Laurent Gbabgo was more powerful than 100 Chagonja's!
  wahenga wametufundisha "Unaweza kumpeleka n'gombe mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji" Kimenuka; timiza wajibu wako chagonja ukijua kwamba "To every action there is always an equal and opposite reaction" hata vitisho vya Gadafi havikumuokoa kwenda kujificha kwenye mtaro wa maji!! What goes comes around!
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Chagonja mi mbumbumbu ....
   
 6. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nikurekebishe kidogo tafadhari. Hapo kwenye rangi nyekundu mkono wako umeteleza nadhani. Huyu bwana ni
  mwanachama HOI wa CCM!!!
   
 7. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Umesema kila kitu kaka!!!
   
 8. U

  UKUBWA JIWE New Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jeshi la polisi ni kweli halihusiki mbona dr.kwa kauli yake amesema tuhuma zinazosambazwa kuhusu kamanda msangi sio za kweli na yeye wala hajasema kuwa arudishiwe simu yake na wallet yake na kamanda huyo.
   
 9. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  chagonja ni miongoni mwa maafisa wanaotumia vyeti bandia waliotambuliwa na NIDA
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhhhhh nimekumbuka chagonja=ugonjwa
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  heeee ngoja nianze wekend sasa
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi lenyewe lajijuwa kama ni mbumbumbu wa sheria? Kuna siku nilimsikia akisema polisi wanaruhusiwa kuuwa na akataja kifungu cha sheria ya kanuni za Adhabu.

  Nilikisoma kile kifungu na kugundua kuwa hakiwaruhusu kuuwa ila tu kama ni kwa kujitetea maisha yao yakiwa hatarini kuuwawa. Lakin tumeona polisi wakiuwa wananchi huku wananchi hao wakiwa hawana silaha zozote za moto, pengine mawe tu na fimbo. Wengine wameuwawa kwa risasi visogoni huku wakikimbia.
   
 13. U

  UKUBWA JIWE New Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli walimwengu waongo, hakuna ACP anayeitwa chagonja, pili huna uhakikika na elimu yake, tatu soma public sercvice act ujue watu wanaoruhisiwa kugoma kisheria, nne usikurupuke kuandika mambo ambayo huyajui
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  nimemuona kwenye TV jana wakati wa taarifa ya habari saa mbili, anawasihi madaktari warudi kazini.

  Anasema haya maneno kama nani? Polisi na kesi za kazi wapi na wapi? Hii yote inaashiria kuwa Chagonja ni mbumbumbu
   
 15. K

  Kishili JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 293
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hatujasoma wala kusikia haya uliyoandika si mumrudishie wallet na simu yake au unataka kusema kuwa Dr hakuwa na simu?
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata kwenye kesi ya mauwaji ya wafanyabiashara wa Morogoro - ZOMBE CASE - polisi walisema, "Wale ni majambazi." Lakini uchunguzi huru ukafanyika na kubainika kuwa wafanyabiashara wale waliuwawa mikononi mwa polisi na hawakuwa hata na chembe ya ujambazi.

  Sasa nani ataamini Kagonja na majambazi menzake iliyojivisha kilemba cha ulinzi wa usalama wa raia kumbe ni wauaji wakubwa?
   
 17. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  "If you only have a hammer, you tend to see every problem as a nail. Abraham Maslow". Kumbe hili halina ubishi. Kuwafunga madokta wote hao kwa sababu ya mgomo, lazima uwe na maguvu sana maana utatengeneza tatizo kubwa kuliko lile la kuyumba kwa uchumi baada ya vita vya Kagera
   
 19. Q

  Qixima mQiqa Senior Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni mngese sana
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kamanda wa Operesheni maalum Paul Chagonja amemtisha Dr Ulimboka Stephen kwamba kauli zake juu ya kumtambua ACP Msangi kwamba alihusika kumteka zitamgharimu mwenyewe.

  Kamanda Chagonja amesema hakuna hata mtu mmoja anayejua ni nani alimteka na kumpiga Dr Ulimboka na ndiyo maana tume maalum inafanya uchunguzi.

  Katika kejeli na kiburi cha hali ya juu Kamishna Chagonja alihoji mbele ya waandishi ''NANI ANA UHAKIKA JE KAMA ALIKAMATWA NA MKE WA MTU NDIYO AKAPIGWA?''

  Source: Mtanzania Jumamosi
   
Loading...