tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,241
- 4,466
Mtunzi mmoja maarufu, George Bernard Shaw, aliwahi kusema: "Ikiwa wachumi wote wangewekwa kona hadi kona, hawangefikia hitimisho (tamati)." (Tafsiri yangu)
Kwa hiyo, inakuwaje wachumi wawili wabobezi wenye uzoefu, maarifa, wanasoma na kuchambua takwimu sawa na kila mmoja anakuja na utabiri au njia tofauti kabisa ya kukuza uchumi wa taifa? Kwa nini wataalamu hawa mara nyingi hawakubaliani na wenzao? Kuna sababu nyingi, lakini moja ni kuu - Shule ya uchumi anayoamini (economic schools of thought).
Wachumi wengi hawakubaliani kwa sababu wengi wao kawaida huanguka katika shule mbili za kiuchumi zinazoshindana kimawazo: Uchumi wa Keynesian na uchumi wa soko huria.
Wachumi wa Keynesian wanaamini kuwa serikali inapaswa kuchukua jukumu katika kusimamia masoko ilhali wachumi wa soko huria (naamini Mwigulu yupo huku) wanaamini kwamba serikali inapaswa kutoweka mikono yake na kuacha soko lijidhibiti.
Sasa Mwigulu, kujifanya yeye kama mchumi wa Kwanza Duniani anayepaswa kusikilizwa yeye tu ni kosa, maana anachoamini wachumi wengi hawakiamini.
Mwigulu acha KIBURI.