Kama upo mtaani muda mrefu bila kazi, tatizo ni wewe!

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,370
Siingiagi sana huku jukwaa la ajira lakini leo nimepitia post nyingi sana na nimesoma comments mbalimbali za watu.

Nachotaka nikwambie tu wewe unaeangaika muda mrefu kutafuta kazi na hupati tatizo sio mtu mwingine yoyote tatizo ni wewe mwenyewe.

Yes tatizo ni wewe, japo wengi hatupendi kukubali huu ukweli kwamba tuna mapungufu upande wetu siku zote tunapenda kutafuta mtu wa kumbebesha mizigo yetu ya lawama.

Vijana wengi tunapenda kulaumu na tukishadanganywa na wajanja haswa wanasiasa basi ndio tunarelax kabisa tukiamini kuna mtu ndio tatizo ndio maana hatutoboi.

Mimi binafsi sinaga time ya kulaumu mtu na imenisaidia sana. Nachukulia almost kila kitu positively.

Ili upate ajira tena nzuri unahitaji vitu vitatu.

1. Skills
2. Connection
3. Confidence au uthubutu.

Kabla ya kumlaumu mtu au kulalamika January mpaka December, jiulize umeshafanya lolote kuwa na hivyo vitu vitatu?

Je ukiitwa kwenye interview wanayohitaji watu wenye uwezo unaweza kuwashinda wenzako?

Unaweza kuandika CV na cover letter inayoweza kukuuza?
Unaweza kujibu vizuri maswali ya kwenye interview?

Una skills ambazo zinahitajika au zinazoweza kukutofautisha na degree holders wenzako?
Ukipata kazi unaweza kuleta results ?

Kabla haujapeleka lawama popote pale anza na wewe.

Lazima ujifunze tuko dunia ya kibepari hakuna wa kukuonea huruma hata ukitia huruma.

Kila mtu na maisha yake usitake watu wapiganie maisha yako wakati umekaa kizembe tu kama fala flani.
 
Namba moja na mbili zimachukua muda mrefu kuzijenga,sio Swala linalozuka tu kijana akitoka chuoni,it takes veeery long time,
You don't just wake up one day and,wolaaaa you have connections!

Kwa uzoefu wangu inabidi upitie ajira kadhaa Ili kupata connections,au uwe na ndugu jamaa ambao ni well connected Ili wakuingize kwenye ajira.

Udhubutu ni muhimu sana,vijana inabidi wawe na uwezo hata wa kuuliza,na kuomba msaada specific.

Kitaani kwetu kulikuwa na vijana Wana shahada zao za uhandisi,walikuwa wananipita tu,siku walipo ambiwa ongeeni na huyo bro jirani,anaweza kuwasaidia,mambo yalibadirika fasta.
 
Namba moja na mbili zimachukua muda mrefu kuzijenga,sio Swala linalozuka tu kijana akitoka chuoni,it takes veeery long time,
You don't just wake up one day and,wolaaaa you have connections!..
Kujiongezea skills ulimwengu wa sasa hakuitaji muda mrefu kama unavyozungumza.

Ukiingia YouTube kuna kila kitu.

Kuna platform kama udemy na nyingine unaweza kujifunza skills kibao.

Connection siku hizi kupata sio lazima kwa mjomba hata huku kwenye social media ukiamua kufanya interactions in a positive way kuna connection kibao mfano mimi kuna watu nafanya nao biashara tulikutana Twitter wengine kwenye groups za WhatsApp.
 
Mkishapata kazi mna amini mnaelewa kila kituu.
Nilishawai pitia phase kama yako kwenye maisha yangu. Nilikuwa naona kila mtu mbaya na kila mtu hataki kunisaidia.

Kuna siku niliamka nikajihukumu mwenyewe kwa nini siitwi interview? kwa nini nikipata interview sitoboi? nnakosa nini wakati wengine wana ajiriwa?

Hapo ndio nilianza kubadili page ya life yangu.

Nilirudi kuandika upya CV yangu na cover letter.
Nikafungua account LinkedIn na nikatafuta mshikaji akanisaidia namna ya kuiandika na kuitumia.

Nilijipa miezi miwili ya kupiga tizi la interview nilikuwa nna maswali karibu yote kwenye interview ya field yangu niliyaandaa kutumia google na sources mbalimbali. Nikawa na majibu yake, so ilikuwa kawaida kunikuta ghetto nazungumza mwenyewe kama chizi au sometimes naenda zangu coco beach.

Nilikubali weakness yangu nikaifanyia kazi.
 
Acha kusema wenzio wavivu, waconnect kwa waliokupa kazi nao wapate, Mungu akikubariki kidogo unaanza kuona wenzio vilaza! Haupo kwenye viatu vyao
Kwa nini usubiri watu wakuconnect!? wasipotokea ni uzembe wa nani?

Mfano mimi kazi yangu ya kwanza niliipata LinkedIn, nilienda mwenyewe inbox (inmail) kwa don wa kampuni flani nikajieleza kila kitu mimi ni nani, skills zangu, elimu yangu, nitaongeza thamani gani kwenye organization yao, nikaacha details zote muhimu. Siku ya siku nilishasahau nikaona email naitwa kwa ajili ya discussion kuna opportunity flani.
 
Nilishawai pitia phase kama yako kwenye maisha yangu. Nilikuwa naona kila mtu mbaya na kila mtu hataki kunisaidia.

Kuna siku niliamka nikajihukumu mwenyewe kwa nini siitwi interview? kwa nini nikipata interview sitoboi? nnakosa nini wakati wengine wana ajiriwa?

Hapo ndio nilianza kubadili page ya life yangu.

Nilirudi kuandika upya CV yangu na cover letter.
Nikafungua account LinkedIn na nikatafuta mshikaji akanisaidia namna ya kuiandika na kuitumia.

Nilijipa miezi miwili ya kupiga tizi la interview nilikuwa nna maswali karibu yote kwenye interview ya field yangu niliyaandaa kutumia google na sources mbalimbali. Nikawa na majibu yake, so ilikuwa kawaida kunikuta ghetto nazungumza mwenyewe kama chizi au sometimes naenda zangu coco beach.

Nilikubali weakness yangu nikaifanyia kazi.
Aaaagh! Kila mtu ana riziki yake bhana! Jitihada hazishindi kudra! Wapo watu wametumia kila mbinu lakini wapiiii....

Kama Mungu amekubariki ajira,mshukuru tu kisha uwaombee na wengine awafanyie wepesi.

Ukifanikiwa usiwaone wengine kama wana makosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...hujielewi ww hujui kuna matajir duniani km elon musk na jack ma walio scramble kupata kazi na hawakupata wakaamua kuw self made
Achana na story za motivesheno spika wewe sio Elon Musk au Jack Ma hao ni gifted.

Ona sasa huna kazi hauna mradi wowote unajifariji na story za kina Jack Ma na umri unakwenda unaonekana boya tu kitaa sababu hauna maisha.
 
Aaaagh! Kila mtu ana riziki yake bhana! Jitihada hazishindi kudra! Wapo watu wametumia kila mbinu lakini wapiiii....

Kama Mungu amekubariki ajira,mshukuru tu kisha uwaombee na wengine awafanyie wepesi.

Ukifanikiwa usiwaone wengine kama wana makosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri ukienda kwenye somo la riziki ndio unaweza zeeka umetulia unasubiri rizki.

Unajua kwamba rizki ni kama maji uwa inafata mkondo?

What if haukuzaliwa kwenye mkondo wa rizki?

Usitie huruma mzee hakuna wa kukuonea huruma dunia hii.
 
Anaemuona boya mwenzie kisa yeye kapata, Atambue dunia duara na kesho yetu aijuaye ni Muumba
Usijifariji kwa maneno ya huruma hata muumba anasaidia waliojiandaa. Mungu alisimama na wafalme waliokuwa wanaua maboya maboya wanaotia huruma.

Utapewa opportunity na Mungu lakini haujajiandaa, unapigwa maswali unatetemeka haujui uanzie wapi Mungu anampa aliye tayari.
 
Me nimejiajili sijaajiliwa, na nina vyeti safi mzee na nimeacha kazi 2 kisa naona maslahi hayafiki malengo yangu, sitilii huruma ila naelewa haso za watu
 
Mungu akusamehe, hujui usemalo.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Si ajabu ukaanza kunilaumu mimi ndio nakukwamisha au nakukatisha tamaa. 😂😂😂😂

Toka kwenye comfort zone pambana.

Tuma hiyo CV, tuma hiyo proposal, jinoe uwe jembe watu wakutafute, ingia front tafuta opportunities ikibidi tumia njia chafu.

Usitie huruma hakuna anaekuonea huruma sio mjomba sio bro sio dada sio rais wako. Dunia ni maisha ya upweke ukiwa nacho ni cha wote ukipigika na maisha yako peke yako.
 
Back
Top Bottom