Kama unaona Bei ya mafuta iko juu na huwezi kuimudu - Hamia Burundi

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Ndugu zangu ukweli lazima usemwe.

Nchi inajengwa na wananchi kwa kuchangia maendeleo. Mnataka tuwe kama china, mnataka tuwe kama Korea au Japani lakino hamtaki njia walizotumia kufikia huko waliko. Hizi ni ndoto za alinacha.

Mnataka maendeleo lakini hamtaki wajibu.

Tuliwambia kuhusu Katiba Mpya itakayodhibiti ubadhilifu wa mali, kusimamia rasilimali za taifa kunufaisha watanzania wote mkakataa mkasema nyie ni wazalendo sana.

Sasa mnalia nini?.

Mlisema upinzani uliwachelewesha sana. Mkakata wagombea wote ili mfike pazuri. Nchi iko mikononi mweny sasa nini kimewashinda? Kila mahali wizi mtupu.

Hata leo tunaambiwa Waziri Mkuu Amenusa harufu ya ubadhilifu wa mali huko MSD wa mabilioni ya fedha. Huku watanzania mkiwakamua kwa lundo la makodi.

Ewe mwananchi wakawaida ni wakati sasa wa kufata ule ushauei murua. Ushauri wa waziri wa Fedha Dr Mwigulu kama unaona mambo yako hayako sawa badala ya kulalamika Hamia burundi uache kutupigia makelele.

Kuna wanaccm maelfu kwa maelfu wanalalamika sana. Hasa wnaatupia lawama kwa Rais Wetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan kitu ambacho sio sawa.

Kama unaona Rais na Kundi lake wanafaidi sana badala ya wewe kuendelea kutupigia makelele ya malalamiko na vilio visivyo na tija bora uungane nao na wewe ule asali. Kama huwezi kaa kimya.

Mwisho: Mtaitaka katiba mpya muda ambao sisi tutakuwa tumeshaachana nayo tunaendelea na maisha mengine.

Katiba Mpya ni sasa.
 
Tabia ya kumlalamikia Rais kila kitu ikome
Sisiem bana..kila likifanyika zuri mnasema mama anaupiga mwingi,mara ooh asante serikali ya mama Samia Kwa kutufanyia hiki na blah blah kibao

Sasa yanapotokea mabaya msiyoyapenda Kwa nn asilaumiwe yeye pia?

Burundi tumegoma kwenda tutabanana hapa hapa bongo
 
Sisiem bana..kila likifanyika zuri mnasema mama anaupiga mwingi,mara ooh asante serikali ya mama Samia Kwa kutufanyia hiki na blah blah kibao

Sasa yanapotokea mabaya msiyoyapenda Kwa nn asilaumiwe yeye pia?

Burundi tumegoma kwenda tutabanana hapa hapa bongo
Hamtaki kwenda burundi bado muwe tayari kujenga nchi yenu kwa kulipa kodi
 
Kitu ambacho sijaona kupanda bei ni Kahawa chungu tu siku nayo ikipanda Vijiwe vyote vitamuandama Mwugulu hadi Nyumbani kwake.
 
Kama Katiba ndio itakuwa inatisha watu wasiibe au itadhibiti wizi Basi na iwe
Ila siamini kama Katiba itasababisha watu wawe na hofu ya sheria

Wizi hauishi kwa maaandishi bali sheria kali zitakazofuatwa
 
Back
Top Bottom