Nakubaliana na wewe. Kule majuu ni mateso matupu. Kwanza gharama za maisha ziko juu, pesa unayopata ni kidogo kulinganisha na matumizi yaani (hand to mouth), ni vigumu kuweka akiba, hakuna cha ndugu yangu atanisaidia, hakuna kutembeleana kuwa weekend nitakula kwa ndugu yangu(bajeti yao ni ya kufa mtu) na mwisho hakuna loose money kwa maana ya kick back. Kule kama unapata $5000 sidhani kuwa unaweza kufanya saving yeyote. Huku kwetu kama unaweza kuweka angalau hata Tshs.500,000 baada ya matumizi yako yote nakushauri usiende majuu kule ni mateso makubwa.Mtu mzima unafanya kazi mpaka masaa 18 kwa siku kwa sbabu ya utafutaji. Hivyo ndivyo wanavyoteseka huko.