Kama una mpenzi ambaye yupo mbali yataka moyo sana

Wahenga walisema "Fimbo ya mbali haiui Nyoka"

Hivyohivyo watu walio mbali yako hawawezi kukuua wala kuua ndoto yako ila watu wa karibu, ulioruhusu wakujue vizuri, ulioruhusu ukaribu nao.
.
totoadela
Watu8
 
Kuna mwanafalsafa anaitwa Hope urassa aliwahi kuandika namnukuu" Mapenzi ya mbali yatakua imara sana kama wote wanne mkiwa serious "mwisho wa kunukuu
Ya mbali yanafaa ila picha linatisha hili
 

Attachments

  • FB_IMG_1714231467403.jpg
    FB_IMG_1714231467403.jpg
    71.4 KB · Views: 3
Ni sehemu ndogo sana ya wapenzi wanaoishi mbalimbali ambao hudumu kwenye uhusiano wao kwa muda mrefu.

Hiki kinaonekana kuwa ni kitendawili kigumu sana kwa wapenzi wengi kuvumiliana kwenye uhusiano bila kusalitiana.

Ninapozungumzia umbali ninamaanisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa au mkoa na mkoa au nchi na nchi au bara na bara.

Ninaamini miongoni mwetu ama tumeshuhudia au kusikia au kuona au kuadithiwa kuwa kuna mwanaume au mwanamke ambaye alikuwa na mpenzi, mara mpenzi wake akapata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine au nchi nyingine, lakini mwisho wa siku ukasikia wapenzi wale wameachana baada ya mmoja kupata mpenzi mwingine huko aliko.

Inawezekana mpenzi wako alihamishwa kikazi nje ya wilaya uliyopo, lakini mwisho wa siku ukabaini kuwa mwenzio amepata mtu mwingine na mapenzi kwako yameanza kupungua au yamepungua kama siyo kwisha kabisa.

Kwanza kabisa ili udumu na mpenzi wako kuwa na ...

UAMINIFU
Kutokuwa na uaminifu miongoni mwenu, kama wapenzi mtakuwa ni waaminifu katika uhusiano wenu, basi kila unapoingiwa na pepo wa usaliti unakumbuka uzuri wa mpenzi wako, basi unaacha na kujizuia kisha unakuwa umemshinda pepo huyo.
Hili suala hata Equation x unaelewa

UZALENDO
Kutokuwa mzalendo kwa mpenzi wako. Jaribu kumpenda kwa kuwa ndiye uliyemchagua kuwa naye, kila siku Tanzania inasema watumishi wake wawe wazalendo, siyo wao tu hata mapenzi yanahitaji uzalendo wa hali ya juu. Uzalendo wa kupenda kitu chako, kumpenda mpenzi wako, mkeo, mumeo au mchumba wako.mkuu Analyse Lazima ujivunie, ujisifie kuwa naye kisha mthamini.

SUBIRA
Wapenzi kutokuwa na subira au uvumilivu; Hili nalo huchangia kwa kiasi kikubwa mapenzi ya mbali kuvunjika. Kama ilivyo subira ya kila mtu kuamini kuwa ipo siku ataondoka kwenye shida na ugumu wa maisha alio nao, basi Mzee wa kupambania amini na kuwa na subira au uvumilivu kwa mpenzi wako ili mfikie ndoto zenu.

MAZINGIRA
Jiepushe sana na mazingira ambayo yanaonekana kabisa yanaweza kukusababisha ukaingia kwenye uhusiano usio rasmi tena, pengine kwa mtu ambaye huna ndoto naye. Tatizo la kujiingiza kwenye uhusiano kwa sababu za kimazingira linaweza kukufanya ukajikuta umezama kwenye mahaba na mtu ambaye hana mapenzi na wewe na mwisho wa siku ukajikuta unaumia sana. Ukabaki kulaumu watu kama dronedrake


MAWASILIANO
Kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nayo huchangia sana kuvunjika kwa mapenzi ya mbali au kupoteza ladha, lakini kama mtu anakupenda kwa dhati, anakupenda tu, anaweza kukupigia simu na kukutumia SMS kibao, lakini akawa bado ni tatizo. Chunga sana mzee wa miongozo Smart911



TAMAA
Kama utaishi kwa kutamani vitu usivyokuwa na uwezo navyo ni dhahiri utajikuta unamsaliti mpenzi wako kwa kuwa tu uko mbali na unaona hawezi kukubana wala kukufuatilia. Ingawa ningekushauri ufanye kitu kwa kujiongoza na siyo kwa kuongozwa na tamaa au kwa kuwa mpenzi wako hayuko karibu nawe.


MKUMBO
Acha maisha ya kufuata mkumbo. Kama mwenzako amefanya kitu f’lani, basi eti na wewe unataka ukifanye au ukipate ili uonekane wa kisasa au mjanja. Kumbuka kuwa mwisho wa siku mtamaliza chuo na mengineyo, kila mtu atasambaa, kama uliharibu kwa mpenzi wako, mwenzio hatakuwepo tena na hapo ndipo utakapoanza kumangamanga na dunia

""Se.x is overrated play safe kama kijana usikubali kutafuta matatizo ambayo yataharibu bajeti yako ya maisha. Maana mtaji wetu sisi hustler ni afya ""'. fundi bishoo said
Kimwili haiwezekani au next to impossible,ila kiroho inawezekana,lazima muwe karibu sana na Mungu kwa maombi na sala kwani kitendo hicho ni sawa na kuingia vitani bila bunduki,hakunaga shetani anayeshindwa kirahisi hivyo...
 
Bila pesa hakuna cha uzalendo,subira,uaminifu wala nini....wanawake wa sasa angalau ukiwa na pesa atadumu na wewe hata kama hakupendi atapenda pesa zako!
 
Mapenzi ya mbali ni kupotezeana muda.
Ili kuepuka changamoto za kutengana na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali
 
Bila pesa hakuna cha uzalendo,subira,uaminifu wala nini....wanawake wa sasa angalau ukiwa na pesa atadumu na wewe hata kama hakupendi atapenda pesa zako!
Japo pesa inachangia kwa kiasi furani ilaa Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja.

Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara
 
Back
Top Bottom