Kama tunaamini katika vyama, CCM itatawala daima!

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Ikiwa tunaamini kuwa kiogozi fulani ni bora na atatuvusha kutoka A kwenda B Tunajidanganya!

Ikiwa tunaamini kwamba Chama fulani ndicho bora na kitatukomboa basini dhahiri kabisa
TUMEPOTOKA!

Ukombozi wa kweli utatokana na wananchi wenyewe watanzania na si vyama vya siasa hivi tulivyonavyo. Hivi vyama tulivyonavyo bado vina uasilia wa CCM kataeni ama kubalini huo ndio ukweli wenyewe.

Kama kuna mtu anaamini katika vyama basi na ajiulize mbona ndani ya vyama vyenyewe wanashindwa kukubaliana kutokubaliana? Kama wao wanajenga demokrasia kwanini wanajengena chuki na kutengana kwa mawazo yasiofanana? Je kwanini baadhi wanataka kuwafunika wengine waonekane wao ndio CHAMA chenyewe? Je vyama hivi vikiwa vina wenyewe kama ilivyo CCM ukombozi utatokea wapi!?

Ndugu zangu,
Tunapaswa kubadilika na kuitazama Tanzania tuitakayo, tunapaswa kutafakari vipi iwe Tanzania ijayo. Na ikiwa ndivyo hivyo basi tutambue ya kwamba kwa uhakika mpaka sasa hatuna chama hata kimoja (hivi tunavyoita vya upinzani) ambacho kipo kwa maslahi ya watanzania.

NI MVINYO ULE ULE KATIKA CHUPA MPYA!
 
Na katika nyongeza ya hayo.
Napenda kuwakumbusha jambo jingine... Tazameni kwa makini hao wanaopiga vita ufisadi hii leo. Wengi wao wana kashfa za ufisadi huko nyuma walikopita! (ni kama mwizi anapomkimbiza mwizi! ama akimkamata basi humpiga sana ili isijulikane kwamba naye alishiriki wizi) - nisinukuliwe vibaya hapo nimesema wengi wao si wote!

NASISITIZA TENA:

UKOMBOZI WA KWELI NI WA WANANCHI WENYEWE NA SI HIVI VYAMA VILIVYOUNDWA ILI TUSINYIMWE MISAADA NA WAFADHILI!!
 
...kilichotokea jana Arumeru Mashariki, Mwanza, Kiwira na Songea ndio jibu lenu!
 
Hii inatokana na ukweli kwamba, mtanzania ni mvivu wa kufikiri na mvivu wa kudai haki yake ya msingi. Ingekuwa nchi nyingine, serikali ya CCM ingeshaondolewa kwa sababu,

  1. Viongozi wake wanatuhumiwa kufanya biashara ya madawa kulevya lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya kuwalinda. Hadi wanajigamba kwamba wao ndio wenye nchi, watoto wao wanauza unga na hakuna wa kuwakamata
  2. Viongozi wa CCM wanakula rushwa, ni mafisadi wakubwa lakini hakuna wa kuwachukulia hatua yoyote, zaidi wanatetewa na masikini wa kutisha kwenye mitandao kama Ze macorpolo, Chama ritz etc….
  3. Sheria za Tanzania ni kwa ajili ya kuwalinda mafisadi na familia zao na kuwakandamiza raia masikini
  4. Viongozi wa CCM wanatuhumiwa kuficha fedha nyingi sana nje ya nchi lakini hakuna wa kuwachukulia hatua
  5. Viongozi wa CCM wanabaka watoto, wanawapa UKIMWI na hilo likawa tu ni upepo wa kupita
  6. Uspika na Bunge la Tanzania vimekuwa ni vilabu vya kupitisha na kulinda agenda za watawala wa CCM.
  7. Vyeo vya uongozi vinagawiwa kwa undugu, urafiki na ufuasi
  8. CCM itaendelea kutawala kwa sababu polisi wanawaua raia lakini hakuna wa kuwajibishwa, badala yake wanapandishwa vyeo
  9. CCM itaendelea kutawala kwa sababu ukibishana nao, either unauwawa, unamwagiwa tindikali, kung’olewa kucha au kupotea katika mazingira ya kutatanisha
  10. Huu ukoo wa panya umeweza kutupumbaza kwa kuwapa watoto wetu elimu duni ili waendelee kuwa wajinga wa kutaliwa
  11. Serikali ya CCM imeweza kuiuza nchi kwa wachina ambao wanaiba rasilimali zetu kwa kasi ya ajabu. Imefika hadi viongozi wao, kama balozi kuingilia mambo yetu ya kisiasa bila kuchukuliwa hatua.
  12. Serikali ya CCM imekaa kimya huku raia wa kichina wakitengeneza madawa ya kulevya kwenye majumba yetu wanayokodi huku wakilindwa na watawala
  13. Serikali yetu itaendelea kututawala kwa sababu, licha ya kwamba ajira ni tatizo nchini Tanzania, wafungwa wa kichina wanaletwa kufanya vibarua huku vijana wetu wakiwa kandoni mwa barabara wakiangalia
  14. CCM itaendelewa kuwa madarakani kwa miaka 300 kwa sababu wameweza kubuni namna ya kugawa vyama vya upinzani kuwatumia mamluki, wasaliti na watu ambao wameonyesha tamaa ya fedha na madaraka kwa kuwapa kiburi na yale yote mazuri wanayoyatamani mamluki hao
  15. Licha ya kwamba baadhi yetu, hatuwezi hata kujinunulia au kukodi sehemu ya maana ya kulala, tumeendekeza njaa zetu za pilau, Buku 7, tisheti tukifuraia kuwa neema kwetu huku mafisadi ya CCM yakichota mabilioni ya kodi na kuzipeleka nje kwenye akaunti zao.
  16. CCM itaendelewa kuwa madarakani kwa sababu Mahakama imekuwa ikilinda zaidi viongozi wa CCM na mafisadi wanaoua, kubaka, huku raia wanaobambambikiziwa kesi kusote kwa miaka 20 magereza bila kesi zao kusikilizwa
Hizi ni sababu tosha za CCM kuendelea kututawala kwa miaka 300 ijayo. hiyo imethibitishwa na Mbakajai Kapuya kwamba hao ndio wenye nchi na hakuna tunaloweza kufanya.

CCM hoyee !!!!!
 
Gharama ya ignorance
watz hawajiandikishi wala kupiga kura
hawajihusishi na issue zenye kuleta mustakabali wao na wa nchi
mtaani watu wanajipambanua kuwa kodi haziwahusu coz hawafanyi kazi au hawana biashara kubwa wanasahau wakipanda daladala,wakinywa soda na bia,wakivuta sigara wakilipia startimes,wakinunua nguo,wakipiga simu nk wanalipa KODI
Umaamumas huu unatuua
 
Ccm haiwezi kuondoka madarkani leo, kesho, wala kesho kutwa. Kwa sababu kinapendwa mno na watz
 
MAKADA WATANO CHADEMA KORTINI *Ni watuhumiwa wa tindikali Igunga 2011 *Waachiwa na kukamatwa, wapelekwa Tabora MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Igunga, wakituhumiwa kummwagia tindikali Musa Tesha mwaka 2002. Watuhumiwa hao, walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora jana, ambapo upande wa mashitaka uliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili mahakamani hapo, hivyo kuachiwa huru lakini walikamatwa tena hapo hapo na kurudishwa korokoroni. Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, mwendesha mashitaka wa polisi, Cosmas Mboya aliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili watuhumiwa hao kwa kutumia kifungu cha 98 (A) cha Sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1985, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kuhusu mwendesha mashitaka kufanya hivyo. Baada ya kuondoa shitaka hilo, Hakimu Milanzi alikubaliana na upande wa mashitaka na kusema kuwa, washitakiwa wako huru. Baada ya kufutiwa shitaka hilo, watuhumiwa walianza kutoka nje ya mahakama lakini ghafla walizingirwa na askari zaidi ya 40 waliokuwa wamesheheni silaha aina ya mabomu, bunduki na pingu ambao waliwakamata tena. Walifungwa pingu, kisha wakapakiwa ndani ya magari mawili ya polisi ambayo yaliondoka eneo la mahakama kwa kasi huku yakiwaacha wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani hapo katika mshangao. Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga (OCD), Abeid Maige aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa wamepelekwa Tabora kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka mengine mapya. Hata hivyo hakuyataja. Washitakiwa hao ni Evodius Justian (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage (36) mkazi wa Ndala mkoani Shinyanga, Rajabu Daniel (24) mkazi wa Singida na Seif Magesa (37) mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza. Wote walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili 12 mwaka huu, kwa kosa la kummwagia tindikali Mussa Tesha (26) mkazi wa Igunga Mjini, wakati wa kampeni za Uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka 2011. CHANZO: Mtanzania
 
Back
Top Bottom