Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,798
- 12,240
Tanzania tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi. Hili ni jambo jema ili kushirikisha watu wote katika maendeleo yetu. Lakini hatuwezi kupata maendeleo kama kila chama au kiongozi kuwa na sera yake ya maendeleo.
Mfano CCM imekuwa chama tawala tangu tupate uhuru lakini kila awamu imekuwa na sera yake na pia kila kiongozi amekuwa na sera yake mbali na sera ya chama. Hii ni changamoto kubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo au kuendeleza nchi.
Katika awamu ya tatu CCM ilikuwa na sera yake lakini pia Rais Mkapa alikuwa na sera yake. Hivyo kwa miaka 10 ya utawala wa Rais Mkapa serikali ilikuwa inatekeleza sera ya CCM na ahadi za Mkapa wakati wa kampeni. Awamu ya nne ya Rais Kikwete hali ilikuwa hiyo hiyo. Katika awamu hiyo kwa mfano tuliaminishwa tutatumia umeme wa gesi, lakini ilivyokuja awamu ya tano ya Rais Magufuli alitupilia mbali umeme wa gesi na badala yake akaja na umeme wa maji wa bwawa la Nyerere. Awamu ya sita ya Rais Samia iko njia panda haijui ifuate umeme wa maji au wa gesi.
Sasa utaratibu huu hauwezi kutuletea maendeleo badala yake tutakuwa tunakwenda mbele na kurudi nyuma. Hivyo mabadiliko yanahitajika kama kweli tunataka kusonga mbele kimaendeleo. Tunatakiwa kuwa na sera moja ya maendeleo ya Taifa. Sera ambayo itafuatwa na vyama vyote vya siasa na viongozi wote tutakaowapata. Vyama vya siasa na viongozi washindane katika kutengeneza mikakati ya utekelezaji (Strategies). Siyo kila chama kiwe na sera yake na viongozi wawe na ahadi zao tofauti na sera ya Taifa. Sisi wananchi tutakuwa na kazi nyepesi ya kuangalia, kupima na kuchagua mkakati upi ni bora na inatekelezeka kirahisi katika mazingira yetu. Pia wananchi tutakuwa na kazi ya kuchagua ni kiongozi yupi anauwezo mkubwa zaidi wa kutekeleza mkakati wa chama chake.
Nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kutuletea maendeleo vinginevyo tutasota kwa muda mrefu kama Taifa.