Kama sielewi elewi vile!


Aiseee; tupo tofauti sana hadi michuchumio tena!
 
Duh yaani msiba wa kakake kabisa . Ama kweli kuishi kwingi kuona mengi na mjini kuna mengi . Unajua nilipokua nasoma huu uzi nilidhani mwisho itaishia alikua anatania kumbe ni msiba tena wa ndani. Kweli maendeleo ya sayansi na teknolojia. Sasa hawa wanetu enzi zao sijui zitakuaje manake sipati picha.
 
mi mwenyewe nilipata ganzi......
wala siyo kisa cha kutunga wala ku-wish cc. EMT
yametokea kweli kabisaaaaaa, na ni kaka wa baba na mama mmoja.....
hiyo ndo habari ya mujini
 
Last edited by a moderator:
hata kama hajaacha watoto, au kawaacha na mali zao, tunacholilia ni kuondokewa na huyu ndugu..... mama sijui naye alikuwa amepetukia wapi (cc. moto2012, snowhite, Kipipi ) ila katika zile simu alikuwa ana-organize pia mavazi ya mama
Kweli binadamu tunatofautiana! Mi hata kama kuna sale ya khanga, sidhani kama nitanyanyuka kwenda dukani.
 
Last edited by a moderator:
Kweli binadamu tunatofautiana! Mi hata kama kuna sale ya khanga, sidhani kama nitanyanyuka kwenda dukani.
wangoni haya bado hayajatukuta.......
utafanyia wapi kule mpitimbi?
kanga utaletewa mdogo wangu
 
ukitaka uufaidi huu uzi chukua time kuupitia
but juukwajuu lazima utaona kama mnaonewa tu.

 
nilienda kwenye msiba wa baba wa rafiki nikakuta mama anaburudika na muziki wa Yesu, hii ilikuwa kidini zaidi..... hakuna kulia ni kuburudika tu kuwa kaenda kwa Baba..... nilijishangalia, lol!

marangu kwa mara nyingine, msiba wa baba ya rafiki yangu/mwanachama mwenzangu, nipo nae kwenye kikundi, hii nayo ilikuwa funga kazi,tumetoka KCMC kuchukua mwili tukisindikizwa na tarumbeta, pale home kuna mahema ya kutosha, msiba unafatiliwa kwa njia ya projector, kila hema lilikuwa na meza kubwa ya kila aina ya vinywaji, bufee zilikuwa za kutosha, tumefika nyumbani MC anatuongoza kwa kwaya tu,(tenzi za rohoni hazina nafasi siku hizi) tuliimba kichaga kidogo wakati wakienda kuzika,makaburini walienda familia/ndugu wa karibu sana, wengine tuliendelea kufatilia na projector huku wahudumu wakiwasikiliza mnatumia vinywaji gani,rafiki yetu huyo anawatuma wahudumu "unaowana walee waliovaa sare za purple ni kikundi changu cha arusha, kuna wanaokunywa ballantin, amarula, savannah wasikilizwe kila mmoja anachotumia apatiwe", tumemaliza msiba rafiki yetu karudi arusha tumeenda kumpa pole akatuambia msiba ulitumia 22mil.
 
Undugu wa siku hizi umebaki kuwa ni indentity tu.Nikupe mfano halisi huyu mama amebahatika kupata watoto sita.Inafikia hatua huyu mama anaishiwa nguvu na anaumwa sana.

Kati ya watoto hawa,ni watoto watatu tu wenye kuonesha kujali hali ya mama yao,na bahati mbaya uwezo wao wa kifedha ni mdogo.Ugonjwa aliougua mama yao waweza kutibika pengine kwenye referal hospitals,ndugu hawa hawaoneshi kumuhangaikia mama yao inavyostahili.Hatimaye siku inafika mama anafariki.

Wakati wa msiba umoja unaooneshwa na ndugu hawa ni wa kushangaza,kwa mara ya kwanza wanakutana na kujadiliana kuhusu mazishi ya mama yao 'kipenzi".

Bajeti kubwa ya mamilioni inapitishwa,sare zinashonwa,spika kubwa na Dj mzoefu vinakodishwa na chakula cha kila aina kipo msibani.

Nikija kwenye uzi ulioletwa hapa,kuna mawili,huyo dada inawezekana kwa upande mmoja anawakilisha familia ambazo hazijaliani,undugu isn't a big deal,na kwa vyovyote kujirembua nk ni maandalizi ya ufahari utakaoenda kuoneshwa msibani.

Kwa upande wa pili huyu dada pengine anaonesha true colour yake kwa misingi ya kwamba mahusiano yake na huyo kaka ambaye ni marehemu tangu mwanzo hayakuwa mazuri,hii inaweza kuwa inachangiwa na sababu nyingi zikiwemo tofauti za wazazi,kosa la marehemu nk

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
juzi juzi kuna rafki yangu wa kike kafiwa na mumewe,basi ikawa tupo kanisani katika kuaga,lakini nikaona kama ndugu wa mume wanamtenga hv? nikauliza rafki yetu mwingine ndo akanipa mkasa,kumbe yule dada jana yake alikaa chumbani akajishonea hilo sijui weaving akajiremba sasa ndugu wa mume wakakasirika kweli,yaani mwenzio kafa hata kuzikwa hajazikwa we unajiremba....wameenda kuzika mkoani,lazima kutakua na shida sana huko. lakini watu hawana upendo wa kweli nowdays.
 
ahahahhah dada langu bana!
si ajabu ulianza kulia hapo!
hii ndo daslam bana!
we unadhani wote hawaogi siku tatu kama kule kumpitimbi?
NAJUA ULIVYOSTUKA dada wa mimi!
lakini ndo hivo tena!pooole mpenzi kuanzia leo naanza kuongozana na wewe kokote wasije wakaniulia dadangu bure kwa presha!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…