Kama siasa ni maisha, basi katiba ni document ya kisiasa juu ya mgawanyo wa madaraka na utowaji haki

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Enyi wanasheria mnioneshe ibara yoyote kwenye katiba yetu ya 1977 inayoelezea wajibu, haki na madaraka ya mkulima/ mfugaji katika kumiliki ardhi, kulima/ kufuga na kupata masoko.

Au nionesheni ibara inayoonesha haki, wajibu na madaraka ya mfanyabiashara ktk kupata soko, kupanga bei ya bidhaa, kupanga malipo ya kodi (TRA) na tozo nyingine.

Kwenye katiba kuna maelezo ya jumla jumla kuhusu haki za kiraia, kisiasa na zile binadamu. Ambazo akizipata mwanasiasa hata mm mkulima/ mfugaji/ mvuvi nitakuwa nimezipata.

Kwa mantiki hiyo katiba imetawaliwa na masuala ya kisiasa kwa asilimia kubwa. Inaongelea kwa marefu na mapana mgawanyo wa mamlaka/ madaraka, namna ya kuyapata, sifa za kuyapata pamoja na muda wa kukaa mamlakani.

Kwa ufufanuzi huo basi, nionavyo mm ni kwamba wanasiasa ni watu sahihi wa kuuteka mchakato wa kupata katiba mpya.

Lakini pia Rais Samia anajichanganya. Mbona kwenye kikosi kazi hakuwahusisha wakulima na wafuagaji?? Je, waliwakilishwa na akina prof. Mukandala? Au aliwapuuza na kuona hawana umuhimu?

Katiba ni sasa kwasabb wadau na wahusika wakubwa wa katiba (wanasiasa ) wanalalamikia katiba iliyopo (1977). Miaka 3 ya elimu kwa wananchi haikubaliki.
 
.Kwa mantiki hiyo katiba imetawaliwa na masuala ya kisiasa kwa asilimia kubwa. Inaongelea kwa marefu na mapana mgawanyo wa mamlaka/ madaraka, namna ya kuyapata, sifa za kuyapata pamoja na muda wa kukaa mamlakani.

Kwa ufufanuzi huo basi, nionavyo mm ni kwamba wanasiasa ni watu sahihi wa kuuteka mchakato wa kupata katiba mpya.
Karibu pande hizi Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
Baada ya kikosi kazi, sasa itaundwa kamati ambayo itashirikisha watu wa kada mbalimbali.
P
 
Back
Top Bottom