Kama ningekuwa Rais Zanzibar vipi ningetatua matatizo ya Muungano. Ni mambo Matatu...

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
662
1,000
1) Tukumbuke Mwalimu Julias Kambarage Nyerere alisema sitawapiga Mabomu Wazanzibari wakikataa Muungano haki hio tunayo.

Kama Rais Naamrisha Wabunge wote Wa Zanzibar ikiwa CCM au CUF ACT. Kutoka Bungeni Kurudi Zanzibar.

2) Nikiwa kama Rais wa Zanzibar Nasitisha Shughuli zote za Kimuungano kwa Zanzibar. Mpaka yatekelezwe matakwa ya Makubaliano. Hamtaniunga mkono.?

3) Nikiwa Rais ni lazima Wabunge na Wawakilishi wote wa Zanzibar wa vyama vyote kukutana na kujadiliana kila linalokwenda Bungeni kabla .

Tufanye maamuzi kwa pamoja ya Zanzibar .

Kama alivyowahi kusema Marehemu Dkt Omar Ali Juma .
alipowaita Wabunge na wawakilishi ukumbi wa Abdulwakil.

Dkt Omar .Akawambia Semeni kwa Pamoja mie kama makamo wa Rais sina Sauti. Je atakua nayo Mh Samia.

4) Kwa kuwa tuna Kila sababu ya utatuzi kama sikufanya hivyo Wazanzibari Hamjamjua Mchawi .

Mwisho Katiba yetu inatupa Haki ya Kura ya Maoni kwa jambo lolote kwa Zanzibar.

Natoa hoja Kwa wananchi wa Wazanzibar akiwa Mtu chama chochote. Au Raia wa kawaida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom