Kama Nikifa leo hii 31/12/2013

Kama Nikifa leo hii 31/12/2013

kwa wana jf wote
cc: invisible paw na wengineo

kama nitakufa leo, nisiuone mwaka mpwa 2014, kama nitaanguka leo hii macho yangu yakafumba nisiione tena kesho, kama nitakufa leo hii, yaani nisiione tena jf, nisiwaone na kuchati na mmu members, chitchat heroes yaani kama nitakufa leo hii.

Najua nitakwenda mbinguni, kule watu waendako wasirudi tena, nitaendelea kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapenda. Nitawaombea ritz na chamviga wapunguze visasi dhidi ya chadema ntaowambea cathode ray arudi jukwaani maana tangu afunge ndoa ndio kaifunga na jf, nitamuombea zumbemkuu apunguze lugha ya ukali dhidi ya ccm. Nitawaombe mabinti wote wa jf na akina kaka wanaotafuta wachumba, kuwa kwa neema ya mungu wakapate kujibiwa haja ya mioyo yao.

Kama nitakufa leo, nisiione jf nitawaombea wale wote wenye chuki binafsi na moderators, nitaiombea jf iendelee na kudumu milele hadi ile siku ya ukombozi itakapofika. Kama nitakufa leo, yaani nisiwepo tena nitamkumbuka mama mchungaji mamndenyi kwa kuwa na misimamo thabiti ya kile anachokiamini lakini kama ni lazima leo hii uhai wangu unitoke basi sitaacha kuimba shairi la inside verossa kwa ajili ya mpwa wangu mpendwa mentor

nitaendelea kuwaombea ikiwa ni lazima nife leo, yaani pumzi na mapigo yangu ya moyo yakisimama leo hivi nitamkumbusha mpwa wangu mani aendelee kutoa nasaha na kuwakusanya group members hata pale ambapo ilibidi kutumia busara na gharama zake binafsi, nitamuombea kwa mungu amuongezee busara hasa katika kumshauri mohamedi mtoi na harakati zake za ukombozi.

Kama roho yangu itauacha mwili wangu leo hii yaani sasa hivi, nitamuombea sana mzee mwenzangu mtambuzi aendelee kuandika makala zake nzuri na tamu na kama sitabahatika kuisoma ile hadithi anayoiandaa inayohusu tanga basi nitamuomba aiweke kwa namna ambayo itawaonya na kuwakumbusha yale mema niliyotenda au kuwahi kutenda.


Lakini kama sitaiona kesho yaani kesho itakapofika isinikute basi namuomba mpwa wangu baba v aongeze ukali kwenye jukwaa la mmu na sometimes aongeze nguvu kwenye chitchat ambako utoto, uhuni na umalaya vinakithiri, yaani jukwaa liwe ni kwa ajili ya kuelimishana na sio kufundishana na kusifiana ujinga,

yaani kama kesho hiyo damu yangu itasimama itakapokataaa kuendelea kuzunguka mwilini tena, hapo moyo wangu utakaposimama na mapigo ya mwili kutoweka nitaomba sana aine paloma ladyfurahia tinna cute smile na heaven on earth wabadilike na kuwa wadada wazuri wenye kuelemisha jukwaa, nitaomba kitu kimoja toka kwenu endapo itabidi nife leo, mtafuteni little angel maana ameliasi jukwaa, seems whatsup imempoteza. Nawapenda dada zangu

nitaomba kabla ya kuupumzisha mwili wangu kwenye nyumba yangu ya milele, nitaomba hili tu na mara hii msikatae, pale mtakapokuwa mmenizunguka kuniaga huku mkibubujikwa na machozi ya furaha na simanzi huku kokutona akiwa amebeba shada la maua dhidi ya elli nawaombeni na ninawakumbusha kunifanyia hili kwa ajili yangu na yenu, yasomeni yale maandiko yangu yote, ukiianza na lile la kwanza hadi lile la mwisho, mkajililie nafsi zenu maana wakati huo nitakua siwasikii tena, nitakuwa nimepumzika kwa amni, vita nitakuwa nimeimaliza.

Kawalilieni watoto wenu na watoto wa watoto wenu maana hapo katiba mpya itakapokuwa imefika, mbichi na mbivu zitajulikana na hakika hakutakua na kitu kitakacho achwa gizani kisiwekwe hadharani, hakuna dhambi itakoykuwa imefanyika sirni isionekane pale wapwa zangu nape nnauye na mwigulu nchemba watakapotubu watakapoyarudia mavumbi maana sisi sote tu mavumbi na mavumbini tutarejea. Kawakumbusheni hao wazililie nafsi zao maana hakika mbele za mola hakuna kinyonge kitakachoionja ahera wala pepo ya mwenyezi mungu

siku ile mkiwa mnaniaga, nikiwa ndani ya jeneza lile, najua unaniona najua machozi yanakutoka, ninakuona unavyoumia na kukiwaza kifo sijui jeneza langu litakuwa limiwekwa pale sitting room kwangu au pale nje chini ya ule mti huku jua kali likiwaka. Mmh najua unaniona usilie mpwa.

Lakini mimi kama nitakufa nisiione kesho nitafanya hayo, je wewe tutakukumbuka kwa yepi? Mungu wangu awabariki na kuwapigania katika mapito yenu, ktika shida ya moyo wako ukapokee haja ya moyo wako, ukajibiwe shida yako siku ya taabu yako kuu. Pale unapokuwa umeshindwa kabisa basi hapo msaada mkubwa na wa ajabu ukaonekane, unaetafuta kazi basi ukapate kazi, unaetafuta mke/mume basi mungu akujibu haja ya moyo wako huo, unataka kujenga maana umechoka kukaa nyumba za kupanga, basi mungu aliyehai akapate kukujibu, huna kodi ya nyumba au ada za watoto ni wakati wa mungu sasa kujibu maombi yako, akaponye ndoa yako, wazazi wako waponywe na familia yako sasa.

Tulianza mwaka na mungu na ni kwa neema yake tu tumefika hadi leo hii, barikiwa sana, tulipitishwa katika mengi, tulifika mahali ndoa zetu zikawa za moto na kazini nako kwa moto tukakosa pa kwenda, lakini mungu alikua kwetu, tuliumwa sana hata wengine wakakata tamaa juu ya uhai wetu, lakini mungu alikua muaminifu leo tena tuwazima, alitukinga na ajali wakati wenzetu wanakufa sisi tulitoka tukiwa salama, sio kwamba tumetenda mema sana ni kwa upendo wake allah hatustahili chochote sisi.

Je unani wewe badala ya kumshukuru mungu wako leo unakuwa na mwazo ya kwenda kulewa, ngono na mengine mabaya? Uwepo wetu jf uwe fundisho na maadili kwa maisha yetu na wala sio chanzo cha sisi kutenda dhambi. Na mungu wangu ninaemwamini atatuvusha na mwaka ujao ili tukawaone watoto na watoto wa watoto wetu. kumbuka kutubu na kusamehe

heri ya mwaka mpya 2014

ashukuriwe mungu nimeuona mwaka 2014. Asanteni kwa maombi yenu. Nami sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya mungu
kyan kyanakyomuhaya mungu ni mwema
kumbukakurekebisha screentouch za huko nisiteseke duniano na mbinguni pia
 
Unajichulia eeeee mi nataka ukifa unipe tu hiyo simu na ile saa etiii
 
Kwa Wana JF wote
CC: Invisible Paw na wengineo

Kama nitakufa leo, nisiuone mwaka Mpwa 2014, kama nitaanguka leo hii macho yangu yakafumba nisiione tena kesho, kama nitakufa leo hii, yaani nisiione tena JF, nisiwaone na kuchati na MMU members, Chitchat Heroes yaani kama nitakufa leo hii.

Najua nitakwenda Mbinguni, kule watu waendako wasirudi tena, nitaendelea kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapenda. Nitawaombea Ritz na CHAMVIGA wapunguze visasi dhidi ya Chadema ntaowambea cathode ray arudi jukwaani maana tangu afunge ndoa ndio kaifunga na JF, Nitamuombea zumbemkuu apunguze lugha ya ukali dhidi ya CCM. Nitawaombe mabinti wote wa JF na akina Kaka wanaotafuta wachumba, Kuwa kwa NEEMA ya MUNGU wakapate kujibiwa haja ya mioyo yao.

Kama nitakufa leo, nisiione JF nitawaombea wale wote wenye chuki binafsi na Moderators, nitaiombea JF iendelee na kudumu Milele hadi ile siku ya ukombozi itakapofika. Kama nitakufa leo, yaani nisiwepo tena nitamkumbuka Mama Mchungaji Mamndenyi kwa kuwa na misimamo thabiti ya kile anachokiamini lakini kama ni lazima leo hii uhai wangu unitoke basi sitaacha kuimba shairi la Inside Verossa kwa ajili ya Mpwa wangu mpendwa Mentor

Nitaendelea kuwaombea ikiwa ni lazima nife leo, yaani pumzi na mapigo yangu ya moyo yakisimama leo hivi nitamkumbusha Mpwa wangu MANI aendelee kutoa nasaha na kuwakusanya group members hata pale ambapo ilibidi kutumia busara na gharama zake binafsi, nitamuombea kwa MUNGU amuongezee busara hasa katika kumshauri Mohamedi Mtoi na harakati zake za ukombozi.

Kama roho yangu itauacha mwili wangu leo hii yaani sasa hivi, nitamuombea sana Mzee mwenzangu Mtambuzi aendelee kuandika makala zake nzuri na tamu na kama sitabahatika kuisoma ile hadithi anayoiandaa inayohusu Tanga basi nitamuomba aiweke kwa namna ambayo itawaonya na kuwakumbusha yale mema niliyotenda au kuwahi kutenda.


Lakini kama sitaiona kesho yaani kesho itakapofika isinikute basi namuomba Mpwa wangu Baba V aongeze ukali kwenye jukwaa la MMU na sometimes aongeze nguvu kwenye Chitchat ambako utoto, uhuni na umalaya vinakithiri, yaani jukwaa liwe ni kwa ajili ya kuelimishana na sio kufundishana na kusifiana ujinga,

Yaani kama kesho hiyo DAMU yangu itasimama itakapokataaa kuendelea kuzunguka mwilini tena, hapo Moyo wangu utakaposimama na mapigo ya mwili kutoweka nitaomba sana Aine Paloma ladyfurahia tinna cute Smile na Heaven on Earth wabadilike na kuwa wadada wazuri wenye kuelemisha jukwaa, nitaomba kitu kimoja toka kwenu endapo itabidi nife leo, mtafuteni Little Angel maana ameliasi jukwaa, seems Whatsup imempoteza. Nawapenda dada zangu

Nitaomba kabla ya kuupumzisha mwili wangu kwenye nyumba yangu ya milele, nitaomba hili tu na mara hii msikatae, pale mtakapokuwa mmenizunguka kuniaga huku mkibubujikwa na machozi ya furaha na simanzi huku KOKUTONA akiwa amebeba shada la maua dhidi ya Elli nawaombeni na ninawakumbusha kunifanyia hili kwa ajili yangu na yenu, Yasomeni yale maandiko yangu yote, ukiianza na lile la kwanza hadi lile la mwisho, mkajililie nafsi zenu maana wakati huo nitakua siwasikii tena, nitakuwa nimepumzika kwa amni, VITA nitakuwa nimeimaliza.

Kawalilieni watoto wenu na watoto wa watoto wenu maana hapo KATIBA mpya itakapokuwa imefika, mbichi na mbivu zitajulikana na hakika hakutakua na kitu kitakacho achwa gizani kisiwekwe hadharani, hakuna dhambi itakoykuwa imefanyika sirni isionekane Pale Wapwa zangu Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba watakapotubu watakapoyarudia mavumbi maana sisi sote tu mavumbi na mavumbini tutarejea. Kawakumbusheni hao wazililie nafsi zao maana hakika mbele za mola hakuna kinyonge kitakachoionja AHERA wala PEPO ya mwenyezi MUNGU

Siku ile mkiwa mnaniaga, nikiwa ndani ya Jeneza lile, najua unaniona najua machozi yanakutoka, ninakuona unavyoumia na kukiwaza kifo sijui JENEZA langu litakuwa limiwekwa pale sitting room kwangu au pale nje chini ya ule mti huku jua kali likiwaka. Mmh najua unaniona usilie Mpwa.

Lakini mimi kama nitakufa nisiione kesho nitafanya hayo, je wewe tutakukumbuka kwa yepi? MUNGU wangu awabariki na kuwapigania katika mapito yenu, ktika shida ya moyo wako ukapokee haja ya moyo wako, ukajibiwe shida yako siku ya taabu yako kuu. Pale unapokuwa umeshindwa kabisa basi hapo msaada mkubwa na wa ajabu ukaonekane, unaetafuta KAZI basi ukapate kazi, Unaetafuta Mke/MUME basi MUNGU akujibu haja ya moyo wako huo, unataka kujenga maana umechoka kukaa nyumba za Kupanga, BASI MUNGU aliyehai akapate kukujibu, Huna kodi ya nyumba au ada za watoto NI wakati wa MUNGU sasa kujibu maombi yako, akaponye NDOA yako, Wazazi wako waponywe na familia yako sasa.

Tulianza mwaka na MUNGU na ni kwa NEEMA yake tu tumefika hadi leo hii, barikiwa sana, tulipitishwa katika mengi, tulifika mahali NDOA zetu zikawa za moto na kazini nako kwa MOTO tukakosa pa kwenda, lakini MUNGU alikua kwetu, tuliumwa sana hata wengine wakakata tamaa juu ya uhai wetu, lakini MUNGU alikua muaminifu leo tena tuwazima, alitukinga na AJALI wakati wenzetu wanakufa sisi tulitoka tukiwa salama, sio kwamba tumetenda MEMA sana ni kwa upendo wake ALLAH hatustahili chochote sisi.

Je unani wewe badala ya kumshukuru MUNGU wako leo unakuwa na mwazo ya kwenda kulewa, ngono na mengine mabaya? Uwepo wetu JF uwe fundisho na maadili kwa maisha yetu na wala sio chanzo cha sisi kutenda dhambi. na MUNGU wangu ninaemwamini atatuvusha na Mwaka Ujao ili tukawaone watoto na watoto wa watoto wetu. Kumbuka kutubu na kusamehe

Heri ya mwaka Mpya 2014

ASHUKURIWE MUNGU NIMEUONA MWAKA 2014. ASANTENI KWA MAOMBI YENU. NAMI SITAKUFA BALI NITAISHI ILI NIYASIMULIE MATENDO MAKUU YA MUNGU
kyan kyanaKyoMuhaya Mungu ni mwema
R.I.P Mtoi
 
aaah acha kabisa, he was my best friend aiseeeee
Kabla sijajiunga na JF nilimjua tu pale alipotutupa mkono na kurejea kwa muumba wake, maana nilikuwa sifuatilii Siasa kipindi hicho ndio maana nilikawia kumfahamu.

Wakati nipo hapa JF nikawa nafukua makaburi mara nikaona huyu member nikaangali na nyuzi zake, kiukweli alikuwa ni mtu mwenye sifa zake ambazo wewe ndio unazijua vizuri.

R.I.P Mtoi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom