Kama ni ndoto, mbona haiishi?

Ok, wakati naandika nilikuwa naishiwa hata nguvu ya kuendelea, lakini sababu niliishaamua kuitoa sikuweza kuacha. Kwa hiyo, kilichokuwa hewani ni kuandika na siyo mpangilio. Sorry for that.

I can feel now like you. Can I say something?? Let me do this................PM
 
pole sana mkubwa. Kupoteza ubavu ambao mlishibana kila idara ni pigo kubwa mno. Yahitaji mkono wa Mungu kuvuka. Wish it waz just a dream
 
Pole sana ni wakati mgumu inahuzunisha sana napenda kukwambia Mungu yupo pamoja nawe mwombe sana atakuondoa kwenye hiyo ndoto kwa uwezo wetu hatuwezi bala kwa kumtumainia yeye. MUNGU WETU NI MUNGU WA FARAJA WA MATUMAINI NA WAMAPENDO

Bwana alitoa na Bwana ametwa jina la bwana na lihimidiwe
 
Pole kaka. Mshukuru Mungu kwani kwa Mujibu wa jirani wa mgonjwa, mgonjwa alitubu.kwa imani yupo mbinguni kwa mungu.siku1 utamwona tena.
ila na wewe andaa jia nzuri kufika huko.
Pole mkuu, Mungu akupe maisha mengine mapya.
 
Mkuu Mestod, Kwanza pole sana kwa masaibu mazito yaliyokufika. Japokuwa haijanitokea lakini ninaamini inaumiza sana. M'mungu akupe nguvu na kukuongoza bro. Pili naomba nitofautiane na wale waliosema kuwa ni ndefu, kwa kweli mi sioni kama ndefu sana, kwani inatumia muda gani kuisoma jamani??!!! Yaani leo ndiyo nimeamini kuwa watanzania ni wavivu sana wa kusoma. Yaani watu wanataka sredi yenye mistari miwili au mitatu.........inasikitisha sana.

Wito: Tujitahidi kuwazoesha hata watoto wetu tu tabia ya kupenda kusoma maana inaonekana sisi wenyewe imetushinda.
 
Yah, ni kweli. I lost her on 18th, and buried her on 21st Jan. Hii ni sehemu ndogo sana ya mwisho, ila ni mengi yalitokea hadi namzika na hadi leo siamini kama kweli kafariki. Ni kweli kabisa.

Pole sana mkuu....Mungu azidi kukupa nguvu!
 
pole sana mkuu,kumpoteza mtu unayempenda inauma sana,hata mimi nina hiyo ndoto isiyoisha toka nilipompoteza baba mzazi ghafla.
 
Pole bwana inaumaaa inatia uchungu sana.vp hukua na mtoto nae?pole mkulu
 
pole sana mkuu, nimeona ni jinsi gani ulivyoweweseka that nite, ubavu wako kuondoka sio mchezo, pole sana
 
Doooh, mkuu nimeisoma na kwa kweli inahuzunisha sana.
Pole sana Ndugu.
Kazi ya Mola hiyo, nasi tumshukuru kwa kila jambo.
 
No, hatukuwa na mtoto, bali ndo tulikuwa kwenye process za harusi June this year. Wazazi pande zote walishatoa baraka zao.
 
Pole sana kaka angu!!! Mungu ampe raha ya milele na Mwanga wa milele umwangazie.
Kaka yangu mpendwa tukumbuke kwamba sisi hapa ni wasafari na wapitaji tu. Hayo ndio tulioandikiwa sisi wanadamu.

Tulia tu Mungu atakupa mke mwingine mwema kabisa. Ni kweli kwamba ni ngumu kuisahau lkn pia yatupasa tuyapokee na kuyakubali, kwa sababu yapo juu kabisa ya uwezo wetu!!!

Mungu akutie nguvu na akupiganie siku zote za maisha yako.
 
No, hatukuwa na mtoto, bali ndo tulikuwa kwenye process za harusi June this year. Wazazi pande zote walishatoa baraka zao.

Njia za Mungu sio kama njia zetu, na wala mawazo yake sio kama mawazo yetu. Jipe moyo ktk Mungu, tulia kabisa jua hakika Mungu anakuwazia mawazo ya amani. Mshukuru kwa yote, yeye anajua mwanzo na mwisho wetu kuliko sisi tujuavyo.

Najua lazima uliomba sana apone, ulifanya juhudi kubwa kuokoa maisha yake, lakini huo ndio uliokuwa mpango wa Mungu. Mshukuru kwa yote, mwombe akupe Neema na nguvu ya kusonga mbele!!!

Be happy my dear,hatuwezi kushindana na kazi ya Mungu.
 
Back
Top Bottom