Kama ni ndoto, mbona haiishi?

Haya mambo ya kutoana machozi asubuhi si mazuri mkuu.

Pole sana mungu akupe nguvu
 
Kaka!
ndivyo inavyotokea pale tunapowapoteza wapendwa wetu,mawazo yetu yan ndani huwa hayataki kuamini na huwa tunatamani iwe tofauti na ilivyo,inauma sana.

Ila Mungu ni muweza wa yote weka kila kitu kwake naye atakupa nguvu na imani kuweza kuyakubali hayo yaliyotokea na kuendelea na maisha,kwa nguvu zetu wenyewe mengi hayawezekani ila kwa nguvu zake Manani yote yanawezekana,amini sote tutakutana nae tena Sayuni kwenye siku ilee ya mwisho.

Pole kaka.
 
Mungu amlaze mahalipema peponi Amin. naakupe afuwan inshaalaah. kisahiki kimeniliza sana nahizi uchungu mpaka sasa. pole sana mkuu mungu kampenda zaidi


Ni saa sita na dk hamsini na moja usiku. Nimejiegesha kupata usingzi wa mang'amung'amu baada ya uchovu na mawazo mengi, simu nimeishika. Mara simu ina vibrate na kutoa mlio. Nashituka na kuona screen imeandika 'wife calling.....' 'Hallow', naitika. 'Wewe, umelala?', unanijibu. 'Hapana, nimejiegesha si unajua usingizi hauji?' (kwani nakumbuka mara ya mwisho nimeangalia saa ilikuwa saa sita na nusu), nakujibu na unanambia unajua. Unaanza kunambia njaa inakuuma sana na hauna nguvu, huna nguvu na hata manesi unawaita hawaji. Nafarijika kuona atleast unapata apettite ya kula na nakusihi uvumilie na kukuambia si unajua manesi wetu walivyo hasa hapo muhimbili? Nakusihi umuombe jirani yako ambaye kidogo ana nguvu akusaidie.

Unanambia huna nguvu nami nakuambia najua sababu toka umeanza kuumwa ni zaidi ya mwezi huli vizuri na ukila unatapika chakula chote. Unanambia kesho uje saa kumi na mbili kuninywesha uji. Nakuambia usijali mpenzi, nitakuja. Mara unanambia kata simu nguvu inaisha piga baadaye kidogo. Nakata bila kujibu lolote na nahisi kuchanganyikiwa. Naangalia call duration tumeongea kama dk 1.01. Nakaa kama dk kumi napiga tena. unapokea na kunishukuru kwa kukusaidia, nikakuambia usijali mama, Mungu atakuponya. Bado unasisitiza kuhusu kuwahi kukunywesha uji kesho nakuambua sawa, mara unanambia kata simu nguvu imeisha nakata simu. Naangalia call duration, tumeongea dk 2.02.

Nakaa macho na mara ya mwisho naangalia saa ni saa tisa unusu usiku. Nikiwa usingizini naota nikisema 'Mungu mponye, Mungu mponye....' huku machozi yanatoka. Nashituka na kuona ninatoa machozi kweli. Naangalia saa na kujiuliza ni nini hii? Ni saa kumi na dk 35. Naamua kuamka na kujiandaa ili nije kukunywesha uji. Natoka nyumbani saa kumi na moja unusu. Nikiwa mzunguko wa uhuru kariakoo, kaka yako anapiga simu ananambia, 'mzee, dada ameshatucha, amefariki aisee'. Nahisi kuchanganyikiwa, mbele sioni. Nafika sewahaji namba 10. Naona nesi anampa vitu vyako kaka kwenye mfuko wa plastic wa kijani. Naenda kitandani naona umefunikwa gubi gubi na wamezungushia mashuka ya kijani. Duh, kijani tena. Namkuta jirani yako, ananambia, pole kaka, muone huyo hapo. Nafunua shuka, nashika paji la uso, umeshapoa mpenzi umekuwa wa baridi. Nashika paji la uso wako, machozi yangu yanaanguka juu ya paji la uso wako. Nakuuliza 'd, huu ndo uji uliosema niwahi kukunywesha? Zile shukrani kumbe ndo Muumba alikuwa anakuita?' nakufunika na kutoka.

Jirani yako ananambia, 'kaka mwache mwenzio apumzike kwani alikuwa anaishi kwa mateso sana'. Namuuliza 'ilikuwaje usiku wa leo'? Akanambia aliongea na simu kama mara mbili hivi baadaye alisema, "MUNGU NAOMBA UNICHUKUE, LAKINI KABLA HUJANICHUKUWA NISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE". Akanambia ulirudia mara nyingi na baadaye kati ya saa kumi na saa kumi na moja ukatulia.

Mpenzi, yote yaliyotokea hata siamini, ni kama ndoto, kwamba haupo nami.
Lakini kama ni ndoto, mbona siamki? Inamaana ndoto hii naota tuu, toka January mpenzi? Kama ni ndoto mbona naenda kazini? Ishu zinazotokea mbona naziona na kuzisikia? Mabomu Gongo la Mboto, Babu Loliondo na kero zingine?

Maisha kwangu sasa ni taabu sana ni kama jana tuu, matukio yote yametokea. Sikuamini pale uliposhushwa kwenye nyumba yako nyingine na ya milele, mrembo wangu. Nakukumbuka sana mpenzi. Comitment zako za dhati, uaminifu, ucheshi, my dia. RIP MY SWEET MAMAA!
 
Ndugu yangu, naomba kukutia nguvu, ni ngumu na haisahauliki ila mgeukie MUNGU WA MBINGUNI yeye anauwezo wa kuziba majonzi moyoni mwako kwa upendo wake.jitaidi kuwa msomajiwa Biblia na vitabu mbalimbali, kutazama sinema na kukaa na marafiki isikae mwenyewe ili kupunguza mawazo.nataka uwe na moyo mkuu na ujasiri.tunakuombea kwa MUNGU WETU atakutia nguvu.
 
".....I ain't got no time to pretend that I'm not missin' You
Oh no no no no
I know You're in good hands the same hands that hold my heart
And I'll cherish every moment that we've spent
As a gift from God above for He takes care of all fragile hearts.."

Kipande toka Fragile hearts wa Yolanda Adams ukipata muda usikilize..,
Pole sana Mkuu
 
story yako imenitia uchungu na simanzi moyoni,mungu akutie nguvu na ujasiri pole sana mpendwa
 
Duh, nimelia aje? hii ni mipango ya mungu MESTOD yani wengine tunalia vitu vidogo vya masahibu ya mapenzi mwenzetu una zigo kubwa la matatizo na mawazo, mungu akutie nguvu sana mpendwa, haya yote ni mapito ya dunia lazima tuyapitie. muombee mungu marehemu huku ukijipa moyo na kuendelea na maisha, binadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni fupi sana nazo zimejaa misukosuko ya hapa na pale walipoandika haya hawakukosea.POLE SANA
 
Dedication mwimbo mpya wa lina, najuaaa kama umelala, na huwez amkaaaa, wewee. ila kufumba kwako macho..............
 
Duh, nimelia aje? hii ni mipango ya mungu MESTOD yani wengine tunalia vitu vidogo vya masahibu ya mapenzi mwenzetu una zigo kubwa la matatizo na mawazo, mungu akutie nguvu sana mpendwa, haya yote ni mapito ya dunia lazima tuyapitie. muombee mungu marehemu huku ukijipa moyo na kuendelea na maisha, binadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni fupi sana nazo zimejaa misukosuko ya hapa na pale walipoandika haya hawakukosea.POLE SANA

Ahsante Gaga. Lakini unajua tatizo ni tatizo tu. Huwezi kuwa na maumivu ya kichwa halafu mwenzio kakatwa mkono ukasema afadhali mimi kichwa kuliko yule kakatwa mkono. Maumivu yataumiza tu, haijalishi ukubwa wake.
 
Back
Top Bottom