Kama ni ndoto, mbona haiishi?

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,798
2,003
Ni saa sita na dk hamsini na moja usiku. Nimejiegesha kupata usingzi wa mang'amung'amu baada ya uchovu na mawazo mengi, simu nimeishika. Mara simu ina vibrate na kutoa mlio. Nashituka na kuona screen imeandika 'wife calling.....' 'Hallow', naitika. 'Wewe, umelala?', unanijibu. 'Hapana, nimejiegesha si unajua usingizi hauji?' (kwani nakumbuka mara ya mwisho nimeangalia saa ilikuwa saa sita na nusu), nakujibu na unanambia unajua. Unaanza kunambia njaa inakuuma sana na hauna nguvu, huna nguvu na hata manesi unawaita hawaji. Nafarijika kuona atleast unapata apettite ya kula na nakusihi uvumilie na kukuambia si unajua manesi wetu walivyo hasa hapo muhimbili? Nakusihi umuombe jirani yako ambaye kidogo ana nguvu akusaidie.

Unanambia huna nguvu nami nakuambia najua sababu toka umeanza kuumwa ni zaidi ya mwezi huli vizuri na ukila unatapika chakula chote. Unanambia kesho uje saa kumi na mbili kuninywesha uji. Nakuambia usijali mpenzi, nitakuja. Mara unanambia kata simu nguvu inaisha piga baadaye kidogo. Nakata bila kujibu lolote na nahisi kuchanganyikiwa. Naangalia call duration tumeongea kama dk 1.01. Nakaa kama dk kumi napiga tena. unapokea na kunishukuru kwa kukusaidia, nikakuambia usijali mama, Mungu atakuponya. Bado unasisitiza kuhusu kuwahi kukunywesha uji kesho nakuambua sawa, mara unanambia kata simu nguvu imeisha nakata simu. Naangalia call duration, tumeongea dk 2.02.

Nakaa macho na mara ya mwisho naangalia saa ni saa tisa unusu usiku. Nikiwa usingizini naota nikisema 'Mungu mponye, Mungu mponye....' huku machozi yanatoka. Nashituka na kuona ninatoa machozi kweli. Naangalia saa na kujiuliza ni nini hii? Ni saa kumi na dk 35. Naamua kuamka na kujiandaa ili nije kukunywesha uji. Natoka nyumbani saa kumi na moja unusu. Nikiwa mzunguko wa uhuru kariakoo, kaka yako anapiga simu ananambia, 'mzee, dada ameshatucha, amefariki aisee'. Nahisi kuchanganyikiwa, mbele sioni. Nafika sewahaji namba 10. Naona nesi anampa vitu vyako kaka kwenye mfuko wa plastic wa kijani. Naenda kitandani naona umefunikwa gubi gubi na wamezungushia mashuka ya kijani. Duh, kijani tena. Namkuta jirani yako, ananambia, pole kaka, muone huyo hapo. Nafunua shuka, nashika paji la uso, umeshapoa mpenzi umekuwa wa baridi. Nashika paji la uso wako, machozi yangu yanaanguka juu ya paji la uso wako. Nakuuliza 'd, huu ndo uji uliosema niwahi kukunywesha? Zile shukrani kumbe ndo Muumba alikuwa anakuita?' nakufunika na kutoka.

Jirani yako ananambia, 'kaka mwache mwenzio apumzike kwani alikuwa anaishi kwa mateso sana'. Namuuliza 'ilikuwaje usiku wa leo'? Akanambia aliongea na simu kama mara mbili hivi baadaye alisema, "MUNGU NAOMBA UNICHUKUE, LAKINI KABLA HUJANICHUKUWA NISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE". Akanambia ulirudia mara nyingi na baadaye kati ya saa kumi na saa kumi na moja ukatulia.

Mpenzi, yote yaliyotokea hata siamini, ni kama ndoto, kwamba haupo nami.
Lakini kama ni ndoto, mbona siamki? Inamaana ndoto hii naota tuu, toka January mpenzi? Kama ni ndoto mbona naenda kazini? Ishu zinazotokea mbona naziona na kuzisikia? Mabomu Gongo la Mboto, Babu Loliondo na kero zingine?

Maisha kwangu sasa ni taabu sana ni kama jana tuu, matukio yote yametokea. Sikuamini pale uliposhushwa kwenye nyumba yako nyingine na ya milele, mrembo wangu. Nakukumbuka sana mpenzi. Comitment zako za dhati, uaminifu, ucheshi, my dia. RIP MY SWEET MAMAA!
 
ndefu sana bwana. kweli mbona haiishi. tunapiga kazi huku tunapata threads muda mfupi.
 
Duuh!!pole kaka!

Mi hapa hadi machozi yanatoka..Mungu alimpenda zaidi.Let her R.I.P
 
sijaisoma kwa kuwa ni ndefu ila nimeona wengi wanakupa pole!!!Basi bwana POLE.duuh
 
Mestod, hii ni hadithi ama ni kweli yamekutokea (samahani nakuuliza hivi!)?

Yah, ni kweli. I lost her on 18th, and buried her on 21st Jan. Hii ni sehemu ndogo sana ya mwisho, ila ni mengi yalitokea hadi namzika na hadi leo siamini kama kweli kafariki. Ni kweli kabisa.
 
Yah, ni kweli. I lost her on 18th, and buried her on 21st Jan. Hii ni sehemu ndogo sana ya mwisho, ila ni mengi yalitokea hadi namzika na hadi leo siamini kama kweli kafariki. Ni kweli kabisa.

Pole sana japokuwa sijasoma. Umemzika mkeo kumbe pole sana duuuuhhh inauma mno
 
ndefu sana bwana. kweli mbona haiishi. tunapiga kazi huku tunapata threads muda mfupi.

Mkuu ningewza ningeifupisha. Lakini nashindwa na hapa nimeisummarise sana. Ila kama huna muda ipotezee. But ni kweli yamenitokea.
 
Yah, ni kweli. I lost her on 18th, and buried her on 21st Jan. Hii ni sehemu ndogo sana ya mwisho, ila ni mengi yalitokea hadi namzika na hadi leo siamini kama kweli kafariki. Ni kweli kabisa.

Jamani Mestod, ...niliposoma nilifikiri umetengeneza hadithi! Jamani....inaumiza mnoo!! Pole sana mkuu. Mungu akutie nguvu, akufariji na akuponye! Naelewa sio rahisi, ni Mungu tu ndo aweza kukuponya! POLE SANA!
 
POLE SANA,nimeisoma imeniuma sana,na hata hapa ninapoandika nimejifuta machozi.
hii ipo,tena kwa mtu aliekukaa moyoni,inakua ngumu sana kuamini na bado unaona ni ndoto.
hiyo ni kazi ya mungu nasi tunaelekea huko.imeniuma sana nimefanya imagination kama imenitokea mimi.POLE SANA.
 
Jamani Mestod, ...niliposoma nilifikiri umetengeneza hadithi! Jamani....inaumiza mnoo!! Pole sana mkuu. Mungu akutie nguvu, akufariji na akuponye! Naelewa sio rahisi, ni Mungu tu ndo aweza kukuponya! POLE SANA!

Thanks
 
pole my dear,,,, watakiwa kusema ina lillah waina ilayhy raj-uun,,,, kwani kila mmoja atarejea alipotoka,,, wewe ulimpenda lakini allah kampenda zaid,,,kinachotakiwa n kusahau yaliopita na kuangalia yajayo usikae ukajikumbusha na kujitia mawazo yatakuumiza,,,inshaAllah utafarijika na kumpata atakae kuliwaza.... pole kwa hilo,,mbele ni yake nyuma yetu inshaAllah..,
Yah, ni kweli. I lost her on 18th, and buried her on 21st Jan. Hii ni sehemu ndogo sana ya mwisho, ila ni mengi yalitokea hadi namzika na hadi leo siamini kama kweli kafariki. Ni kweli kabisa.
 
pole sana,mungu akutie nguvu,nimeumia sana mimi binafsi,mungu akusaidie na akuongoze,pole sana jamani uuuwi i cant even explain how i feel,pole sana
 
Thanks. She was my wife to be. Harusi ilikuwa iwe June this year na tuliisha anza maandalizi.

My Godness???!!! Du pole sana Mestod Mungu akupe faraja na nguvu. Mungu kampenda zaidi yetu Pole sana my Dear

Mie ilinishinda kusoma bana hukuweka hata paragraph nikaona kizunguzungu kumbe ni kitu cha maana na kinauma kiasi hiki siku nyingine weka angalau tuweze kusoma.
 
Ok, wakati naandika nilikuwa naishiwa hata nguvu ya kuendelea, lakini sababu niliishaamua kuitoa sikuweza kuacha. Kwa hiyo, kilichokuwa hewani ni kuandika na siyo mpangilio. Sorry for that.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom